Tukubaliane, hatuna wimbo wa Taifa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
KUMEKUWAPO na mjadala kwamba Watanzania hatuna wimbo wa taifa. Mjadala huu upo ndani na nje ya nchi yetu. Unashirikisha Watanzania na wasio Watanzania, anaandika Ansbert Ngurumo.

Kuhusu suala hili, nakumbuka niliwahi kubanwa na baadhi ya raia waSwaziland na Lesotho, mwaka 2001 nikiwa jijini Mbabane kwa mafunzo mafupi ya uchambuzi wa kisiasa.

Tulikuwa kundi la waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika Kusini mwa Sahara. Watanzania tulikuwa wawili – mimi, na Mayage S. Mayage, wakati huo nikiwa naandikia magazeti ya The African na Rai.

Katika shamrashamra za hapa na pale, siku moja wakati wa mapumziko, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, raia wa Lesotho, akapendekeza kila watu waimbe wimbo wao wa taifa. Likaonekana ni jambo jema, kila mtu ajivunie utaifa wake na nchi yake mbele ya wenzake.

Kila wimbo ulipoimbwa, ulihitimishwa kwa makofi ya shangwe na (wakati mwingine) vigelegele kutoka kwa akina dada waliokuwapo. Tulikuwa tunaimba kwa mzunguko. Ilipofika zamu ya Tanzania, tukaanza kuimba kwa mbwembwe.

Hatukumaliza hata ubeti wa kwanza. Mara tukakatizwa na mmoja wa wasikilizaji wetu, akisema, “samahani, tumesema Tanzania. Sasa mbona mnaimba wimbo wa Afrika Kusini? Hamjui utaifa wenu nini?” Kabla hatujajibu, mwingine akadakia: “Hapana, huu wimbo ni wa Zambia. Hebu tuimbieni wimbo wenu.” Wengine wakacheka kama vile wanataka kutuzomea.

Nikakaribia kuwakasirikia, lakini nikawaeleza kwa upole kuwa hoja zao zinaonesha walivyo “washamba” kwa kushindwa kujua kuwa tunachoimba si wimbo wa Afrika Kusini wala wa Zambia, bali wa Tanzania. Nikawaeleza kwamba wangetuacha kwanza tukaumaliza ndipo waufananishe na hizo wanazozungumzia.

Nikawataka waelewe kwamba nyimbo kufanana tuni si kosa, bali ni sehemu ya, na zao la, umoja wa dhamira ya mapambano na ukombozi wa bara letu.

Nikasema kuwa na wimbo unaofanana ni sifa si kejeli; ni kama kuwa na lugha moja inayowafananisha Waafrika na kuonesha udugu na mshikamamo ambao Waafrika wanahitaji sasa, labda kuliko wakati wowote wa historia yao.

“Sawa. Lakini haiondoi kwamba wimbo huo unajulikana ni wa Afrika Kusini. Nyie mmeunakili. Mna hakimiliki?” Alihoji mmoja wao.

Hata hivyo walio wengi waliona mantiki katika hoja yangu ya “kulazimisha.” Nililazimisha hoja hiyo kutetea wimbo wetu, kwa sababu sikuwa na sababu ya kuonesha unyonge wa Watanzania mbele ya raia wa nchi nyingine.

Nilitimiza azima hiyo, lakini dhamiri yangu ilikuwa inaniambia kwamba, “vijana hawa wana hoja.” Bahati niliyokuwa nayo ni kwamba sikukutana na mmoja wao mwenye hoja kali.

Walikuwa na ubishi tu, na waliridhika haraka haraka na maelezo yangu ya juu juu na ya kulazimisha. Labda mjadala ungekuwa mkali na mrefu kama wangehoji zaidi, maana sikuwa tayari kushindwa kueleza kwa nini Watanzania hatuna wimbo wetu.

Hoja hii imekuwa ikijadiliwa pia na baadhi ya wanasiasa wetu, hasa walio katika vyama visivyo madarakani.

Nakumbuka kipindi fulani, akina Bob Makani (wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo) na Freeman Mbowe (katika awamu ya kwanza ya ubunge wake wa Jimbo la Hai), waliwahi kuvalia njuga suala la wimbo wa taifa.

Wapo baadhi ya wanaharakati, wakiwamo waandishi wa habari, walikubaliana nao. Sababu ni zile zile kwamba hatuna wimbo wetu. Tumeazima.

