Tukio lililonijenga kiimani na kuamini Mungu yupo

Tukio lililonijenga kiimani na kuamini Mungu yupo

Wang Shu

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
2,573
Reaction score
3,757
Habarini,

Story, Nikiwa ninamiaka 15_20 nilikuwa ni mtu mbishi sana nisiekubali kitu kiurahisi ila udhaifu wangu ulikuwa uoga wazazi walinijua zaidi na izo.

Kuna wakati nilikuwa tunabishana na marafiki zangu kuhusu uwepo wa mungu mimi ndio nilikuwa mbishi namba 1 kuwaaminisha mungu hayupo mabishano yalidumu kama wiki,ikafikia wakati wakaanza kunichukia na kunitenga maana ubishi nimezidisha.

Siku moja usiku majira ya saa mbili usiku wa giza nilitumwa dukani na wazazi nilikataa kwenda kwasababu ya giza wakanipatia kurunzi(torch) ile ya bati tupu betry mbili kubwa national.

Nikiwa njiani natembea kuelekea dukani nikajikuta najiropokea "ngoja nimmulike mungu juu nimuangalie kama nitamuona kweli" nikaelekeza kurunzi(torch) juu nikanyoosha na mkono mpaka mwisho nikatazama kwakuwa betri zilikuwa mpya niliona miale kwambali kuashilia inamulika anga nikakodoa macho.

Ghafla kurunzi(torch) ilizima nikashusha chini nikaanza kuogopa giza alafu sijafika,nikasimama kama dk 3 nikijalibu kuipiga piga labda itawaka zilikuwa zina tabia iyo ukizipiga zinawakaga,toa betri weka tena wapi haiwaki nikaamua kuachana nayo uku uoga unizidi "nikijisemea au mungu ameamua kuizima ili nisimuone" nikaanza kumuogopa mungu nakuanza kuamini nilijikuta nakimbia mpaka dukani nikanunua nilichotumwa mbio tena mpaka nyumbani.

Kufika nyumbani nahema baba aliniuliza, pesa iliyorudi dukani ipo wapi? Uku nahema kwa uoga nikamjibu "nimesahau pale dukani sijachukua" akanifokea akaniambia naomba iyo kuruzni(torch) akaijalibisha haiwaki akafanya anavyojua lakini haikuwaka akazidi kuchukia alinichapa vizuri sana uku akiniambia nikitumwa nisikimbie mpaka nadondosha vitu na kualibika nikalia nikaenda kulala nilisusa kula.

Tangia usiku ule adi asubuhi yake mpaka leo ninahofu na mungu kila nikiwaza kumletea utani naogopa na nina imani yupo na invisible.

Poleni maana ni ndefu kiasi.

I'm done.
 
Kapige nyungu mkuu kisa chako kidogo sana mpaka kukuaminisha hivyo pole sana maana huenda hizo gropu za tochi ziliungua au hitilafu ilitokea.. pole mkuu
 
Is a theoretical issues . Hakuna kitu kama hicho ni torch tu imeharibika fullstop
 
Kapige nyungu mkuu kisa chako kidogo sana mpaka kukuaminisha hivyo pole sana maana huenda hizo gropu za tochi ziliungua au hitilafu ilitokea.. pole mkuu
asante, mkuu.
 
Kama unamzungumzia Mungu wa mbinguni tunayemuamini, inaandikwa 'Mungu' siyo 'mungu'..!!
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Story ya kutunga. Kwa miaka ile ya kurunzi za bati, mtoto wa umri huo hawezi kuwa jasiri wa kupinga uwepo wa Mungu hadharani
 
Story ya kutunga. Kwa miaka ile ya kurunzi za bati, mtoto wa umri huo hawezi kuwa jasiri wa kupinga uwepo wa Mungu hadharani
Unaeza usiwe jasiri wakupinga lakini inategemea na unaobishana nao watoto wenzako umri sawa mnajuana vizuri unaeza kuna vijitabia vyakiasili unajikuta ww unasimamia jambo lako ata bila uhakika

I'm done.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom