'Tuko njiani kupata ushindi' - Netanyahu

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
836
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema "tuko njiani kupata ushindi".

Akitembelea kambi ya anga ya Israel, alirejelea madai ambayo tumesikia kutoka Israel leo - kwamba "inadhibiti anga ya Tehran".

"Tuko njiani kufikia malengo yetu mawili: kuondoa tishio la nyuklia na kukomesha tishio la makombora," alisema.

Netanyahu pia alisema anataka kuleta tofauti kati ya mashambulizi ya Israel na yale ya Iran, akiongeza kuwa haya ndiyo malengo ya Israel na kudai Iran inalenga raia.

"Tunawaambia raia wa Tehran: 'Ondokeni' - na tutachukua hatua," alisema.

Aliwaambia wale wanaofanya kazi kwenye kituo cha kambi za jeshi: "Asanteni, na kwa uwezo wa Mungu – tutachukua hatua na kufanikiwa, na kuendelea hadi tupate ushindi."

Wizara ya afya ya Iran imeripoti kuwa takriban watu 224 wameuawa katika mashambulizi ya Israel tangu Ijumaa.

Hata hivyo, waandishi wa habari wa BBC hawawezi kuripoti kutoka ndani ya Iran kutokana na vikwazo vya serikali ya nchi hiyo.
 
IMG_20250616_221429.jpg
 
Hata hivyo, waandishi wa habari wa BBC hawawezi kuripoti kutoka ndani ya Iran kutokana na vikwazo vya serikali ya nchi hiyo
Propaganda hii, Israel mbona ndio inazuia taarifa za vifo na majeruhi!! Mfano lile ghorofa lililolipuliwa Haifa, kuna watu 57 hawaonekani, 100 wamejeruhiwa ila wamekufa watatu pekee!!!

Propaganda huwa zipo pande zote, in fact Iran inafurahia zaidi kuonyesha watu wengi wamekufa kuliko uhalisia ili kuonyesha uovu wa Israel kwa dunia, otherwise inafaidika nini ikishusha idadi za vifo?

Anyway vita ni mbaya tuache ushabiki wanaoteseka ni watoto na wamama sio wanajeshi
 
Kwani wasiporipoti bbc ndio haiwezi kuwa habari? Hujui kuwa vyombo vya habari vya kimagharibi huwa ginatia chumvi uzisipendeza?

Back
Top Bottom