Tukubaliane, hatuna wimbo wa Taifa

aiseeeeeeeee kunakaukweli ndani yake acha kubisha bisha usichokijua
Baada ya kuchunguza bado nitasema mada si ya kweli. ..dah..barikiwa my friend
 
Tunes na lyrics ni moja ya misingi ya hatimiliki.

Sasa ukakopi tunes na kubadilisha lyrics kwa lugha ya Kikwenu, utakuwa bado umekopi kazi ya watu.

Ukweli upo pale pale. Wimbo ulikopiwa kutoka wimbo wa chama cha anc cha Afrika ya Kusini.

Haya ndiyo maoni hasi yasiyokuwa na ushahidi wowote zaidi ya hisia na conjectures tu.
Wimbo ule ulikuwa wa kanisani, haukuwa wa siasa, na wala haukuwa na hatimiliki yoyote ile, ndiyo maana ullimbwa katika lugha nyingi sana na hata Ulaya katika baadhi ya lugha za nchi za Scandinavia .
 
Samahani jamani, hivi kati ya Tanzania na SA ipi ilianza kupata uhuru wake
Shida si nani alitangulia kupata uhuru, bali ni asili ya wimbo. Kumbuka mwaka ambao wimbo huu umetungwa na kuimbwa hadharani kwa mara ya kwanza, hata Tz ilikuwa haijapata uhuru. Kwahiyo kinachotazamwa hapo in asili ya wimbo kwa maana ya maali ulipoanzia.
 
Polepole mkuu, ukisema huu wimbo ulikuwa wa kanisani utasababisha wale wanaharakati wa imani ya upande wa pili waanze mchakato wa kuupinga.
 
Hii makala hawajaisoma wamekimbilia kuchangia na kukosoa,.
 
Acheni upotoshaji kwa watu, licha ya kutoa mlolongo wa historia lakini jua yafuatayo:-
1.nchi nyingi za kiafrika zilishirikiana kwa karibu sana katika kudai na kupambania uhuru hivyo zikawa na ufanano mkubwa kuanzia nyimbo zao mpaka falsafa za kitaifa. Mfano wimbo huu wa taifa letu ulitungwa mara ya kwanza na ENOCH SONTONGA wa Afrika kusini lakini ulitumiwa na mataifa mengi kama Angola, South Africa, Tanzania (tanganyika), na nyinginezo hasa za kusini mwa afrika ikiwemo Tanzania.

2. Wimbo wa taifa la Tanzania ni dua na ni uamsho wa kuwaweka waafrika kuwa pamoja katika kudai haki zao hasa kipindi cha mkoloni, kwa hiyo falsafa ya Tanzania haikuwa tofauti na ile ya Angola, South Africa au Mozambique kwani lengo lilikuwa ni ukombozi, mfano hapa Tanzania maeneo kama Mazimbu (sua) zilikuwa ni kambi za watu wa South Africa wakijifunza mbinu za kijeshi chini ya Tanzania kwenda kupigania uhuru kwao hivyo hata wimbo wa taifa haukuwa na utofauti kwani adhima yao ni moja(same aspirations)

3.wimbo wa taifa letu ni kielelezo cha umoja na dua inayo/iliyowaunganisha waafrika kudai uhuru pamoja na adhima ya kuunda afrika yenye umoja(serikali moja) kwa msukumo wa falsafa ya Kwame Nkurumah, J. K. Nyerere na Muammar Gaddafi hivyo kwa nchi za kusini mwa afrika zilikuwa na lengo moja hivyo hata wimbo ulibeba adhima moja ya kiujumla
HITIMISHO: Mantiki ya ukosoaji na uibuaji wa hoja za kuutazama wimbo wetu wa taifa kama sio wetu ni mwelekeo mbaya kwani kuna watu watahoji kuwa kumbe kigoma siyo Tanzania ni Burundi, au au Ruvuma ni msumbiji, n.k lakini tuelewe kuwa wimbo wa taifa letu ni moja ya alama ya taifa letu tulioipokea kutoka kwa waasisi wetu, kuwa na mlolongo wa historia yake sio tatizo.
 
Naona Goodluck Mtenga umehamishia majeshi jf toka fb BREAKING NEWS
 
wimbo wa taifa ni wetu na una lugha yetu mana SA hawaimbi kiswahili,so ni wa kwetu na sioni tatzo kutafsiri.hata wao bendera yao ni copy toka kwetu TZ.Ni ushirikiano tuu kati ya nchi,wimbo ni mzuri kuwa wa taifa.kwanza vazi la taifa limeishia wapi?
 
kwa hoja hiyo nakubaliana ZA hawana tune yao,japokuwa wana wimbo
 
Jf sikuhizi niya kimwendo kasi tu. Mtu katoa hoja, kaweka na historia kama "suporting evidence" inawezekana hoja yake ni ya kitoto au inasukumwa na kitu flani. Nyinyi mliokula chumvi nyingi au kupata kuifahamu saidieni kuweka kumbu kumbu sawa. Mambo ya kuzungusha mikono au kusoma namba hapa siyo ya muhimi sana. Ingawa ukweli ni kuwa, historia ya wimbo wa taifa haijaelezewa kwa kina katika vitabu vya uraia/historia ukilinganisha na historia ya Dr livingstone.
 
Nadhan jamaa huna uzalendo tu manake tz ndo watunzi ndo wakwanza kupata uhuru kwa mara ya kwanza uliimbwa 1961 waat south haipo kwwnye raman kabisaaaa
Wimbo huu ulitungwa na huyu Enoch Sontonga,lkn Tanzania ilikuwa nchi ya kwanza kuutumia kama wimbo wake wa Taifa
 
Kama lengo la wimbo huu ilikukwa ni kuwaamsha waafrika kudai uhuru, sasa kwanini tunaendelea kuuimba wakati uhuru umeshapatikana kwa mataifa yote ya Afrika? Na kama lengo la pili ni kuhamasisha kuwa na serikali moja kama ilivyokuwa falsafa ya Kwame Nkurumah na wengineo, tunawezaje kuendelea kuhamasisha hilo wakati sisi wenyewe hapa Tanzania tumeshindwa kuunda serikali moja na tumebaki kung'ang'ania mbili? Kama hizo ndizo hoja, basi ina maana wimbo huu kwa sasa hautufai, tubadilishe na kuwa na mwingine utakaoendana na adhma yetu kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…