Tukubaliane, hatuna wimbo wa Taifa

Tukubaliane, hatuna wimbo wa Taifa

Watanzania inabidi tujitahidi kuwa tunafikiria mambo ya maana kuliko kutumia muda kwenye keyboard kuandika mambo ambayo hayana maana yoyote. Wimbo wa Taifa lolote ni wimbo unaobeba mashairi yanazungumzia imani au pride ya nchi husika. Kwa vile wimbo wowote uni sifa kadhaa zikiwemo mdundo, mwafaka, mkong'osio na mashairi, cha muhimu katika wimbo wa Taifa ni yale mashari yake. Mdundo, mwafaka na mkong'osio na hata mashairi yenyewe vinaweza kuwa utunzi wa mtu yeyote hata ambaye siyo raia wa Taifa husika lakini mashairi yakawa yanalenga taifa husika.

Mtemi Milambo wa Tabora naye alikuwa na wimbo wake ukiitwa "oohh" chuma chabela mitwe", baadaye wimbo huu ulichukuliwa kuwa wimbo wa TANU "Oooh TANU yajenga nchi" na pia ukawa adopted kuwa wimbo wa KANU ya Kenya kuwa "Oooh KANU yajenga nchi" It is just a song, what matters are the lyrics.
 
KUMEKUWAPO na mjadala kwamba Watanzania hatuna wimbo wa taifa. Mjadala huu upo ndani na nje ya nchi yetu. Unashirikisha Watanzania na wasio Watanzania, anaandika Ansbert Ngurumo.

Kuhusu suala hili, nakumbuka niliwahi kubanwa na baadhi ya raia waSwaziland na Lesotho, mwaka 2001 nikiwa jijini Mbabane kwa mafunzo mafupi ya uchambuzi wa kisiasa.

Tulikuwa kundi la waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika Kusini mwa Sahara. Watanzania tulikuwa wawili – mimi, na Mayage S. Mayage, wakati huo nikiwa naandikia magazeti ya The African na Rai.

Katika shamrashamra za hapa na pale, siku moja wakati wa mapumziko, mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, raia wa Lesotho, akapendekeza kila watu waimbe wimbo wao wa taifa. Likaonekana ni jambo jema, kila mtu ajivunie utaifa wake na nchi yake mbele ya wenzake.

Kila wimbo ulipoimbwa, ulihitimishwa kwa makofi ya shangwe na (wakati mwingine) vigelegele kutoka kwa akina dada waliokuwapo. Tulikuwa tunaimba kwa mzunguko. Ilipofika zamu ya Tanzania, tukaanza kuimba kwa mbwembwe.

Hatukumaliza hata ubeti wa kwanza. Mara tukakatizwa na mmoja wa wasikilizaji wetu, akisema, “samahani, tumesema Tanzania. Sasa mbona mnaimba wimbo wa Afrika Kusini? Hamjui utaifa wenu nini?” Kabla hatujajibu, mwingine akadakia: “Hapana, huu wimbo ni wa Zambia. Hebu tuimbieni wimbo wenu.” Wengine wakacheka kama vile wanataka kutuzomea.

Nikakaribia kuwakasirikia, lakini nikawaeleza kwa upole kuwa hoja zao zinaonesha walivyo “washamba” kwa kushindwa kujua kuwa tunachoimba si wimbo wa Afrika Kusini wala wa Zambia, bali wa Tanzania. Nikawaeleza kwamba wangetuacha kwanza tukaumaliza ndipo waufananishe na hizo wanazozungumzia.

Nikawataka waelewe kwamba nyimbo kufanana tuni si kosa, bali ni sehemu ya, na zao la, umoja wa dhamira ya mapambano na ukombozi wa bara letu.

Nikasema kuwa na wimbo unaofanana ni sifa si kejeli; ni kama kuwa na lugha moja inayowafananisha Waafrika na kuonesha udugu na mshikamamo ambao Waafrika wanahitaji sasa, labda kuliko wakati wowote wa historia yao.

“Sawa. Lakini haiondoi kwamba wimbo huo unajulikana ni wa Afrika Kusini. Nyie mmeunakili. Mna hakimiliki?” Alihoji mmoja wao.

Hata hivyo walio wengi waliona mantiki katika hoja yangu ya “kulazimisha.” Nililazimisha hoja hiyo kutetea wimbo wetu, kwa sababu sikuwa na sababu ya kuonesha unyonge wa Watanzania mbele ya raia wa nchi nyingine.

Nilitimiza azima hiyo, lakini dhamiri yangu ilikuwa inaniambia kwamba, “vijana hawa wana hoja.” Bahati niliyokuwa nayo ni kwamba sikukutana na mmoja wao mwenye hoja kali.

Walikuwa na ubishi tu, na waliridhika haraka haraka na maelezo yangu ya juu juu na ya kulazimisha. Labda mjadala ungekuwa mkali na mrefu kama wangehoji zaidi, maana sikuwa tayari kushindwa kueleza kwa nini Watanzania hatuna wimbo wetu.

Hoja hii imekuwa ikijadiliwa pia na baadhi ya wanasiasa wetu, hasa walio katika vyama visivyo madarakani.

Nakumbuka kipindi fulani, akina Bob Makani (wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo) na Freeman Mbowe (katika awamu ya kwanza ya ubunge wake wa Jimbo la Hai), waliwahi kuvalia njuga suala la wimbo wa taifa.

Wapo baadhi ya wanaharakati, wakiwamo waandishi wa habari, walikubaliana nao. Sababu ni zile zile kwamba hatuna wimbo wetu. Tumeazima.

Walifika mahali pa kusema kwamba, Chadema kikiingia madarakani, watabadili wimbo wa taifa kwa sababu huu uliopo hauna mvuto na hausisitizi utaifa. Wakapendekeza tubadili wimbo, badala ya huu wa sasa, tuimbe “Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo wote…”

Naamini viongozi wetu, kama ilivyo kawaida ya viongozi wa Afrika, waliona suala hilo ni la wapinzani, na ni la kipinzani.

Sijawahi kusikia viongozi wetu wakilijadili. Sijawahi kusikia hata mbunge mmoja wa CCM akinukuliwa kutoa hoja hiyo kwenye vikao vya uamuzi.

Na zikiimbwa nyimbo zote mbili (Mungu Ibariki Afrika; na Tanzania nakupenda kwa moyo wote), ni dhahiri kwamba huu wa pili ndio unasikika na kuhisiwa wa kizalendo kwetu. Ni wimbo wetu.

Zaidi ya hayo, kwa sababu ya ukubwa wa Afrika Kusini na umaarufu wake katika dunia, wimbo wake umefunika wimbo wetu. Siku zikutanapo timu za taifa, au viongozi wetu wanapotembeleana, zikipigwa nyimbo hizo, ndipo ukweli huu unapogundulika. Tumeiga.

Kwa faida tu ya wasomaji, ngoja nieleze historia fupi ya wimbo huu. Katika dunia nzima, hasa Afrika Kusini kwenyewe ulikoanzia, unajulikana kama “Nkosi Sikelel’ iAfrika” – maneno ya lugha ya ki-Xhosa, yenye maana ya “Mungu Ibariki Afrika.”

Mtunzi wake anaitwa Enoch Sontonga, aliyekuwa mwalimu katika shule moja ya misheni ya Kimethodisti, Johannesburg, Afrika Kusini.

Aliutunga ukiwa kama utenzi mwaka 1897. Uliimbwa kwa mara ya kwanza hadharani mwaka 1899 katika ibada ya kuwekwa wakfu mchungaji Boweni, wa Kanisa la Methodist.

Kwaya ya Sontonga na kwaya nyinginezo zikawa zinauimba mara kwa mara katika matukio jijini Johannesburg na Natal. Watu wakaupenda.

Mnamo Januari 8, mwaka 1912, katika mkutano wa kwanza wa Chama cha Wazawa wa Afrika Kusini (SANNC), mtangulizi wa ANC, wimbo huo uliimbwa mara baada ya sala ya kufunga mkutano.

Mwaka 1925, ANC ikauchukua kama wimbo wake rasmi ulioimbwa mwishoni mwa mikutano yake. Tangu hapo, wimbo huo umejulikana nje ya Bara la Afrika kama wimbo wa ANC, kwani ulikuwa ukiimbwa katika mikutano ya ANC katika harakati za ukombozi.

Harakati hizo ndizo zilifikisha wimbo huo hadi kwetu. Nasi tulipopata uhuru, tukauchukua kama wimbo wa taifa, tukautafsiri kwa Kiswahili, tukapunguza baadhi ya aya na kuubakiza kama ulivyo leo.

Zambia nao walifanya hivyo. Namibia pia waliutumia. Zimbabwe nao waliuiga, lakini baadaye “walipopata akili” wakautema, wakatunga wimbo wao.

Kwa kipindi kirefu, Afrika Kusini ilikuwa na “nyimbo mbili za taifa.” Mmoja ulijulikana kama wimbo rasmi na mwingine, usio rasmi.

Wimbo rasmi (uliotumiwa na serikali ya makaburu) uliitwa kwa jina la Die Stem (ki-Afrikaans), yaani Wito wa Afrika Kusini; na usio rasmi (uliotumiwa za wanaharakati wa ANC), ndio huo Mungu Ibariki Afrika.

Siku ANC iliposhinda uchaguzi wa kwanza kidemokrasia mwaka 1994, nyimbo hizo mbili zikatangazwa kuwa nyimbo rasmi za taifa, lakini mwaka 1996 ziliunganishwa; yakachukuliwa maneno huku na huku, ghani ikabaki ile ile ya wimbo wa ANC, ukakarabatiwa na kuwa kama ulivyo leo.

Kwa Afrika Kusini, Nkosi Sikelel’ iAfrika, kabla na baada ya uhuru, ni ishara ya uhuru na mapambano ya ukombozi wao. Unaimbwa katika lugha mbalimbali Kixhosa, Kiingereza, Kisesotho na Kiafrikaans.

Maneno yaliyo katika aya ya kwanza yaliandikwa na mtunzi mwenyewe (Enoch) katika lugha yake ya Xhosa. Mwaka 1927, aliyekuwa mmoja wa washairi maarufu wa nchi hiyo, Samuel Mqhayi, aliongeza aya nyingine saba katika lugha hiyo hiyo.

Kabla ya hapo, mwaka 1923, Solomon Plaatje, mmoja wa waandishi mahiri nchini humo, ambaye pia alikuwa miongoni mwa waasisi wa ANC, ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuurekodi wimbo huo katika studio jijini London, akisindikizwa na muziki wa piano uliopigwa na Sylvia Colenso.

Mwaka huo huo, kiwanda cha uchapaji cha Lovedale Press, katika Jimbo la Eastern Cape, kilichapisha nakala yenye aya zote katika kijitabu. Juni 11, 1927, wimbo huo ulichapishwa katika gazeti la Umtetela Wa Bantu, ukaingizwa pia katika kitabu cha ushairi cha Kixhosa kwa ajili ya kuwafundishia watoto shuleni.

Wimbo huo pia uliingizwa rasmi katika kitabu cha nyimbo za Kixhosa kwenye Kanisa la Wapresbyteri kilichojulikana kama Ingwade Yama-culo Ase-rabe, mwaka 1929. Mwaka 1942, Moses Mphahlele, alichapisha nakala nyingine za wimbo huo katika lugha hiyo na kuzisambaza ili umma ukariri vema maneno yake.

Kwaya ya Ohlange Zulu, ya Mchungaji John L. Dube, ndiyo iliyokuza wimbo huo, kwa kuuimba mara kwa mara katika matamasha mbalimbali jijini Johannesburg.

Taratibu ukawa wimbo maarufu katika mikusanyiko ya kidini, kijamii na kisiasa; badaye ukarekodiwa pia na wasanii kina Ladysmith, Black Mambazo, Boom Shaka na Mahotella Queens.

Historia hiyo pekee inaonesha kwamba sisi bado hatuna wimbo. Kama tunavyoimbiwa na wasanii wa CCM kwamba “CCM ina wenyewe,” basi tuna sababu ya kuamini pia kwamba hata wimbo huu tunaouita wa taifa, una wenyewe – na wenyewe ni Afrika Kusini. Nadhani Wazimbabwe waliligundua hilo mapema. Wakaachana nao. Sisi tunangoja nini?

Ni bahati mbaya kwamba vijana wale waliobishana nami hawakuwa wanajua historia ya wimbo huo kama nilivyoieleza hapa. Vinginevyo, walikuwa na hoja; na wangetuaibisha. Tuna wasanii wa kutosha kutunga nyimbo zetu.