Walifika mahali pa kusema kwamba, Chadema kikiingia madarakani, watabadili wimbo wa taifa kwa sababu huu uliopo hauna mvuto na hausisitizi utaifa. Wakapendekeza tubadili wimbo, badala ya huu wa sasa, tuimbe “Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote…”

Naamini viongozi wetu, kama ilivyo kawaida ya viongozi wa Afrika, waliona suala hilo ni la wapinzani, na ni la kipinzani.

Sijawahi kusikia viongozi wetu wakilijadili. Sijawahi kusikia hata mbunge mmoja wa CCM akinukuliwa kutoa hoja hiyo kwenye vikao vya uamuzi.

Na zikiimbwa nyimbo zote mbili (Mungu Ibariki Afrika; na Tanzania nakupenda kwa moyo wote), ni dhahiri kwamba huu wa pili ndio unasikika na kuhisiwa wa kizalendo kwetu. Ni wimbo wetu.

Zaidi ya hayo, kwa sababu ya ukubwa wa Afrika Kusini na umaarufu wake katika dunia, wimbo wake umefunika wimbo wetu. Siku zikutanapo timu za taifa, au viongozi wetu wanapotembeleana, zikipigwa nyimbo hizo, ndipo ukweli huu unapogundulika. Tumeiga.

Kwa faida tu ya wasomaji, ngoja nieleze historia fupi ya wimbo huu. Katika dunia nzima, hasa Afrika Kusini kwenyewe ulikoanzia, unajulikana kama “Nkosi Sikelel’ iAfrika” – maneno ya lugha ya ki-Xhosa, yenye maana ya “Mungu Ibariki Afrika.”

Mtunzi wake anaitwa Enoch Sontonga, aliyekuwa mwalimu katika shule moja ya misheni ya Kimethodisti, Johannesburg, Afrika Kusini.

Aliutunga ukiwa kama utenzi mwaka 1897. Uliimbwa kwa mara ya kwanza hadharani mwaka 1899 katika ibada ya kuwekwa wakfu mchungaji Boweni, wa Kanisa la Methodist.

Kwaya ya Sontonga na kwaya nyinginezo zikawa zinauimba mara kwa mara katika matukio jijini Johannesburg na Natal. Watu wakaupenda.

Mnamo Januari 8, mwaka 1912, katika mkutano wa kwanza wa Chama cha Wazawa wa Afrika Kusini (SANNC), mtangulizi wa ANC, wimbo huo uliimbwa mara baada ya sala ya kufunga mkutano.

Mwaka 1925, ANC ikauchukua kama wimbo wake rasmi ulioimbwa mwishoni mwa mikutano yake. Tangu hapo, wimbo huo umejulikana nje ya Bara la Afrika kama wimbo wa ANC, kwani ulikuwa ukiimbwa katika mikutano ya ANC katika harakati za ukombozi.

Harakati hizo ndizo zilifikisha wimbo huo hadi kwetu. Nasi tulipopata uhuru, tukauchukua kama wimbo wa taifa, tukautafsiri kwa Kiswahili, tukapunguza baadhi ya aya na kuubakiza kama ulivyo leo.

Zambia nao walifanya hivyo. Namibia pia waliutumia. Zimbabwe nao waliuiga, lakini baadaye “walipopata akili” wakautema, wakatunga wimbo wao.

Kwa kipindi kirefu, Afrika Kusini ilikuwa na “nyimbo mbili za taifa.” Mmoja ulijulikana kama wimbo rasmi na mwingine, usio rasmi.

Wimbo rasmi (uliotumiwa na serikali ya makaburu) uliitwa kwa jina la Die Stem (ki-Afrikaans), yaani Wito wa Afrika Kusini; na usio rasmi (uliotumiwa za wanaharakati wa ANC), ndio huo Mungu Ibariki Afrika.

Siku ANC iliposhinda uchaguzi wa kwanza kidemokrasia mwaka 1994, nyimbo hizo mbili zikatangazwa kuwa nyimbo rasmi za taifa, lakini mwaka 1996 ziliunganishwa; yakachukuliwa maneno huku na huku, ghani ikabaki ile ile ya wimbo wa ANC, ukakarabatiwa na kuwa kama ulivyo leo.

