Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
- Thread starter
- #81
Kama elimu kuwa BURE kweli ni imekuwa BURE KABISA!Elimu bure inatekelezwa
Mikopo kwa wanafunzi elimu ya juu inafika kwa wakati
Ukarabati wa Shule kongwe unamalizika
Michango ya kipuuzi mashuleni imeondolewa
Walimu wamelipwa madeni yao
Miundombinu isiyovutia kwa ujifunzaji na ufundishaji
Maabara za Kikwete hadi leo bado ni magofu kwa asilimia kubwa
Mitaala mipya isiyokuwa na vitabu shule za msingi (wanaambiwa waazime shule za binafsi)
Walimu kila wakati wako stressed na bize kwa uhakika usio na kikomo (japo hili lingefanyika kwa akili ni zuri zaidi)
Upungufu wa madawati na ofisi za walimu, vyoo, Maabara, maktaba nk
Kwa hayo yote, kwa watu makini kipi kilitakiwa kuanza : kuboresha Miundombinu ya shule na maslahi ya walimu au kufuta ada na michango mingine kisha kuwarundika watoto wa watu madarasani huku wakikaa kwa kubanana na wengine chini kabisa!
Halafu, hivi viongozi wa serikali hii wao hawapendi watoto wao wasome bure!? Mbona watoto wao hatuwaoni huko!? Watoto wao wanasoma wapi!? Kwanini wanatengwa na watoto wetu!?!