Tukiacha unafiki, hadi leo utawala huu umeifanyia nini Tanzania?! Umewasaidia nini watanzania!?

KILIMO:
Pembejeo zinawafikia wakulima kwa wakati
Korosho imeimarika haswa
Mahindi ya kutosha hadi wale waliotaka tutangaze njaa wanaona soni
Pamba wamepata soko la MsD
Madalali wa kununua chakula shambani wanepigwa pini
Ushuru wa kipuuzi umefutwa ..
Mifugo yetu inaendelea kutambuliwa
Vifaranga vya Magonjwa kutoka nje vinateketezwa
Migogoro ya wakulima na wafugaji imepungua
Kiwanda cha matrekta Kimezinduliwa
NMC imerudishwa serikalini

.....NAULIZA NIENDELEE?
Kodi za kikoloni zimezidi, wakulima wa pareto, karangaz korosho, mahindi vilio tupu.
 
SGR...Inajengwa
Barabara zinakamilika
Vivuko vinaundwa
Madaraja mfano Kilombero yamekamilika
Fly over zinakamilika
Mabasi ya mwendo kasi yanaongezwa
Ajali barabarani zinapungua
TTCL Inafufuka
ATCL inasimama
......HIYO NI SEKTA YA KWANZA...NIENDELEE?
Naona kila kitu ndio kinaanza! Hahahaaa umeambiwa kilichofanywa tayari na serikali hii dhalimu.
Hii awamu imeleta laana tu badala ya baraka.
 
Hii yote ilianza kipindi cha KIKWETE! leta ambayo magufuli kaianzisha mwenyewe!
Huna akili.Kama ulisikiliza uzindizu wa hospital ya mloganzila ni kuwa jk alitoa bil 14 na jpm alivyoingia alitoa bil 25 ili kukamilisha ujenzi.Sasa kwa hili moja tu utafuta juhudi za jpm? Ok tufanye hakuna analofanya.
 
Ungekua umefika Kinyerezi kuona mradi wa umeme ulipofika na hakika huu uzi usingefungua.Tembea uone sio kujifungia ndani na kushinda kwenye page ya Dada wako wa marekani.Nimepita barabara ya babati kondoa kutokea Dodoma,kazi inayofanyika ktk ujenzi wa hii barabara sio ndogo.TEMBEA UONE.
 
Hamna kitu hapo.Kazi kukuza mambo kwa kutumia media kuaminisha watu mmefanya mambo makubwa.

Hiyo kesi ya IPTL unashitaki waliochotewa hela wakati watumishi wa serikali(BOT) waliowezesha hizo fedha kutoka wako maofisini alafu mnatuambie eti kuna kesi inaendelea.

REA huo ulikuwa ubunifu wa serikali ya JK ambapo sisi watumiaji wa maji na umeme tunakatwa hela ili zitumika kusambaza umeme vijijini na hivyo sio ubunifu wa awamu hii.

Isitoshe huu ni ubunifu wa kumnyonya mtanzania masikini kwa kukata hela yaka anayonunulia umeme na maji.

Miradi mingi mnayojisifu nayo baaadhi ni kwa misaada ya wafadhili na sio kwa fedha zetu za ndani maana vyanzo vya mapato vipya hakuna zaidi ya TRA na Polisi kukamua watanzania.

Nyie ni watu wa makelele mengi tu lakini la maana hakuna zaidi ya kukopa na kununua ndege na kujenga sijui flyover na vitu kama hivyo.

Kwa kifupi mafanikio yenu ni kutuongezea deni la Taifa kwa miradi isiyo na tija kwa watanzanua walio wengi na ndio maana umasikini umeanza kuongezeka na watoto wanaodumaa nao wanaongezeka.
Ok, Hii serikali hakuna inachofanya.furahi.
 
Tumelipwa kishika uchumba cha US$300 million na barrick.

Chezea maguwfool wewe
 
If wishes were horses ,fools could ride. Hapo waingereza wana maana gani? Ni msemo ambao nadhsni sio tusi. Ila unaweza kuwa na maana kuwa mawazo mema usianze kusheherekea kuwa umetimza hayo wakati bado uko kwenye mipango tu. Hayo yanahusu SGR, reii. Dawa hospitali sizioni .Umeme a Stiegler gorge ni mpango
. takwimu za pesa za wanufika mikpo ya ELIMU university haziwani na idadi ya wanufaika,. Mipango ni kitu chema lakini tujivunie utekelezaji ukitimia.
 
MAMBO YA NDANI
Ajali za barabarani zimepungua
Mauaji ya Albino na Vikongwe yamepungua
Wahamiaji haramu wanakamatwa
Pasport za kieletroniki zimepatikana kwa bei chee ba sio ile ya wapiga dili.
Matukio ya moto yanadhibitiwa kwa wakati yaani zile stories za faya walikuja bila maji hazipo
Wizi wa mabenki umepoa despite vyuma kukazwa
Mabasi kutekwa ni historia

..........NIENDELEEE AU NISIENDELEE??
Watu...wanasema ...ENDELEA!
Kwenye kudhibiti mwendo hapo sawa japo nia sio kuokoa abiria ni kupiga hela za fine, ajali za moto zitatoka wapi wakati umeme unakatika? Wizi wa bank utatoka wapi wakati hakuna hela? Mabasi yatatekwa vipi wakati safari zimepungua?
 
Ukiona mtu analamikia serikali ujue hyo ni mvivu...fanya kazi uone kama utakua na huo muda wa kuotoa lawama tafuta hela kwa jasho utapata yani nikiona mwanaume analalmikia serikali daah namchukulia tofauti san
 
Hilo ni swali fikirishi, naomba uorodheshe kikubwa tulichofikia hadi leo ukilinganisha na utawala uliopita!

Kama ni Bara Bara, zilikuwepo na zilikuwa zinaendelea kujengwa!

Watumishi wa umma vilio vilikuwepo vya mishahara midogo japo wakilinganisha na sasa, wanaona bora zaman (hawa kila siku wao ni kulia tu ila kwa sasa wamezidishiwa stress)

Hayo ni yangu machache, nisaidieni kuleta mapya mazuri yakujenga Tanzania mpya yaliyoanzishwa awamu hii

1. Mafisadi na wazembe wameshugulikiwa.
2. Matumizi mabaya ya rasilimali za taifa yamekomeswa
 
1. Mafisadi na wazembe wameshugulikiwa.
2. Matumizi mabaya ya rasilimali za taifa yamekomeswa
1. Mahakama ya mafisadi imetia hatiani wangapi hadi sasa!? Mafisadi wangapi wameshughulikiwa

2. Yamedhibitiwa kwa nani na kwa sasa nani anatumia rasilimali hizo za umma pasipokujali wengine!?

Hapa kilichofanyika ni kama kuhamisha kutoka kwa huyu kwenda kwa yule!! Lakini hili wengi wenu hamuwezi kuliona labda kwa baadae!
 
Tunapoendelea kuacha unafiki,tujiulize sisi tumefanya nini?kwa serikali,kwa taifa,kwa familia zetu.
Utakuta hapo alipo hata viatu vya kuvaa kaazima asichomwe na miba...

Loosers...Endeleeni kujiliwaza by the time tutakapokumaliza kujenga empire zetu tutawaajiri na vizazi vyenu ili viendeleze complains mlizowarithisha...
 
Back
Top Bottom