winnerian
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 335
- 530
Kuukarabati mfumo wa "Utawala bora" pamoja na sheria zetu ili kuziba na kurekebisha mianya, nyufa, matobo, maadili mabovu, uzembe ofisi za umma, pamoja na mambo yote yanayoifanya nchi yetu iende kinyumenyume ikiwa jitahada za dhati zinafanyika na viongozi wakubwa lakini bado matokeo hayaridhishi.
Amini amini nawaambieni hivi leo Rais anatamani sana kuona amefanya kwa ufanisi kwenye awamu yake lakini mfumo wetu hauwezi kumruhusu akatimiza ndoto zake, kwani chini yake ni msururu wa tamaduni zilizojishikiza kwenye mfumo usiotaka maendeleo ya wazi.
Katiba, sheria, na sekta nyingi zinazoelekeza njia ya maendeleo ni kama zimefifia mno kuweza kusomeka barabara.
Tukope hako katrilioni tukatumie kuisuka upya Tanzania na baada ya hapo hata kabilioni kamoja tu kataweza kutuvukisha mbali sana.