Kwa Afrika Kusini, Nkosi Sikelel’ iAfrika, kabla na baada ya uhuru, ni ishara ya uhuru na mapambano ya ukombozi wao. Unaimbwa katika lugha mbalimbali Kixhosa, Kiingereza, Kisesotho na Kiafrikaans.

Maneno yaliyo katika aya ya kwanza yaliandikwa na mtunzi mwenyewe (Enoch) katika lugha yake ya Xhosa. Mwaka 1927, aliyekuwa mmoja wa washairi maarufu wa nchi hiyo, Samuel Mqhayi, aliongeza aya nyingine saba katika lugha hiyo hiyo.

Kabla ya hapo, mwaka 1923, Solomon Plaatje, mmoja wa waandishi mahiri nchini humo, ambaye pia alikuwa miongoni mwa waasisi wa ANC, ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuurekodi wimbo huo katika studio jijini London, akisindikizwa na muziki wa piano uliopigwa na Sylvia Colenso.

Mwaka huo huo, kiwanda cha uchapaji cha Lovedale Press, katika Jimbo la Eastern Cape, kilichapisha nakala yenye aya zote katika kijitabu. Juni 11, 1927, wimbo huo ulichapishwa katika gazeti la Umtetela Wa Bantu, ukaingizwa pia katika kitabu cha ushairi cha Kixhosa kwa ajili ya kuwafundishia watoto shuleni.

Wimbo huo pia uliingizwa rasmi katika kitabu cha nyimbo za Kixhosa kwenye Kanisa la Wapresbyteri kilichojulikana kama Ingwade Yama-culo Ase-rabe, mwaka 1929. Mwaka 1942, Moses Mphahlele, alichapisha nakala nyingine za wimbo huo katika lugha hiyo na kuzisambaza ili umma ukariri vema maneno yake.

Kwaya ya Ohlange Zulu, ya Mchungaji John L. Dube, ndiyo iliyokuza wimbo huo, kwa kuuimba mara kwa mara katika matamasha mbalimbali jijini Johannesburg.

Taratibu ukawa wimbo maarufu katika mikusanyiko ya kidini, kijamii na kisiasa; badaye ukarekodiwa pia na wasanii kina Ladysmith, Black Mambazo, Boom Shaka na Mahotella Queens.

Historia hiyo pekee inaonesha kwamba sisi bado hatuna wimbo. Kama tunavyoimbiwa na wasanii wa CCM kwamba “CCM ina wenyewe,” basi tuna sababu ya kuamini pia kwamba hata wimbo huu tunaouita wa taifa, una wenyewe – na wenyewe ni Afrika Kusini. Nadhani Wazimbabwe waliligundua hilo mapema. Wakaachana nao. Sisi tunangoja nini?

Ni bahati mbaya kwamba vijana wale waliobishana nami hawakuwa wanajua historia ya wimbo huo kama nilivyoieleza hapa. Vinginevyo, walikuwa na hoja; na wangetuaibisha. Tuna wasanii wa kutosha kutunga nyimbo zetu.

Watunge. Kama hatutaki mpya, basi tuchukue zilizopo, zinazoeleza kwa kina historia na utaifa wetu, tuzifanye rasmi nyimbo zetu za taifa, kwani huu tunaoimba sasa si wimbo wetu.
 
SA Africa baada ya kupata uhuru chini ya mandela alikuwa hana uzoefu, kuna maafisa wa Tz waliopelekwa na serikali ya Tz kwa ajili ya maandalizi ya mandela kuchukua nchi, hata kutoa muongozo kwa mandela hata baada ya kuwa raisi. Baadhi ya vitu ambavyo walivifanya ni pamoja na kutoa mafunzo ya maandalizi ya siku ya kuapishwa kwa raisi mandela, kujifunza nyimbo zao za Taifa, bendera, bendi ,kutoa mafunzo ya awali kwa police/jeshi, gwaride na nk, mfano wimbo wa Taifa la Tanzania ulitolewa kwao ili waweze ku update , ili wapate wimbo wao wa SA, kilichofanyika wao SA badala ya ku update wakachukua kama ulivyo wakauweka katika lugha yao na kuimba kama ulivyo. Kwa nini huu wimbo wa Tz kwa sasa chimbuko lake linaonekana limetoka SA? kwanza SA imeendelea, watu wengi wako more aware kuhusu SA kuliko Tz, pili watu wengi wako aware na zaidi kuhusu story za SA na wanafuatilia mambo mengi ya SA kuliko Tanzania. Pili SA ina uwakilishi mkubwa kimichezo zaidi ya Tanzania ( rugby, Olympic, soccer, ) na kila wanapofanya hizo activities wimbo huimbwa na kujulikana. Tanzania haikucopy wimbo huu kutoka SA maana sisi tulipata uhuru mapema na tukaandika wimbo wetu kabla yao.
 
