Tukimalizana na madarasa tujenge nyumba za walimu

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,724
5,901
Nitoe Kongole nyingi kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 10 yanayoendelea kujengwa nchi nzima, lengo ni lile lile la kuboresha Elimu!

Hata hivyo kwa mustakabali mzima wa kuweka ufanisi katika ufuatiliaji nashauri nguvu nyingine kama hii iwekwe kwenye ujenzi wa Nyumba za walimu!

Bila shaka tunajua yapo maeneo ambayo hata kupata nyumba ya kupanga ni changamoto! Na hivyo walimu hulazimika kukaa mbali na shule,

Lakini kama tujuavyo walimu hawana posho ya malazi na hivyo hulazimika kujibana kutokana na mshahara huo huo,

KWA maoni yangu hakuna mwanafunzi bila mwalimu,

Tunaofahamu mazingira ya vijijini na mijini tunaona jinsi walimu wanavyoishi maisha magumu!

Hebu tutafute pesa "PAHALA"
tuwajengee walimu nyumba zenye hadhi wakae shuleni na tuwapunguzie mzigo wa Kodi na umbali tutaona matunda yake!
Nawasilisha.
 
Na ya mtendaji kijiji
Na ya mtendaji kata
Na ya mganga
Na ya bwana shamba
Na ya afisa afya
Na ya polisi kata

Walimuu bwanaa mnajionaga special sanaa pyuuu..
 
Na ya mtendaji kijiji
Na ya mtendaji kata
Na ya mganga
Na ya bwana shamba
Na ya afisa afya
Na ya polisi kata

Walimuu bwanaa mnajionaga special sanaa pyuuu..
Ndio wote wanatakiwa kujengewa nyumba,
Kuna ubaya kwani mkuu?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom