Tukubali deni la dowans lilipwe kuepuka kutengwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukubali deni la dowans lilipwe kuepuka kutengwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanajamii, Oct 27, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wanaharakati wa haki za kibinadamu wa Dar es Salaam pengine kwa kusukumwa na uzalendo , ushabiki wa kisiasa au vyote wanaandaa maandamano ya kupinga kulipwa kwa tozo ya zaidi ya Ths. Bilioni 110 kwa Kampuni ya Dowans. Wapo wanasiasa wa chama tawala na wa vyama vya upinzani ambao wanaunga mkono harakati za taasisi hiyo kupinga malipo ya tozo hiyo.

  Wakati tunaangalia hayo tukubali kwamba nchi hii inaongozwa na utawala wa sheria na bila kuangalia kama DOWANS ni ya nani tukubali kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Biashara ICC ndiyo iliyotoza tozo hiyo kwa Kampuni hiyo.
  Watanzania wengi ambao wanataka tozo hiyo isilipwe hawazingatii kwamba kama ICC ikiombwa na DOWANS inaweza kukaza hukumu na kuitangaza Tanzania kwenye vyombo vingine vya Kimataifa, hatua ambayo inaweza kusababisha mali za Tanzania zikakamatwa mpaka pale tozo hiyo itakapolipwa.

  Suala lingine la msingi la kuzingatia ni kwamba kadri tunavyoendelea kubishana na kuendelea kukataa kulipa deni ndivyo riba itakavyozidi kukua na deni kuongezeka. Deni halisi lilikuwa bilioni 94 na sasa ni zaidi ya bilioni 110.

  Tunachotakiwa kufanya ni kile ambacho serikali inafanya sasa cha kutafuta njia rahisi ya kukaa na Dowans na kupata ufumbuzi unaoweza kuipa nchi ahueni. Maandamano na kelele za majukwaani au kwenye vyombo vya habari hazina tija kwa sasa.

  Naomba kutoa hoja.
   
 2. l

  luhwege Member

  #2
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Wew ni mgonjwa kabisa tuko tayari kula nyasi wakati wowote kuliko kuilipa hiyo kampuni ya mafisadi na wewe mwenyewe nahisi unachochote hapo unataka kutuaminisha upuuzi wako hapa nenda zako na andaa jeshi lako la kifisadi kutupiga mabomu jmosi hatutakiiiiiiiiiii ilipwe na pole sana na njaa zako.
   
 3. c

  chachu Senior Member

  #3
  Oct 27, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  tunataka kuona waliotuingiza kwenye mkataba huo mpovu wakiwajibishwa kwanza, Ni lazima uwe na mauchungu kama mlipa kodi. Au swaiba wewe hulipi kodi inauma......!? bila hayo mafisadi kuwajibishwa hatutakubaliana na uchakachuaji huo wakati mlipa kodi hata zile huduma za kijamii hazipati then what...! tukishalipa wajue tz shamba la bibi ha!!!!!!!!!!
   
 4. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 513
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Hoja yako haina mashiko. Inaonyesha ulivyo mvivu wa kufikiri au una maslahi na tuzo hiyo.
  Labda kwa kusaidia serikali ungetueleza pesa hiyo ilipwe toka kwenye fungu gani?
   
 5. F

  FredKavishe Verified User

  #5
  Oct 27, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kama unataka kulipa tufanya hawa wajinga wote walituingiza humo kuanzia baraza la mawazr lililopita mishahara yao ikatwe kwa 80% walipe'
  halafu huyu jk waukate mshahara Wake kwa 90% kila mwez ndo tulipe'kwa rostam na lowasa mali zao zitaifishwe ndo ela za kulipa zipatikane'yale mav8 ya mawazir wapgwe mnada sione sababu ya wao kutanua wakati wametungiza humo'mwanasheria mkuu wa wakati huo anyongwe
   
 6. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,167
  Likes Received: 1,173
  Trophy Points: 280
  Mtoa mada anatoka ukoo wa aziz!
   
 7. V

  Vitalino mlelwa Member

  #7
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unaakili lakini matumizi ya akili ndiyo na ugomvi nayo tulipe hela kwa nani? Kama umetumwa hv mi ningekuona wamaana kama ungetoa wazo la kuwafilisi wahusika kwanza na kuwafunga ndani halafu tuone nani ataendelea kudai halafu afadhali tungekuwa na shelia kama china hawa wote tungekuwa tumeshawanyonga na usumbufu ungekuwa umekwisha.

  Ni lazima shelia hii tuiingize kwenye katiba mpya najisikia uchungu hasa kodi yangu nayokatwa kila mwezi napoona inatumika vibaya wakati mi mwenyewe naishi kwenye hali ngumu.
   
 8. a

  actus Senior Member

  #8
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 7, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi nyie mnaosema DOWANS wasilipwe kwa sababu hizo mnazotoa eti isitoke kwenye fedha za walipa kodi,ooh wale waliopelekea mkatabata ukafanyika ndo walipe,mnaropoka kwa hoja au kwa masaburi? Walau huyo anayesema wawajibishwe ndo ana hoja.ww mtanzania ndo ulitumia umeme huo wa dowans tena kwa kujiachia sasa unasema kodi yako isituimike kulipa?

  Jinsi gani mkatabata ulipatikana it is immaterial.hata kama mkataba ulikua feki a.k.a nully and void(void abnitio)rules of ICC zinasema zinautambua mkataba husika.

  Tatizo hata hizo rules hamjui na wala judgment hamjasoma mnakurupuka kutukana bila hoja.kwa akili zenu hao majaji waliosema ngoma ilipwe hawakusoma hali za nyakati na kuona ngoma imekaa vibaya?jamani alipwe as much ametoa service mkipata muda wa kutokurupuka na kutoa upuuzi kasomen between the lines ARTICLE 6(4) of the ICC Rules.
   
 9. BABA JUNJO

  BABA JUNJO JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  teh tehe tehe tuhu tuh tu mbwiii!! tuh tuh Nenda kajisadie haja ndogo ukalale maana usipfana hivyo uta achia kitandani.
   
 10. h

  herimimi Member

  #10
  Oct 27, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ICC wanataka downs walipwe, ni haki yao. watanzania wanataka kodi yao isitumike kuwalipa hadi waliosababisha tafrani hiyo wamewajibika kwa kuilipa serikali kiasi hicho cha hasara,mwisho serikali itachukua hizo fedha ilizolipwa na hao mafisadi na kuwalipa downs.

  Mchezo utakuwa umekwisha. tusiruhusu serikalli yetu kulipa deni kabla ya yenyewe kulipwa na hao wajanja waliosababisha hiyo hasara.tutoa funzo kwa viongozi wetu kutuheshima na kuwakumbusha kuwa cheo ni dhamana. walipa kodi tusikubali kuibiwa mchana kweupa.

  Nguvu ya umma inatisha.
   
 11. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,131
  Likes Received: 3,320
  Trophy Points: 280
  Bilioni 150 lazima ilipwe.
   
 12. c

  chachu Senior Member

  #12
  Oct 27, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  SHAMBA LA bibi
   
 13. kukomya

  kukomya JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 344
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Hakika wewe ni mmojawapo wa watakaonufaika na malipo hayo. Sina shaka kwamba wewe ni wa magamba na unafahamu fedha hizo zinakokwenda.

  Haiingii kabisa akilini kuona kundi la vibaka wa kimataifa wakishirikiana na serikali iliyosheheni vibaka kuitapeli nchi na baada ya kubainika kudai fidia! Rais mwenyewe alisema waziwazi kwamba hamjui huyo Dowans ni nani, sasa tuambie ni nani tumlipe?
   
 14. mbongowakweli

  mbongowakweli Member

  #14
  Oct 27, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Halipwi mtu, tuanze kuwalipa wazee na wajane wa EAC, tuboreshe umeme, maji, miundo mbinu, afya na elimu, halafu ndio tutafirikiria kesi ya DOWANS, kama umekuja kuwapigia debe humu ndani basi unapoteza muda.

  Tuna mlolongo mkubwa wa kutumia hela za serikali, na sio kuwaongezea utajiri mapapa na mafisadi wanaotafuna hela za mlalahoi!
   
 15. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Bila shaka wewe ni NGELEJA au ndugu yk
   
 16. a

  actus Senior Member

  #16
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 7, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  DOWANS is a Company as a legal entity.kwa hiyo mnailipa DOWANS.Yani hapo kama huna elimu ya what is a company take trouble ukasome uache kuropoka na kuuliza upupu!!!labda ungeuliza mashare holdars na madirectors wa Dowans kidogo ungejibiwa.usiulize DOWANS.KOMA
   
 17. Nkoboiboi

  Nkoboiboi JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ushindwe na ulaanike kama una mgao zitawatokea puani....!!1
   
 18. a

  actus Senior Member

  #18
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 7, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  issue sio kwamba muanze kuwalipa akina nani,au muimarishe nini?mwisho wa siku italipwa na kwa upeo wako nadhani hata kama imeisha lipwa au haijalipwa hutajua.mie siwapigii debe naeleza kile ICC inachokitambua ktk mikataba.take my words jamaa watalipwa na hutafanya lolote zaidi ya kutuma thread!!!!
   
 19. Nkoboiboi

  Nkoboiboi JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ICC iwalipe..... huo mkataba uliosainiwa hotelini Dar.....!!!! Nawe unaganganyika ki u rahisi hivyo..... wawalipe waishe.... Mungu ataingilia kati ikibidi..
   
 20. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ni vizuri sn wakitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa tumegoma kulipa dowans ili dunia ijue k tumeamka hatutaki upumbavu tena.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...