Komredi, wewe na wenzio mlikuwa mmevimbewa mkaanza leta vitu visivyo na tija na lililokuwa limewakutanisha, na hilo ndio unalojaribu lileta jamvini...!
...kwamba jamhuri ya muungano haina wimbo wa taifa?..."niwie radhi, ni imani nayoipigia saluti ya kidole cha kati"
 
Huyu ana agenda yake. Nitarudi tena atakapojibainisha kile anataka. Maana nakifahamu. Nitarudi akijiweka bayana. Upumbavu huu utaisha lini?
 
SA Africa baada ya kupata uhuru chini ya mandela alikuwa hana uzoefu, kuna maafisa wa Tz waliopelekwa na serikali ya Tz kwa ajili ya maandalizi ya mandela kuchukua nchi, hata kutoa muongozo kwa mandela hata baada ya kuwa raisi. Baadhi ya vitu ambavyo walivifanya ni pamoja na kutoa mafunzo ya maandalizi ya siku ya kuapishwa kwa raisi mandela, kujifunza nyimbo zao za Taifa, bendera, bendi ,kutoa mafunzo ya awali kwa police/jeshi, gwaride na nk, mfano wimbo wa Taifa la Tanzania ulitolewa kwao ili waweze ku update , ili wapate wimbo wao wa SA, kilichofanyika wao SA badala ya ku update wakachukua kama ulivyo wakauweka katika lugha yao na kuimba kama ulivyo. Kwa nini huu wimbo wa Tz kwa sasa chimbuko lake linaonekana limetoka SA? kwanza SA imeendelea, watu wengi wako more aware kuhusu SA kuliko Tz, pili watu wengi wako aware na zaidi kuhusu story za SA na wanafuatilia mambo mengi ya SA kuliko Tanzania. Pili SA ina uwakilishi mkubwa kimichezo zaidi ya Tanzania ( rugby, Olympic, soccer, ) na kila wanapofanya hizo activities wimbo huimbwa na kujulikana. Tanzania haikucopy wimbo huu kutoka SA maana sisi tulipata uhuru mapema na tukaandika wimbo wetu kabla yao.

Acha uongo wewe, Kwanza unaonekana history ya south Africa hujui baada ya apartheid regime kuangushwa kwenye uchaguzi hakuna Kilichobadilika majeshi ni Yale Yale, uongozi wa nchi ndio uliobadilika, kumbuka kuwa Mandela alikua na uzoefu mzuri tuu maana alishakaa kwenye transition government for 5 years, makaburu walishajua kuwa ipo siku watatoka madarakani ndio maana waliwaaanda watu weusi kuongoza nchi, kilichochelewesha Mandela na wenzake wasipewe nchi mapema ni vinu vya nyulkia ambavyo South Africa ilikua inamiliki na hivi Declerk alikua hawaamini Akina Mandela walikua allied na viongozi Kama Gaddafi etc hivo hizi silaha zingeweza kuangukia mikononi mwao hivi ilibidi vinu viharibiwe Kwanza then ndio wakaja kupewa nchi.
 
Ubaguzi wa imani na assumtion kuwa wimbo wetu unafavor din flan ndo upumbavu wa mleta uzi huu.

ujinga na upumbavu wakiimani ukimvaa mtu hujiona anaonewa kwakila jambo. kisha kuzusha yakijinga kwanjia yoyote yakifedhuri akitafuta kuungwa mkono na wapumbuvu wenzake.

Mungu ibariki TANZANIA, Dumisha uhuru na amani .....
 
KUMEKUWAPO na mjadala kwamba Watanzania hatuna wimbo wa taifa. Mjadala huu upo ndani na nje ya nchi yetu. Unashirikisha Watanzania na wasio Watanzania, anaandika Ansbert Ngurumo.

