Tukiwa wadogo tulitamani kufanya mambo mengi ila tulibanwa na wazazi, leo tumekuwa watu wazima tunatamani kufanya mambo mengi ila tunabanwa na Uchumi

Habari wakuu,

Ni ukweli usiopingika kipindi ukiwa mtoto, kuna mambo mengi ya utotoni ulitamani kuyafanya lakini wazazi/walezi walikukataza, kutokana na saababu mbalimbali kitu kilichopeleka kuhisi kukosa uhuru

Maisha yanabadilika unakuja kuwa mtu mzima ukiwa na uhuru wa kufanya kila kitu lakini Uchumi nao unakubana ,hii hali inafanya tutafakari mengi kuhusu maisha

Itafikia kipindi utakua na uhuru wa kiuchumi lakini kuna mambo mengine utatamani kufanya lakini mazingira hayatakuruhusu

Tujifunze kuwa na kiasi katika matamanio yetu

Tafakari!
Mambo mengine Umri nao (uzee)unatubana.
 
Back
Top Bottom