Mkimuyangu
JF-Expert Member
- Oct 5, 2022
- 1,054
- 1,929
Hii ni stori ya kweli kabisa, iliyonifanya nichungulie mauti.
Samahani kwa uandishi mbovu, kwa asili mimi ni muhehe,najiamini sana,sina hata chembe ya woga,linapokujaga swala la woga,nikisema Uoga una tofauti yake, mfano mtu mwingine anaogopa kutembea usiku,au kulala peke yake,na kunakuogopa vitu vya giza kama wachawi au majambazi
Lakini kwangu mimi hakuna ninachoogopa iwe popote pale,nakumbuka kunasiku tulisafiri na boti kupitia ziwa nyasa,kutoka Malawi kwenda Mozambique,tulipofika mwisho wa safari,kila abiria akashika njia yake kwenda kwake,na palikuwa hamna guest,basi nikatoa mizigo yangu nikaweka kwenye mchanga,umbali kidogo kutoka kwenye maji,nikaokota vipande vya miwa vikavu,nikawasha moto,mpaka asubuhi,hiyo unajikuta unashindana na usingizi,hutaki kulala sababu ya usalama wako, na usingizi nao unataka ulale
Siku yenyewe niliyoamua kujivua nyota au kujishusha cheo ilikuwa hivi, kipindi cha korona Mozambique walifunga mipaka,ikawa hakuna kusafiri,tukajikuta inabidi kusafiri kama wezi,yaani mnapita mpakani usiku wa manane kama wezi,mnachokifanya mnakula diri na baadhi ya maskari,mnawapa hera,halafu wanakuja kuwavusha usiku,na wanawaambia ukisikia shaba,utajijua mwenyewe na mmewapa hela
Sasa siku hiyo nilijikuta niko peke yangu msafiri baada ya kufika border,ambayo inabidi nivuke,nikapiga hesabu hawa nikila nao dili la kunivusha watanipiga hela ndefu,
Ikanibidi niamke kama saa nane ya usiku ya Tanzania kwa ajili ya kuanza safari,ukumbuka niko upande wa Tanzania,nikapita freshi uhamiaji ya Tanzania,huku walinzi wakiwa wamelala,nikavuka mto ruvuma ambao unatenganiza mpaka,nikaingia upande wa Mozambique,hapa kuna taa zinawaka,kwa hiyo mwanga ni mkubwa,nikawa napita kwenye vivuli ya miti,nikafanikiwa kuipita border bila kikwazo,ninakokwenda kama umbali wa mita 500 kuna Camp ya askari,ambapo getini kuna maskari,ikabidi niingie porini ili nikatoke mbele yake,ni msituni,nikajikuta natokea kijijini,hapo nimeshakata kama kilomita moja na nusu,inabidi nitembee ya miguu kilomita 20,huko ndiyo nitakuwa salama na ni katikati ya mbuga.
Kuangalia saa inasema ni kama saa tisa na madakika,nikasema hapa nikizubaa hawa jamaa wakinikuta azabu yao ni viboko,ngoja nieendele mbele,mapambazuko yanikutie msituni,nikakata kama nusuu saa hivi,niseme ndiyo naviacha vijiji sasa nitokomee msituni,nikakuta nyumba moja kuna watu wako inje,wakastuka kuniona,ikabidi nijisalimishe kwa kuwasalimia,maana hapa lugha inayotumika ni kiswahili na kiyao,ikabidi waniite na kuniuliza,kulikoni usiku huu,unaenda wapi?nikawadanganya, nimepungukiwa na nauli,nataka hiki kipande cha kilomita 50,nitembee ya miguu,
Wakaniambia kaa kwanza hapo,ili nianze kuhojiwa, sasa tunakuwaga na umafia wetu,unapoona umebanwa,kila ulichonacho ni silaa,ili upate huruma
Nilikuwa na mikate na juisi,nikwapa watoto zao wadogo,kuonyesha kama huruma na upendo,mala nyingi binadamu ukimuonyesha upendo mwanaye,anakuwaga na huluma
Wakaniambi,alikuja gavana wa jimbo,akawaambia mkiona mgeni yoyote amevuka border,inabidi mkaripoti polisi,maana yake ameleta corona,pili wakaniambia yaani huu mda unaotembea,unaenda kuliwa na simba sasa hivi,da!! nilihisi tumbo linaunguruma,wakaniambia itabidi ukae mpaka kuanze kupambazuka ndiyo uanze safari,hiyo mida ilikuwa inakwenda kwenye saa 10 kasoro,
Nikaka pale huku naota moto,ilipofika saa 11 kama na nusu hivi,wakaniambia unaweza kwenda,nilikata nikasema bado mapema
ilipofika saa 12 alfajiri safari ikaanza,naikata mbuga ya wanyama pana kilomita 20 kwenda kukipata kijiji kinachofuata,nikaanza kuacha nyumba,mala mashamba,likaanza pori kidogokidogo,badaye nikaanza kuona miguu ya wanyama wadogowadogo waliokuwa wanacheza usiku,baadaye nikaingia kwenye msitu ulioshonana,huku najitaidi kupambana na uchovu,begani nina begi la kilo kama 15,
Ikanipita pikipiki,ilikuwa na watu wamepakizana,ilikuwa kama saa 2 asubuhi hivi,kumetulia sana,ni sauti za ndege na nyan, ndiyo zinazosikika,
NIkawa naangalia nyayo zilizokanyagwa na pikipiki inamaana za jana,na nyayo zilizokanyaga pikipiki inamaana za leo,alhamdulilah nikakutana na unyayo wa tembo ambao umekanyaga juu ya pikipiki,inamaana huyu tembo kama ingekuwa vipi ningekutana naye,kidogo uwoga ukaanza kuniingia na uchovu ndani huku nikiwaza,kama nitakutana nao nifanyaje?kupanda juu ya mti haiwezekani labda uwe mti mkubwa kama mbuyu,kukimbia nasikia tembo ana mbiyo sana,ikabidi niwe namuomba Mungu tu
Mara nikakutana na unyayo wa simba ambao umekanyaga,juu ya pikipiki,kwa kweli nilichanganyikiwa na kuanza kujilaumu kwa ujasiri wangu,nikasema hapa leo sijui kama kunakupona, nikakata shauri kama litatokea gari linakokwenda kule ninakotokea,itabidi nipande tu,bila kujali nitakamatwa au vipi huko nitakakokwenda,kila nikikata msitu naona haupungui wala hauongezeki inamaana niko katikati ya msitu,
Badaye sana nikaona msitu unapungua kidogokidogo mpaka nilipoanza kuona mashamba ya watu,nikajua da leo nimepona kufa,na huu ujasiri wangu najivua kuanzia leo,siyo kila kitu ni cha kukifanyia ujasiri