Kuhusu suala hili, nakumbuka niliwahi kubanwa na baadhi ya raia waSwaziland na Lesotho, mwaka 2001 nikiwa jijini Mbabane kwa mafunzo mafupi ya uchambuzi wa kisiasa.

Tulikuwa kundi la waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika Kusini mwa Sahara. Watanzania tulikuwa wawili – mimi, na Mayage S. Mayage, wakati huo nikiwa naandikia magazeti ya The African na Rai.

Katika shamrashamra za hapa na pale, siku moja wakati wa mapumziko, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, raia wa Lesotho, akapendekeza kila watu waimbe wimbo wao wa taifa. Likaonekana ni jambo jema, kila mtu ajivunie utaifa wake na nchi yake mbele ya wenzake.

Kila wimbo ulipoimbwa, ulihitimishwa kwa makofi ya shangwe na (wakati mwingine) vigelegele kutoka kwa akina dada waliokuwapo. Tulikuwa tunaimba kwa mzunguko. Ilipofika zamu ya Tanzania, tukaanza kuimba kwa mbwembwe.

Hatukumaliza hata ubeti wa kwanza. Mara tukakatizwa na mmoja wa wasikilizaji wetu, akisema, “samahani, tumesema Tanzania. Sasa mbona mnaimba wimbo wa Afrika Kusini? Hamjui utaifa wenu nini?” Kabla hatujajibu, mwingine akadakia: “Hapana, huu wimbo ni wa Zambia. Hebu tuimbieni wimbo wenu.” Wengine wakacheka kama vile wanataka kutuzomea.

Nikakaribia kuwakasirikia, lakini nikawaeleza kwa upole kuwa hoja zao zinaonesha walivyo “washamba” kwa kushindwa kujua kuwa tunachoimba si wimbo wa Afrika Kusini wala wa Zambia, bali wa Tanzania. Nikawaeleza kwamba wangetuacha kwanza tukaumaliza ndipo waufananishe na hizo wanazozungumzia.

Nikawataka waelewe kwamba nyimbo kufanana tuni si kosa, bali ni sehemu ya, na zao la, umoja wa dhamira ya mapambano na ukombozi wa bara letu.

Nikasema kuwa na wimbo unaofanana ni sifa si kejeli; ni kama kuwa na lugha moja inayowafananisha Waafrika na kuonesha udugu na mshikamamo ambao Waafrika wanahitaji sasa, labda kuliko wakati wowote wa historia yao.

“Sawa. Lakini haiondoi kwamba wimbo huo unajulikana ni wa Afrika Kusini. Nyie mmeunakili. Mna hakimiliki?” Alihoji mmoja wao.

Hata hivyo walio wengi waliona mantiki katika hoja yangu ya “kulazimisha.” Nililazimisha hoja hiyo kutetea wimbo wetu, kwa sababu sikuwa na sababu ya kuonesha unyonge wa Watanzania mbele ya raia wa nchi nyingine.

Nilitimiza azima hiyo, lakini dhamiri yangu ilikuwa inaniambia kwamba, “vijana hawa wana hoja.” Bahati niliyokuwa nayo ni kwamba sikukutana na mmoja wao mwenye hoja kali.

Walikuwa na ubishi tu, na waliridhika haraka haraka na maelezo yangu ya juu juu na ya kulazimisha. Labda mjadala ungekuwa mkali na mrefu kama wangehoji zaidi, maana sikuwa tayari kushindwa kueleza kwa nini Watanzania hatuna wimbo wetu.

Hoja hii imekuwa ikijadiliwa pia na baadhi ya wanasiasa wetu, hasa walio katika vyama visivyo madarakani.

Nakumbuka kipindi fulani, akina Bob Makani (wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo) na Freeman Mbowe (katika awamu ya kwanza ya ubunge wake wa Jimbo la Hai), waliwahi kuvalia njuga suala la wimbo wa taifa.

Wapo baadhi ya wanaharakati, wakiwamo waandishi wa habari, walikubaliana nao. Sababu ni zile zile kwamba hatuna wimbo wetu. Tumeazima.

Walifika mahali pa kusema kwamba, Chadema kikiingia madarakani, watabadili wimbo wa taifa kwa sababu huu uliopo hauna mvuto na hausisitizi utaifa. Wakapendekeza tubadili wimbo, badala ya huu wa sasa, tuimbe “Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote…”

Naamini viongozi wetu, kama ilivyo kawaida ya viongozi wa Afrika, waliona suala hilo ni la wapinzani, na ni la kipinzani.

