Tukio la Mauaji Dar, ni Ujambazi, Kisasi au Ugaidi? Tujifunze kitu

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,273
Ni zaidi ya Msaa 8 hivi kupita baada ya tukio la leo 25/8/2021 kubwa kwa nchi yetu, hatujapata kuwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga kwa risasi nadhani tangu Tanganyika ipate Uhuru wake, Ni tukio kubwa kimedani na linatulazimisha tuweke kando siasa zetu chafu tukae chini na tutafakari na kuruhusu taaluma zifanye kazi. Kwanza natoa pole nyingi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP na kwa ndugu na jamaa wote waliofiwa na makamanda waliokuwa katika oparesheni hii ngumu kabisa.

Tukio hili limenikumbusha mahojiano maalumu niliyoyafanya tarehe 23 June 2021 kupitia Radi Ebony FM, nikachambua ziara ya Rais Samia nchini Msumbiji ambako pamoja na mambo mengine, Tanzania iliteuliwa na SADC kuwa kitovu cha vita dhidi ya Ugaidi. Uchambuzi wangu uko katika Audio/video hii hapo.

Tukio la leo linaweza kushahabiana kinadharia, lakini linaweza kutofautiana kimanti. Kwanza tunakubaliana wote kwamba kumetokea tukio la mauaji. Hili wote tunakubaliana. Pili tukio hili tunaliitaje kwa jina? Hili ni mtihani mgumu kwa jicho la kiraia lakini ni jambo dogo kwa jicho la kiusalama. Ili tupate jina la tukio hili ni lazima tuainishe aina ya matendo katika tukio hili zima ndio yatatupeleka kulipa jina halisi tukio hili na kundi lake halisi.

(1) Ni tukio la Ujambazi?
Hapana linakosa sifa ya ujambazi kwakuwa mhusika kwamjibu wa mashuhududa na video za awali zinaonyesha hakushughulika na uporaji wa mali za watu wala bank ya Stanbick iliyopo jirani na tukio. Kwa nadharia hii tukio hili kwenye ujambazi halipo linakosa sifa kuitwa tukio la ujambazi.

(2) Mhusika huyu wa mauaji ni mtu karukwa na akili/ni kichaa?
Hapa ni vigumu kutoa majibu ya moja kwa moja kwakuwa ni lazima tupate historia ya nyuma ya mtuhumiwa huyu na kwakuwa amefariki basi historia itapatikana kwa ndugu na marafiki zake wa karibu. Bahati nzuri taarifa za awali zinasema ni mkazi wa Dar es Salaam Upanga. Hivyo naamini hatua hii ya awali itakuwa ishafanywa na vyombo vya usalama.

(3) Inaweza kuwa ni kisasi cha mtu huyu dhidi ya polisi (Serikali)? Hili linaweza kuwa kweli kwakuzingatia video za mtu huyu hakushughulika kulenga risasi raia isipokuwa Polisi tu, uwezekano mwingine unakuja pale mtu huyu anapoonekana kama mtu aliyechanganyikiwa kipiga risasi hovyo hewani licha ya kuwaua polisi wa wili na kupora bunduki zaidi ya nusu saa nzima hakuondoka eneo hilo kujaribu kukimbia hadi polisi wakaja na akajibizana nao. Uwezekano mwingine kwamba yaweza kuwa kisasi binafsi ni pale lugha ya mwili ya mtu huyu inapoonekana akitoa lugha ya ghadhabu kwakuonyesha amewakomoa hasa akijipiga kifuani kwa mkono wake. Hili linaweza kutafrika katika uchambuzi wa mwili wa mtu kwa video. Hoja inaweza kuwa ni kisasi cha nini dhidi ya nani.

(3) Ni tukio la Kigaidi? Uwezekano ni mkubwa kuwa la kigaidi, nikiunganisha na mkutano wa wakuu wa SADC uliofanyika Msumbiji na kuiteua Tanzania kuwa kitovu cha vita, kuna uwezekano mkubwa makundi ya Kigaidi yameamua kutuma salamu kwamba yapo kila pembe ya Afrika. Baadhi ya mashuhuda wanasema mtu huyu hakushughulika sana kulenga raia isipokuwa alishughulika na polisi na wakaongeza kuwa alikuwa anatoa sauti yenye maneno ya lugha inayodhaniwa ni ya kiarabu akijipigapiga kifuani kwamkono wake huku akitamba kwa madaha.

