Tukumbuke Kidogo: Is It Possible Today??

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,486
86,003
Naamini walio wengi (sio wote) mlisoma kitabu chenye Title " Is It Possible?" na kile kingine cha " This Time Tomorrow"
Basi siku moja Jamaa akawa anakanyatia kabinti kamoja ambako alikua anasoma nako sekondari za enzi hizo ambazo mnakutana likizo kwa likizo tu; kufika home Jamaa akamkuta Mzee (Baba wa Binti) ambaye ni mkali sana hasa linapokuja suala la mabinti zake.

Jamaa kuona hivyo akili ikamjia kichwani fasta akasalimia kwa heshima zote na akaomba kuonana na Jane (si jina halisi) kwani amefuata kitabu; Jane akaitwa huku wazazi wa binti wakiwepo; Jamaa akamuuliza Jane;

Jamaa: Hivi Jane una kile kitabu cha Literature cha " Is It Possible Today?" (Today aliiongezea tu ili kuweka mambo sawa)
Jane: mmh mbona hicho sina labda kile cha "This Time tomorrow"

Jamaa akawa ameshafikisha ujumbe kwa Jane na kuondoka salama usalimini eneo la tukio huku Mzee akiwasifia watoto hawa kwa kupenda kusoma; Mzazi kuwa makini
 
Mhhh, hiyo kali mkuu! Ujumbe umefika bila kushtukiwa! Iko poa.
Angeweza kuongezea kuwa: Ni vizuri kusoma "No longer at ease" ili tusijeshindwa kujibu maswali ya "the river between"!
 
I see mmenikumbusha mbali sana na hako kamtindo ila mm nilimjibu jamaa "NO LONGER AT EASE"
 
Mmegundua kuwa nyuma kutamu eee? Sasa msilalamike sana
 
Kwa wazee wa zamani hiyo sawa lakini siku hizi ungeshtukiwa(joke)
 
Back
Top Bottom