Sijawahi kusikia viongozi wetu wakilijadili. Sijawahi kusikia hata mbunge mmoja wa CCM akinukuliwa kutoa hoja hiyo kwenye vikao vya uamuzi.

Na zikiimbwa nyimbo zote mbili (Mungu Ibariki Afrika; na Tanzania nakupenda kwa moyo wote), ni dhahiri kwamba huu wa pili ndio unasikika na kuhisiwa wa kizalendo kwetu. Ni wimbo wetu.

Zaidi ya hayo, kwa sababu ya ukubwa wa Afrika Kusini na umaarufu wake katika dunia, wimbo wake umefunika wimbo wetu. Siku zikutanapo timu za taifa, au viongozi wetu wanapotembeleana, zikipigwa nyimbo hizo, ndipo ukweli huu unapogundulika. Tumeiga.

Kwa faida tu ya wasomaji, ngoja nieleze historia fupi ya wimbo huu. Katika dunia nzima, hasa Afrika Kusini kwenyewe ulikoanzia, unajulikana kama “Nkosi Sikelel’ iAfrika” – maneno ya lugha ya ki-Xhosa, yenye maana ya “Mungu Ibariki Afrika.”

Mtunzi wake anaitwa Enoch Sontonga, aliyekuwa mwalimu katika shule moja ya misheni ya Kimethodisti, Johannesburg, Afrika Kusini.

Aliutunga ukiwa kama utenzi mwaka 1897. Uliimbwa kwa mara ya kwanza hadharani mwaka 1899 katika ibada ya kuwekwa wakfu mchungaji Boweni, wa Kanisa la Methodist.

Kwaya ya Sontonga na kwaya nyinginezo zikawa zinauimba mara kwa mara katika matukio jijini Johannesburg na Natal. Watu wakaupenda.

Mnamo Januari 8, mwaka 1912, katika mkutano wa kwanza wa Chama cha Wazawa wa Afrika Kusini (SANNC), mtangulizi wa ANC, wimbo huo uliimbwa mara baada ya sala ya kufunga mkutano.

Mwaka 1925, ANC ikauchukua kama wimbo wake rasmi ulioimbwa mwishoni mwa mikutano yake. Tangu hapo, wimbo huo umejulikana nje ya Bara la Afrika kama wimbo wa ANC, kwani ulikuwa ukiimbwa katika mikutano ya ANC katika harakati za ukombozi.

Harakati hizo ndizo zilifikisha wimbo huo hadi kwetu. Nasi tulipopata uhuru, tukauchukua kama wimbo wa taifa, tukautafsiri kwa Kiswahili, tukapunguza baadhi ya aya na kuubakiza kama ulivyo leo.

Zambia nao walifanya hivyo. Namibia pia waliutumia. Zimbabwe nao waliuiga, lakini baadaye “walipopata akili” wakautema, wakatunga wimbo wao.

Kwa kipindi kirefu, Afrika Kusini ilikuwa na “nyimbo mbili za taifa.” Mmoja ulijulikana kama wimbo rasmi na mwingine, usio rasmi.

Wimbo rasmi (uliotumiwa na serikali ya makaburu) uliitwa kwa jina la Die Stem (ki-Afrikaans), yaani Wito wa Afrika Kusini; na usio rasmi (uliotumiwa za wanaharakati wa ANC), ndio huo Mungu Ibariki Afrika.

Siku ANC iliposhinda uchaguzi wa kwanza kidemokrasia mwaka 1994, nyimbo hizo mbili zikatangazwa kuwa nyimbo rasmi za taifa, lakini mwaka 1996 ziliunganishwa; yakachukuliwa maneno huku na huku, ghani ikabaki ile ile ya wimbo wa ANC, ukakarabatiwa na kuwa kama ulivyo leo.

Kwa Afrika Kusini, Nkosi Sikelel’ iAfrika, kabla na baada ya uhuru, ni ishara ya uhuru na mapambano ya ukombozi wao. Unaimbwa katika lugha mbalimbali Kixhosa, Kiingereza, Kisesotho na Kiafrikaans.

