Tujikumbushe Bar na Kumbi Maarufu Zilizotamba Miaka ya Nyuma

Mussolin5

JF-Expert Member
Apr 23, 2015
18,379
2,000
Wakuu wa jukwa kwema?

Leo nimeona sisi wahenga tujikumbushe zile Bar na Kumbi maarufu za starehe zilizotamba miaka ya nyuma ambazo leo hii hazipo tena au zimechuja kwa kiasi kikubwa sana.

Mi naanza na Silent Inn, miaka ile ya mwanzoni mwa 2000, ilikuwa iko vizuri ghafla ikapotea kwenye ramani, baadae nkasikia mmiliki ameokoka.

Miaka ile pia kipindi wasanii wanazindua albamu zao, nani ambaye hakuwahi kusikia Diamond Jubilee? Nakumbuka jinsi Juma Nature alivyozindua albamu yake ya Ugali na kujaza nyomi ya watu. Kuujaza ukumbi wa Diamond Jubilee ilihitaji uwe katika level za Juma Nature kwa miaka ile.

Ni ukumbi upi au Bar ipi unaikumbuka jinsi ilivyotesa miaka hiyo?
Karibuni....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom