Tukio la kutisha mkoani mara!!!!!!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukio la kutisha mkoani mara!!!!!!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kadogoo, Jan 20, 2011.

 1. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Inasikitisha kusikia habari hii ya Wananchi mkoani Mara kuchukua sheria mikononi mwao kwa kuchoma moto nyumba 3 za Mchungaji wa kanisa kwa sababu za ushirikina na uchawi! na ku sababisha Mchungaji na familia yake kutoroka na mahali walipo haijulikani!

  Jamani tunaelekea wapi tena huko? gonga hapa: HabariLeo | Mchungaji adaiwa kukutwa na marehemu 3
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  nilipoona neno Mchungaji nikapata hisia kuwa lazima source itakuwa HabariLeo.

  Nadhani wamepewa pesa ya kufanya utafiti kuhusu kinachoendelea makanisani. Siyo bure.
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Habari Leo: Mchungaji adaiwa kukutwa na marehemu 3
  WANANCHI wa kijiji cha Nyankanga, Musoma Vijijini, mkoani Mara wamevamia kwa Mchungaji Paulo Magesa wa kitongoji cha Iginaimwe na kuchoma nyumba zake tatu na kuharibu bustani yake kwa tuhuma za ushirikina.

  Tukio hilo lilitokea Januari 16 saa 3 asubuhi, wakati Mchungaji huyo alipokutwa akiwa na vijana watatu wa kijiji hicho ambao wanasadikiwa walishafariki dunia miaka mingi iliyopita.

  Waandishi wa habari walifika eneo la tukio na kujionea uharibifu mkubwa uliofanywa na wananchi hao, lakini mtuhumiwa na familia yake hawakuwapo, kwa madai kuwa walitorokea kusikojulikana.

  Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho, walidai kuwa Mchungaji huyo alikuwa anatoa huduma za kiroho kwa familia yake pekee alifika kijijini hapo takribani mwaka mmoja na nusu uliopita na kununua eneo la ekari zaidi ya 10 kutoka kwa Marwa Kitamara.

  "Aliuziwa eneo hilo, lakini kitu cha kushangaza baada ya kuhamia vifo vya ajabu ajabu vilianza kutokea, lakini siku ya tukio alikutwa akiwa na watu waliokufa siku nyingi, kuna kijana wa Bweri na mama aitwaye Mama Asha, na mwingine hawakumfahamu jina.

  "Ndipo vijana hao wakapiga yowe na kumhoji kuwa alikuwa anawapeleka wapi na wakati wakiendelea kumhoji watu hao walitoweka kusikojulikana ndipo wananchi walipopandwa hasira na kwenda kuchoma na kubomoa nyumba zake tatu na kuharibu bustani na shamba lake," alisema Mamkama Imanyi wa Iginaimwe.

  Wananchi hao walidai kuwa ilipofika saa 12 jioni aliokotwa kijana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 14 karibu na eneo la Mchungaji huyo akidaiwa ni msukule na baada ya kumhoji anatoka wapi alitaja zaidi ya vijiji vitano na jina lake halijui, ndipo wakamkabidhi kwa polisi wa doria na kupelekwa kituo kikuu cha Polisi mjini hapa.

  Ofisa Mtendaji wa Kijiji hicho, Masau Magalu, alikiri kupokea malalamiko ya wananchi kuwa Mchungaji huyo alikuwa anajihusisha na mambo ya kishirikina lakini Serikali haiamini mambo ya uchawi ingawa walikuwa wanaendelea na uchunguzi wa kubaini ukweli wa jambo hilo.

  "Tulishapata malalamiko kutoka kwa wananchi wetu, lakini sisi Serikali hatuamini mambo ya kishirikina, ingawa tulikuwa tunafuatilia malalamiko na jana (juzi) wananchi walimvamia kwa madai kuwa alikutwa na watu watatu akiwapeleka mjini, ndipo wakachoma na kubomoa nyumba zake tatu na kuharibu mashamba yake na sasa hatujui aliko," alisema Magalu.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Robert Boaz, alisema: "Habari za kuchomewa na kubomolewa nyumba zake na kuharibiwa mashamba tumezipata, lakini cha kushangaza Mchungaji wa Kanisa atawezaje kuwa mchawi.

  "Pia kijana ambaye wananchi wanadai kuwa ni msukule si kweli, kijana yule alikuwa amepotea njia lakini kwa kuwa alikuwa mazingira hayo, wananchi wakamhusisha na tukio hilo, lakini ameshachukuliwa na wazazi wake," alisema Kamanda Boaz.

  Kamanda aliongeza kuwa wanafanya uchunguzi wa kina kubaini wananchi waliohusika na uharibifu huo, ili sheria ichukue mkondo wake kwa kuwafikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

  Taarifa zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya wananchi wa kijiji hicho na mjini hapa zilisema matukio ya kuchomewa nyumba Mchungaji huyo yametokea mara nyingi kwani hata katika maeneo ya Majita, Musoma Vijijini, alichomewa nyumba na kufukuzwa kwa tuhuma hizo hizo za ushirikina.

  Alihamia mjini Musoma na mwaka juzi aliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari baada ya kuchomewa nyumba katika kitongoji cha Zanzibar karibu na Mlima Balima akidai kuwa alikuwa anafanya utafiti wa madini huku akijihusisha pia na masuala hayo hayo.
  My Take

  Kwanza:

  Hata mtu apate daraja la uchungaji anapaswa kupata elimu ya kiwango fulani kuhusu maswala ya kiroho. Ninaomba Habari Leo watupatie CV ya huyo mtu wanayemuita mchungaji.


