Tukio lililoisisimua Dunia....

wiseboy.

JF-Expert Member
Aug 11, 2014
2,932
4,534
Mwaka 1918 ktk ulimwengu wa kisiasa nchini Marekani kulitokea Tukio la kusisimua ambalo limeacha maswali mengi mno Duniani yasiyojibiwa.
Mtu mmoja mweusi aliamua kugombea Ugavana wa Jimbo la Tennessee, kipindi kile kulikuwa na ubaguzi wa rangi uliotukuka, yaani mtu mweusi alionekana Kama nyani.
Dennis Con alichukua form huku kila mtu akishangaa ujasiri huo aliutoa wapi, aliamua kuchuana na Andrew Miller mzungu mwenye asili ya Ireland.
Kidume alichukua form na kuijaza kibabe, na kisha kuirudisha Kwenye tume ya uchaguzi ya Jimbo la Tennessee.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa Jimbo hilo aligoma kuisaini hiyo form, watu weusi walichukia mno kuona wanabaguliwa waziwazi.
Dennis Con aliitisha maandamano na kuyaongoza kwenda Kwenye tume ya uchaguzi, Police wakapewa amri ya kutawanya waandamanaji wote.
Police walipiga risasi juu ili kuwatawanya waandamanaji, ajabu risasi moja ilienda juu mno kisha ikaanza kukata kona, mara ikaanza kushuka chini, kabla haijafika chini ikapaa tena umbali wa mita 30 kutoka usawa wa Bahari, kisha risasi hiyo ikakimbilia ndani ya basi la wanafunzi wa kizungu na bahati mbaya risasi hiyo ikampata kijana wa kizungu na kusambaratisha kifua chake, papo hapo akafariki.
Risasi hiyo ilikuwa ni ya aina gani? Wanasayansi wa Marekani wameshindwa kubaini baada ya uchunguzi wa miaka mingi, hakika ni Tukio la kusisimua.
 
Tukio hilo unapenda kulihusisha na siasa zetu au??? Au ni coincidence tu kwa tukio la kndoni
 
Dennis Con hakufunguliwa mashtaka ya kubambikiziwa ya kumuua huyo mzungu mwanafunzi?
Vipi, hata mashtaka ya uasi na ulaghai mwingine wowote Dennis Con hayakumhusu?
Basi kama hivyo ndivyo, Tennessee ya mazungu wabaguzi ilikuwa nafuu zaidi kuliko haya yanayomkabili Mbowe na wenzake! Hebu tupe mlejesho zaidi ya yapi yaliyomtokea Dennis Con baada ya zahama hilo, tulinganishe na haya yanayotokea Tanzania ya 2018, inayodai ilipata Uhuru wake zaidi ya miaka 50 iliyopita.
 
Mwaka 1918 ktk ulimwengu wa kisiasa nchini Marekani kulitokea Tukio la kusisimua ambalo limeacha maswali mengi mno Duniani yasiyojibiwa.
Mtu mmoja mweusi aliamua kugombea Ugavana wa Jimbo la Tennessee, kipindi kile kulikuwa na ubaguzi wa rangi uliotukuka, yaani mtu mweusi alionekana Kama nyani.
Dennis Con alichukua form huku kila mtu akishangaa ujasiri huo aliutoa wapi, aliamua kuchuana na Andrew Miller mzungu mwenye asili ya Ireland.
Kidume alichukua form na kuijaza kibabe, na kisha kuirudisha Kwenye tume ya uchaguzi ya Jimbo la Tennessee.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa Jimbo hilo aligoma kuisaini hiyo form, watu weusi walichukia mno kuona wanabaguliwa waziwazi.
Dennis Con aliitisha maandamano na kuyaongoza kwenda Kwenye tume ya uchaguzi, Police wakapewa amri ya kutawanya waandamanaji wote.
Police walipiga risasi juu ili kuwatawanya waandamanaji, ajabu risasi moja ilienda juu mno kisha ikaanza kukata kona, mara ikaanza kushuka chini, kabla haijafika chini ikapaa tena umbali wa mita 30 kutoka usawa wa Bahari, kisha risasi hiyo ikakimbilia ndani ya basi la wanafunzi wa kizungu na bahati mbaya risasi hiyo ikampata kijana wa kizungu na kusambaratisha kifua chake, papo hapo akafariki.
Risasi hiyo ilikuwa ni ya aina gani? Wanasayansi wa Marekani wameshindwa kubaini baada ya uchunguzi wa miaka mingi, hakika ni Tukio la kusisimua.
Ni sawa na tukio la Akwilina aliyepigwa risasi wakati akiteremka kwenye mlango wa daladala lakini upepo ukageuka na kumpiga kichwani kabla basi halijafika kituoni.
 
Back
Top Bottom