Hili linaweza kuwa tukio lenye uhusiano na makundi ya kigaidi (ISI Somali na Alshababi Msumbiji). Kubwa zaidi ni uwezo wa mtu huyu kutumia bunduki tatu za aina tofauti tofauti, Mafunzo ya matumizi ya silaha SMG na bastola na namna anavyoshika na kuzimiliki inatoa tafsiri kuwa mtu huyu ana mafunzo ya silaha hizi. Muhimu hapa tukae kwenye mambo haya matatu ya tukio, basi haya nawili Ugaidi na Kisasi yana asilimia kubwa kuwa ndio uhalisia. La ujambazi kwangu naona linakosa sifa.

Sasa ukiniuliza mimi kama Yericko Nyerere nitakwambia, kwenye investigations area ukishapata aina ya tukio, ndio unapanga hatua za uchunguzi wako, na kwenye higher intelligence Skils huwa tunaanza na kitu kinaitwa "What is the motive behind?" Tukishajua hicho ndio tunakwenda hatua ya upelelezi kwa ujumla wake.

Sasa Crue ya kiupelelezi bila kuingilia vyombo vya usalama, tuache room hiyo vyombo vifanye kazi yake, tutaendelea kulichambua tukio hili na kadiri siku zinavyosonga na informations zinavyoendelea kumiminika mitaani.

Sio kigogo huyu, kwa jina la hamza?
FB_IMG_1629915071175.jpg
 
Hapo kwenye ugaidi, kwa uchambuzi ulioweka kuna walakini fulani.

Terrorism: “Any act intended to cause death or serious bodily harm to civilians with the purpose of intimidating a population or compelling a government or an international organisation to do or abstain from any act.” United Nations General Report of November 2014

Mkuu, matukio [yote] ya ugaidi yanashabihiana kwenye kuua raia (wanaweza kuwa na sifa ya uraia wao, mahali walipo au uhusiano wao kwa walengwa wa ujumbe wao) ili kufikisha ujumbe wa kuhimiza mamlaka zitende au zisitishe utendaji wa jambo fulani.

Huyu wa tukio la leo alikuwa na nafasi ya kuua raia, ila je kuna raia aliyedhuriwa kwa makusudi?
Je ametoa madai yoyote yanayoamuru mamlaka zitende au zisitende jambo fulani?
Amejitanabaisha kuwa yeye ni gaidi?

Mkuu kweli maswali ni mengi, natumaini wenye taaluma zao na wajibu huu watafanikiwa kutegua hiki kitendawili.

Poleni sana kwa walioondokewa na ndugu/jamaa zao kwenye tukio hili. Majeruhi wapate ahueni wapone mapema.
 
Vyombo vyote vya ulinzi na usalama viwajibike kuchunguza sakata hili kutoka angles zote na kukusanya taarifa za kutosha ili kuepusha matukio kama haya yasijirudie popote Tanzania.

Most likely The Motive behind is needed and the culprit shouldn't been killed.

Let's also ask ourselves as a Nation, are we prepared to timely prevent and manage such situations?We are observing short cuts in combating; Utasikia majambazi idadi Fulani wameuawa na askari na kufanya uchunguzi kuwa mgumu maana mashahidi wote wanakuwa wamefariki/kuuawa. Nawaza tu!
 
Ukiandamana tu akakupiga risasi ukafa kesho anakutangaza kuwa ameuwa jambazi sugu au gaidi.
 
Ni zaidi ya Msaa 8 hivi kupita baada ya tukio la leo 25/8/2021 kubwa kwa nchi yetu, hatujapata kuwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga kwa risasi nadhani tangu Tanganyika ipate Uhuru wake, Ni tukio kubwa kimedani na linatulazimisha tuweke kando siasa zetu chafu tukae chini na tutafakari na kuruhusu taaluma zifanye kazi. Kwanza natoa pole nyingi kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP na kwa ndugu na jamaa wote waliofiwa na makamanda waliokuwa katika oparesheni hii ngumu kabisa.

Tukio hili limenikumbusha mahojiano maalumu niliyoyafanya tarehe 23 June 2021 kupitia Radi Ebony FM, nikachambua ziara ya Rais Samia nchini Msumbiji ambako pamoja na mambo mengine, Tanzania iliteuliwa na SADC kuwa kitovu cha vita dhidi ya Ugaidi. Uchambuzi wangu uko katika Audio/video hii hapo.

Tukio la leo linaweza kushahabiana kinadharia, lakini linaweza kutofautiana kimanti. Kwanza tunakubaliana wote kwamba kumetokea tukio la mauaji. Hili wote tunakubaliana. Pili tukio hili tunaliitaje kwa jina? Hili ni mtihani mgumu kwa jicho la kiraia lakini ni jambo dogo kwa jicho la kiusalama. Ili tupate jina la tukio hili ni lazima tuainishe aina ya matendo katika tukio hili zima ndio yatatupeleka kulipa jina halisi tukio hili na kundi lake halisi.

(1) Ni tukio la Ujambazi? Hapana linakosa sifa ya ujambazi kwakuwa mhusika kwamjibu wa mashuhududa na video za awali zinaonyesha hakushughulika na uporaji wa mali za watu wala bank ya Stanbick iliyopo jirani na tukio. Kwa nadharia hii tukio hili kwenye ujambazi halipo linakosa sifa kuitwa tukio la ujambazi.

(2) Mhusika huyu wa mauaji ni mtu karukwa na akili/ni kichaa? Hapa ni vigumu kutoa majibu ya moja kwa moja kwakuwa ni lazima tupate historia ya nyuma ya mtuhumiwa huyu na kwakuwa amefariki basi historia itapatikana kwa ndugu na marafiki zake wa karibu. Bahati nzuri taarifa za awali zinasema ni mkazi wa Dar es Salaam Upanga. Hivyo naamini hatua hii ya awali itakuwa ishafanywa na vyombo vya usalama.

(3) Inaweza kuwa ni kisasi cha mtu huyu dhidi ya polisi (Serikali)? Hili linaweza kuwa kweli kwakuzingatia video za mtu huyu hakushughulika kulenga risasi raia isipokuwa Polisi tu, uwezekano mwingine unakuja pale mtu huyu anapoonekana kama mtu aliyechanganyikiwa kipiga risasi hovyo hewani licha ya kuwaua polisi wa wili na kupora bunduki zaidi ya nusu saa nzima hakuondoka eneo hilo kujaribu kukimbia hadi polisi wakaja na akajibizana nao. Uwezekano mwingine kwamba yaweza kuwa kisasi binafsi ni pale lugha ya mwili ya mtu huyu inapoonekana akitoa lugha ya ghadhabu kwakuonyesha amewakomoa hasa akijipiga kifuani kwa mkono wake. Hili linaweza kutafrika katika uchambuzi wa mwili wa mtu kwa video. Hoja inaweza kuwa ni kisasi cha nini dhidi ya nani.

(3) Ni tukio la Kigaidi? Uwezekano ni mkubwa kuwa la kigaidi, nikiunganisha na mkutano wa wakuu wa SADC uliofanyika Msumbiji na kuiteua Tanzania kuwa kitovu cha vita, kuna uwezekano mkubwa makundi ya Kigaidi yameamua kutuma salamu kwamba yapo kila pembe ya Afrika. Baadhi ya mashuhuda wanasema mtu huyu hakushughulika sana kulenga raia isipokuwa alishughulika na polisi na wakaongeza kuwa alikuwa anatoa sauti yenye maneno ya lugha inayodhaniwa ni ya kiarabu akijipigapiga kifuani kwamkono wake huku akitamba kwa madaha.

Hili linaweza kuwa tukio lenye uhusiano na makundi ya kigaidi (ISI Somali na Alshababi Msumbiji). Kubwa zaidi ni uwezo wa mtu huyu kutumia bunduki tatu za aina tofauti tofauti, Mafunzo ya matumizi ya silaha SMG na bastola na namna anavyoshika na kuzimiliki inatoa tafsiri kuwa mtu huyu ana mafunzo ya silaha hizi. Muhimu hapa tukae kwenye mambo haya matatu ya tukio, basi haya nawili Ugaidi na Kisasi yana asilimia kubwa kuwa ndio uhalisia. La ujambazi kwangu naona linakosa sifa.

Sasa ukiniuliza mimi kama Yericko Nyerere nitakwambia, kwenye investigations area ukishapata aina ya tukio, ndio unapanga hatua za uchunguzi wako, na kwenye higher intelligence Skils huwa tunaanza na kitu kinaitwa "What is the motive behind?" Tukishajua hicho ndio tunakwenda hatua ya upelelezi kwa ujumla wake.

Sasa Crue ya kiupelelezi bila kuingilia vyombo vya usalama, tuache room hiyo vyombo vifanye kazi yake, tutaendelea kulichambua tukio hili na kadiri siku zinavyosonga na informations zinavyoendelea kumiminika mitaani.

View attachment 1908459
Mtaalam asante kwa uchambuzi mzuri
 
Back
Top Bottom