Watunge. Kama hatutaki mpya, basi tuchukue zilizopo, zinazoeleza kwa kina historia na utaifa wetu, tuzifanye rasmi nyimbo zetu za taifa, kwani huu tunaoimba sasa si wimbo wetu.
Hivi umejiuliza south Africa na Tanzania nani ameanza kuwa huru na kuimba wimbo Wa Taifa !? Kwa wimbo Wa Zambia ni sawa na wetu tena ni kwania makusudi kuonesha dunia mfungamano Wa nchi za Africa .Tafuta hotuba ya Nyerere kuhusu hili
 
SA Africa baada ya kupata uhuru chini ya mandela alikuwa hana uzoefu, kuna maafisa wa Tz waliopelekwa na serikali ya Tz kwa ajili ya maandalizi ya mandela kuchukua nchi, hata kutoa muongozo kwa mandela hata baada ya kuwa raisi. Baadhi ya vitu ambavyo walivifanya ni pamoja na kutoa mafunzo ya maandalizi ya siku ya kuapishwa kwa raisi mandela, kujifunza nyimbo zao za Taifa, bendera, bendi ,kutoa mafunzo ya awali kwa police/jeshi, gwaride na nk, mfano wimbo wa Taifa la Tanzania ulitolewa kwao ili waweze ku update , ili wapate wimbo wao wa SA, kilichofanyika wao SA badala ya ku update wakachukua kama ulivyo wakauweka katika lugha yao na kuimba kama ulivyo. Kwa nini huu wimbo wa Tz kwa sasa chimbuko lake linaonekana limetoka SA? kwanza SA imeendelea, watu wengi wako more aware kuhusu SA kuliko Tz, pili watu wengi wako aware na zaidi kuhusu story za SA na wanafuatilia mambo mengi ya SA kuliko Tanzania. Pili SA ina uwakilishi mkubwa kimichezo zaidi ya Tanzania ( rugby, Olympic, soccer, ) na kila wanapofanya hizo activities wimbo huimbwa na kujulikana. Tanzania haikucopy wimbo huu kutoka SA maana sisi tulipata uhuru mapema na tukaandika wimbo wetu kabla yao.
Safi sana kumfahamisha huyu RAIA.maana ameandika bila tafiti.
 
Awali nilikua mwepesi sana kuamini kila anachokiandika Malisa G. J
Nilikuamini kuliko ninavyoiamini Google..
Unfortunately nimekugundua wewe ni mtu wa kupika sana taarifa.. in short huna usichokijua.. Mchumi wewee!! Historian wewe!! Muhisabati wewe!! Geologist wewe!! Politician wewe!! Journalist wewe!! Mwanaharakati wewe!! Linguist wewe!! Plus many other self imposed titles... U must be a genius of some sort i guess!! Otherwise you are just another Con artist...
Maajaaliwa yako ya kuandika andika huoni haya wala kusita kuyatumia kuandika kile unachofikiri hata kama ni cha upotoshaji..
Maarufu kweli kweli kwenye kutaja taja majina tu kwenye mabandiko yako hata kama hayana uhusiano wowote ule na mada unayojaribu kuipigia debe... taking advantage ya wabongo majority wanaoshindia vichwa vya habari bila undani wa habari yenyewe plus wabongo wasivyowepesi kufuatilia nyaraka kubaini ukweli na uongo wa taarifa unayojivunia kuwadadavulia... unatumia hizi platforms za social media kuwajaza watu your cooked information ambazo hata huwa sijui unazitoaga wapi na kwa manufaa ya yepi...
Slow down buddy tumekubaini...
Nakushauri ungehamia kwenye uandishi wa riwaya na hekaya.. ingekufaa zaidi..

U r free kunidhihaki na kunitukana.. but it wont change the fact of u true colours...
 
TZ na SA ninani wakwanza kupata uhuru??au unachanganya kati ya uhuru na ubaguzi wa rangi??
 
Huyu ana agenda yake. Nitarudi tena atakapojibainisha kile anataka. Maana nakifahamu. Nitarudi akijiweka bayana. Upumbavu huu utaisha lini?
Huyu jamaa kila kukicha analeta mada za ajabu ajabu. Juzi kasema manager ww hotel kateuliwa kua DED sasa sijui na hii habari ya kubanwa tumwamini ama la
 
Wafuasi wa CDM kwa ubaguzi hatari wanabagua mpk wimbo wa Taifa. Wanaharakati nasikia mmeanza kumbagua ht Mbowe sasa
 
Awali nilikua mwepesi sana kuamini kila anachokiandika Malisa G. J
Nilikuamini kuliko ninavyoiamini Google..
Unfortunately nimekugundua wewe ni mtu wa kupika sana taarifa.. in short huna usichokijua.. Mchumi wewee!! Historian wewe!! Muhisabati wewe!! Geologist wewe!! Politician wewe!! Journalist wewe!! Mwanaharakati wewe!! Linguist wewe!! Plus many other self imposed titles... U must be a genius of some sort i guess!! Otherwise you are just another Con artist...
Maajaaliwa yako ya kuandika andika huoni haya wala kusita kuyatumia kuandika kile unachofikiri hata kama ni cha upotoshaji..
Maarufu kweli kweli kwenye kutaja taja majina tu kwenye mabandiko yako hata kama hayana uhusiano wowote ule na mada unayojaribu kuipigia debe... taking advantage ya wabongo majority wanaoshindia vichwa vya habari bila undani wa habari yenyewe plus wabongo wasivyowepesi kufuatilia nyaraka kubaini ukweli na uongo wa taarifa unayojivunia kuwadadavulia... unatumia hizi platforms za social media kuwajaza watu your cooked information ambazo hata huwa sijui unazitoaga wapi na kwa manufaa ya yepi...
Slow down buddy tumekubaini...
Nakushauri ungehamia kwenye uandishi wa riwaya na hekaya.. ingekufaa zaidi..

U r free kunidhihaki na kunitukana.. but it wont change the fact of u true colours...

Bado na wewe hujatupa sababu au mifano ya upotoshaji wa Malisa it is not mere allegations kama ulivyoandika
 
SA Africa baada ya kupata uhuru chini ya mandela alikuwa hana uzoefu, kuna maafisa wa Tz waliopelekwa na serikali ya Tz kwa ajili ya maandalizi ya mandela kuchukua nchi, hata kutoa muongozo kwa mandela hata baada ya kuwa raisi. Baadhi ya vitu ambavyo walivifanya ni pamoja na kutoa mafunzo ya maandalizi ya siku ya kuapishwa kwa raisi mandela, kujifunza nyimbo zao za Taifa, bendera, bendi ,kutoa mafunzo ya awali kwa police/jeshi, gwaride na nk, mfano wimbo wa Taifa la Tanzania ulitolewa kwao ili waweze ku update , ili wapate wimbo wao wa SA, kilichofanyika wao SA badala ya ku update wakachukua kama ulivyo wakauweka katika lugha yao na kuimba kama ulivyo. Kwa nini huu wimbo wa Tz kwa sasa chimbuko lake linaonekana limetoka SA? kwanza SA imeendelea, watu wengi wako more aware kuhusu SA kuliko Tz, pili watu wengi wako aware na zaidi kuhusu story za SA na wanafuatilia mambo mengi ya SA kuliko Tanzania. Pili SA ina uwakilishi mkubwa kimichezo zaidi ya Tanzania ( rugby, Olympic, soccer, ) na kila wanapofanya hizo activities wimbo huimbwa na kujulikana. Tanzania haikucopy wimbo huu kutoka SA maana sisi tulipata uhuru mapema na tukaandika wimbo wetu kabla yao.
Wimbo wetu watanzania ulikuwa huu, Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote.
 
Inabidi tuanze na mfumo wa nchi. Bila hivyo itabakia historia.
Kwa kuwa TZ ni muungano (TGK+ZNZ) tutashirikisha lafudhi za Qaswida na mashairi pia....!!
manyimbo ya kwaya kwaya tutasimamisha sasa !!

ombi bora tuanze propaganda za nyimbo za alwatan....
 
Mleta mada ameweka historia ya wimbo. Mnaopinga ukweli wake weken historia ya wimbo wetu na mtunz nani!!
Haiwezekan kitu cha kitaifa kisiwe na kumbukumbu!! Vinginevyo mleta mada yuko sahihi na tutafute wimbo wetu
Binafsi sina tatizo na mleta mada pamoja na historia aliyotoa lakini kwa sababu alikuwa na lengo la kutoa darasa juu ya wimbo wa taifa, alichopaswa pia ni kueleza hata kidogo namna tulivyocopy wimbo huo na ni nani alihusika kufanya hivyo lakini pia ni kwanini tuliamua kutumia wimbo huo. Na ni vipi nchi karibu tano zote zikopy wimbo huu? Habari za hati miliki zimekaa vipi katika hili?
 
Back
Top Bottom