Maneno yaliyo katika aya ya kwanza yaliandikwa na mtunzi mwenyewe (Enoch) katika lugha yake ya Xhosa. Mwaka 1927, aliyekuwa mmoja wa washairi maarufu wa nchi hiyo, Samuel Mqhayi, aliongeza aya nyingine saba katika lugha hiyo hiyo.

Kabla ya hapo, mwaka 1923, Solomon Plaatje, mmoja wa waandishi mahiri nchini humo, ambaye pia alikuwa miongoni mwa waasisi wa ANC, ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuurekodi wimbo huo katika studio jijini London, akisindikizwa na muziki wa piano uliopigwa na Sylvia Colenso.

Mwaka huo huo, kiwanda cha uchapaji cha Lovedale Press, katika Jimbo la Eastern Cape, kilichapisha nakala yenye aya zote katika kijitabu. Juni 11, 1927, wimbo huo ulichapishwa katika gazeti la Umtetela Wa Bantu, ukaingizwa pia katika kitabu cha ushairi cha Kixhosa kwa ajili ya kuwafundishia watoto shuleni.

Wimbo huo pia uliingizwa rasmi katika kitabu cha nyimbo za Kixhosa kwenye Kanisa la Wapresbyteri kilichojulikana kama Ingwade Yama-culo Ase-rabe, mwaka 1929. Mwaka 1942, Moses Mphahlele, alichapisha nakala nyingine za wimbo huo katika lugha hiyo na kuzisambaza ili umma ukariri vema maneno yake.

Kwaya ya Ohlange Zulu, ya Mchungaji John L. Dube, ndiyo iliyokuza wimbo huo, kwa kuuimba mara kwa mara katika matamasha mbalimbali jijini Johannesburg.

Taratibu ukawa wimbo maarufu katika mikusanyiko ya kidini, kijamii na kisiasa; badaye ukarekodiwa pia na wasanii kina Ladysmith, Black Mambazo, Boom Shaka na Mahotella Queens.

Historia hiyo pekee inaonesha kwamba sisi bado hatuna wimbo. Kama tunavyoimbiwa na wasanii wa CCM kwamba “CCM ina wenyewe,” basi tuna sababu ya kuamini pia kwamba hata wimbo huu tunaouita wa taifa, una wenyewe – na wenyewe ni Afrika Kusini. Nadhani Wazimbabwe waliligundua hilo mapema. Wakaachana nao. Sisi tunangoja nini?

Ni bahati mbaya kwamba vijana wale waliobishana nami hawakuwa wanajua historia ya wimbo huo kama nilivyoieleza hapa. Vinginevyo, walikuwa na hoja; na wangetuaibisha. Tuna wasanii wa kutosha kutunga nyimbo zetu.

Watunge. Kama hatutaki mpya, basi tuchukue zilizopo, zinazoeleza kwa kina historia na utaifa wetu, tuzifanye rasmi nyimbo zetu za taifa, kwani huu tunaoimba sasa si wimbo wetu.

kutoka mwandishi wa magazeti ya The African na Rai, hadi mleta umbea jf pole sana
 
Mleta mada ameweka historia ya wimbo. Mnaopinga ukweli wake weken historia ya wimbo wetu na mtunz nani!!
Haiwezekan kitu cha kitaifa kisiwe na kumbukumbu!! Vinginevyo mleta mada yuko sahihi na tutafute wimbo wetu
Wewe pia unatuambia, na unataka tuamini kuwa ati hatuna wimbo wetu wa taifa.....
...kwamba ni melody ya asili ktk kusini mwa afrika ndi sababu kuwa ati hatuna wimbo wa taifa?
Kinyesi!
Acha uongo wewe, Kwanza unaonekana history ya south Africa hujui baada ya apartheid regime kuangushwa kwenye uchaguzi hakuna Kilichobadilika majeshi ni Yale Yale, uongozi wa nchi ndio uliobadilika, kumbuka kuwa Mandela alikua na uzoefu mzuri tuu maana alishakaa kwenye transition government for 5 years, makaburu walishajua kuwa ipo siku watatoka madarakani ndio maana waliwaaanda watu weusi kuongoza nchi, kilichochelewesha Mandela na wenzake wasipewe nchi mapema ni vinu vya nyulkia ambavyo South Africa ilikua inamiliki na hivi Declerk alikua hawaamini Akina Mandela walikua allied na viongozi Kama Gaddafi etc hivo hizi silaha zingeweza kuangukia mikononi mwao hivi ilibidi vinu viharibiwe Kwanza then ndio wakaja kupewa nchi.
 
dah! maandishi yote kumbe ni uwongo...bado nusu ningemwamini mtoa mada, kumbe uwongo!
 