  Pili:

  Habari Leo limekuwa gazeti la hovyo. Gazeti linaloandikwa (nadhani) na wavuta bangi kama si wabwia unga. Hivi? Inatosha kusema Mchungaji, bila hata kutaja ni wa Kanisa gani? Kama huu si udaku, basi neno udaku halina maana.


  Tatu:

  Habari Leo mumejiingiza kwenye vita ambavyo hamtashinda. Mnaandika habari za Kanisa la Mungu kuliko hata magazeti yaliyosajiliwa kuandika habari za Kanisa. Mbaya zaidi munaadika ushakunaku, uchonganishi na kufuru dhidi ya Kanisa. Hadithi yenu ya leo inapeleka ujumbe kuwa Kanisa la Mungu linafanya mambo ya ushirikina. Hii ni aibu kwenu, kama hamuna cha kuandika, lazima muandike???

  Mimi si muandishi wa habari, lakini nina wasiwasi kama Habari Leo wanaandika taarifa zao kwa kuzingatia weledi na maadili.
   
 4. M

  Mtaka Haki JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 492
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Habari leo!!!
   
 6. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Habari leo
   
 7. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Habari Leo wanajitahidi kukuza dhana dhaifu ya udini kwa manufaa ya serikali ya CCM, Kadri wanavyoeneza propaganda ndivyo JK na serikali yake inavyopoyeza dira, Mungu anaiadhibu CCM kwa kuwa imegeuka genge la wahuni badala ya chama cha siasa.
   
 8. A

  Aine JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Unajua waandishi wengine wanajali kuuza gazeti tu na si kuandika ujumbe sahihi, ameshasema alikuwa anatoa huduma katika familia yake pekee! halafu anamuita mchungaji???? hajafanya utafiti kwamba mtu anayetoa huduma katika familia anaitwa nani?? huku ni kudhalilisha wachungaji na gazeti hili LIOMBE MSAMAHA KWA WACHUNGAJI NA WATU WOTE KWA UJUMLA
   
 9. amanibaraka

  amanibaraka JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  du!
   
 10. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Jamani nafasi ya Boss (Mhariri Mtendaji) wa magazeti haya ipo wazi karibu miaka miwili sasa.
  Anayekaimu hiyo nafasi hana sifa za kitaaluma kuchukua nafasi hiyo. Huyu bwana kwa uchu wa hiyo nafasi yuko tayari kuandika chochote so long as habari hiyo itapendwa na Salva, JK, RA, EL na wengine.

  Na kwa mwendo huu nadhani watachakachua sifa za waombaji ili kumbeba maana huyu ndiye aliyeapia kwa miungu kwamba Dr. Slaa will never be the URT President.

  Ila anapogusa kanisa la Mungu ajue kaingia kwenye anga hatari akumbuke : 1Chroniicles 16:22 Saying; Touch not mine anointed, and do my prophets no harm (KJV)
   
 11. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Jamani nashindwa kuwaelewa! hii habari mbona mnahusisha na CHADEMA na KANISA? kuna uhusiano gani kati ya CDM na Kanisa? mbona kila akitajwa mchungaji au Kanisa harakaharaka CDM inatajwa! sasa hapa kuna agenda gani?
   
 12. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Toa Quote iliyotaja hicho chama.
  Au aliyetajwa kwenye quote yako ndio chama?
  Yaani nyie ndio mnaishusha JF Hadhi.
  You deserve a Life ban, As this is a place of great thinkers but you are not one of them.
   
 13. BULLDOZZER

  BULLDOZZER Senior Member

  #13
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mchungaji = kibwetere
   
 14. M

  Mayu Ngoma New Member

  #14
  Jan 20, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona hawa walitaka kupotosha na kupoteza wananchi kuhusu habari ya ukweli ambayo imetokea huko mkoani mara kwa mh.boxer ambapo walinzi wa muekezaji mmoja wameua mwananchi wa kawaida kwa tuhuma kuwa ngombe wake aliingia kwenye eneo la mwekezaji. Na taarifa ilipotelewa police na kwenye vyombo vingine husika wala hatujaona 'sheira inachukua mkondo sijui mkanda wake'. habari kamili itafuata, bado uchunguzi unaendelea. ofukozi haitaonekana kwenye vyombo vya jk labda ikiwa imeshachakachuliwa.

  Wana habari ebu fanyieni kazi kiapo chenu na sikuongopea watu na kuogopa wengine!
   
 15. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  pumba!!!!!!!!!
   
 16. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Poleni wa mara.
   
 17. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,084
  Likes Received: 4,667
  Trophy Points: 280
  wachungaji wachawi ni kama mama Rwakatare, kila kitu yy, kujilimbikizia mali, rushwa, mlafi wa uongozi, siasa, hana mume, then ana kanisa
  lake kuchukua sadaka za watu ale bure, huu ni uwizi pia mshirikina
   
 18. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  nani ameitaja CDM inahusika kwa mchungaji wa Mara?
   
 19. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Utsababisha JF ipelekwe mahakamani, maana m-mama yule anapenda kesi....

   
 20. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Unajua kuandika lakini kusoma hujui!
   
Loading...