Kwani kuna tatizo gani kuiga kitu cha Mwafrika mwenzetu? Mbona hausemi kwamba Tanzania hatuna Sheria zetu wenyewe kwa maana zote ni British common law? Au kwa kuwa tumeiga kwa Mzungu ni sawa ila kuiga kwa Mwafrika mwenzetu unataka kupinga?
 
Acha uongo wewe, Kwanza unaonekana history ya south Africa hujui baada ya apartheid regime kuangushwa kwenye uchaguzi hakuna Kilichobadilika majeshi ni Yale Yale, uongozi wa nchi ndio uliobadilika, kumbuka kuwa Mandela alikua na uzoefu mzuri tuu maana alishakaa kwenye transition government for 5 years, makaburu walishajua kuwa ipo siku watatoka madarakani ndio maana waliwaaanda watu weusi kuongoza nchi, kilichochelewesha Mandela na wenzake wasipewe nchi mapema ni vinu vya nyulkia ambavyo South Africa ilikua inamiliki na hivi Declerk alikua hawaamini Akina Mandela walikua allied na viongozi Kama Gaddafi etc hivo hizi silaha zingeweza kuangukia mikononi mwao hivi ilibidi vinu viharibiwe Kwanza then ndio wakaja kupewa nchi.

1) SA wamekuwa na wimbo wao hata kabla ya mwaka 1994, huo wimbo ni tofauti kabisa na wimbo wa "sasa Nkosi sekelel", so SA tu hata bongo kabla ya uhuru kulikuwa na song tofauti kabisa sijui mungu msaidie malkia kama sikosei, then likapigwa chini.
2) Kuna vitu watu wengi wanachanganya, tune ya nkosi sekelel origin yake ni mwanamziki Joseph parry wa wales ikaja ikawa adopted na sontonga wa SA Enzi za 1897, baadae Tanzania wakaandaa wimbo kwa maneno yetu ya Kiswahili lakini kwa kutumia ile tune, hadi mwaka 1961 siku ya uhuru tukatumia wimbo wa mungu ibariki tukaondoa wimbo wa wakoloni, hivyo ukazidi kuchochea kasi ya mapambano ya kuondoa ukoloni Africa, hivyo mungu ibariki tune ikawa imeingia hadi nchi za Zambia/Zimbabwe wakitumia same tune but different words kulingana na makabila /lugha zao, so baada ya mwaka 1994 SA kapata uhuru nao pia wakapiga chini wimbo wao wa kikoloni na ndo wakaja na nkosi ambao haukuwa wimbo officially wa taifa, so walichofanya ni kutumia same nkosi tune na ku add maneno.
3) Kila nchi Kabla ya ukoloni kulikuwa na jeshi /police kila kitu, swali hapa je jeshi au police lilikuwa lina serve under for which interest? jeshi lilikuwa na lina serve black or white interests? kama lilikuwa lina serve under black interest je kulikuwa na sababu ya nchi za kusini kuomba hifadhi TZ? wanajeshi wengi ( weusi) wa SA walio fanikisha shughuli nyingi za uhuru SA walipata mafunzo Tz, Libya ,Nigeria na Zambia, ndo hao wakaja kuunda jeshi jipya baada ya mandela kuingia madarakani.
 
historia ya huo wimbo unayo au unatokwa na mate bila sababu ya msingi?
Wewe mjadala wa waliovimbewa, wakakosa la kufanya na kuamua kuimbishana nyimbo za taifa, kisha kuanza bishania juu ya tanzania, ndo ukupe imani kuwa hatuna wimbo wetu wa taifa? Bila kujali asili ya wimbo, wabishanaji unaowapampekia walieleweshana juu ya nini kilichokubaliwa juu ya melody ya nkosi sikeleli miongoni mwa mataifa ya afrika kipindi cha miaka ya kupigania uhuru? Wanajua nafasi na msimamo wa tanzania ktk afrika?...
 
Ahsante sana kamarade, kamanda, mzalendo...! Fb inazidi kuwa(chambilecho mwl Nyerere), kokoro...! Ubaya kunaanza kujazwa na "wenye kujua kupita, wasichokijua"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom