Tukiacha unafiki, hadi leo utawala huu umeifanyia nini Tanzania?! Umewasaidia nini watanzania!?

AFYA:
Muhimbili imeboreshwa
Wagonjwa wanakwenda kutibiwa nje hada vigogo wamepungua
CT SCAN Zinapiga kazi
Hospitali yaMlongazila imeanza kazi
Huduma ya dialysis kuanza kutolewa Mlonganzila
Huduma za Tiba ya mionzi kutolewa kwenye hospitali za kanda
Hospitali za mikoa zimepandishwa hadhi
Ujenzi wa Theatre kwenye vituo vya Afya umepamba moto
Bajeti ya dawa imepaa kutoka bilioni 20+ hadi bilioni 200+
MSD inaagiza dawa kutoka kwa Manufacturers na sio wapiga dili
Upatikanaji wa dawa muhimu ni zaidi ya 80%
Coverage ya BIMA ya afya kwa wote inaendelea vyema refer Toto Afya cards n.k
Kitengo cha kupambana na Majanga kimeboreshwa
Matukio ya ubakaji na uonevu wa kijinsia yanapungua
Albino wapo salama
Viwanda vya dawa vinajengwa

........UNATAJA NIENDELEE.....?TUSIKIMBIANE HAPA!
 
Tunapoendelea kuacha unafiki,tujiulize sisi tumefanya nini?kwa serikali,kwa taifa,kwa familia zetu.
Kwa serikali nitaandamana kupinga upuuzi wake. Kwa taifa nitaandamana kuhakikisha amani,uhuru na usawa vinatawala. Kwa familia nitaamdamana ili kuwatengenezea misingi bora kwa maisha ya kesho.
 
Ww bado sana. Unajiuliza nchi imekufanyia nini. Badala ujiulize nchi umeifanyia nn.
Mimi natimiza wajibu wangu kama raia wa nchi hii, kwa kulipa kodi. Lakini kodi zinaishia mifukoni mwa wajanja wa CCM, huku wakitudanganyia 'vimaendeleo' uchwara, kwa kisingizio kasungura kadogo.

Pili, napiga kura kuchagua viongozi ninaoona watafaa kwa kuongoza mapambano ya maendeleo. Lakini uchaguzi siyo huru na wa haki. Hivyo kura yangu inaishia kutokuwa na maana.

Na tatu, nikitoa madukuduku yangu juu ya hayo masuala mawili, naitwa mchochezi!

Sasa chifu, unataka nifanye zaidi kama raia? Nafikiri hakuna la kufanya zaidi ya people's revolution.
 
SGR...Inajengwa
Barabara zinakamilika
Vivuko vinaundwa
Madaraja mfano Kilombero yamekamilika
Fly over zinakamilika
Mabasi ya mwendo kasi yanaongezwa
Ajalia barabarani zinapungua
TTCL Inafufuka
ATCL inasimama
......HIYO NI SEKTA YA KWANZA...NIENDELEE?

Acha ushamba Tanzania hakuna fly over vile ni vivuko tu kwenye msongamano. Yaan ni kama madaraja ya manzese, kimara, morocco na furahisha mwanza ila hyo yanapita magari ndio utofaut. Fly over mchezo unadhan, angalia dunian huko flyover kilomita zaiya 10 mzigo upo juu tu.
 
MAMBO YA NDANI
Ajali za barabarani zimepungua
Mauaji ya Albino na Vikongwe yamepungua
Wahamiaji haramu wanakamatwa
Pasport za kieletroniki zimepatikana kwa bei chee ba sio ile ya wapiga dili.
Matukio ya moto yanadhibitiwa kwa wakati yaani zile stories za faya walikuja bila maji hazipo
Wizi wa mabenki umepoa despite vyuma kukazwa
Mabasi kutekwa ni historia

..........NIENDELEEE AU NISIENDELEE??
Watu...wanasema ...ENDELEA!
 
Acha ushamba Tanzania hakuna fly over vile ni vivuko tu kwenye msongamano. Yaan ni kama madaraja ya manzese, kimara, morocco na furahisha mwanza ila hyo yanapita magari ndio utofaut. Fly over mchezo unadhan, angalia dunian huko flyover kilomita zaiya 10 mzigo upo juu tu.
Daraja la Kigamboni limekamilika....Nilipitiwa kidogo!!
 
SGR...Inajengwa
Barabara zinakamilika
Vivuko vinaundwa
Madaraja mfano Kilombero yamekamilika
Fly over zinakamilika
Mabasi ya mwendo kasi yanaongezwa
Ajali barabarani zinapungua
TTCL Inafufuka
ATCL inasimama
......HIYO NI SEKTA YA KWANZA...NIENDELEE?

SGR...Inajengwa
Barabara zinakamilika
Vivuko vinaundwa
Madaraja mfano Kilombero yamekamilika
Fly over zinakamilika
Mabasi ya mwendo kasi yanaongezwa
Ajali barabarani zinapungua
TTCL Inafufuka
ATCL inasimama
......HIYO NI SEKTA YA KWANZA...NIENDELEE?
Hii yote ilianza kipindi cha KIKWETE! leta ambayo magufuli kaianzisha mwenyewe!
 
Elimu bure inatekelezwa
Mikopo kwa wanafunzi elimu ya juu inafika kwa wakati
Ukarabati wa Shule kongwe unamalizika
Michango ya kipuuzi mashuleni imeondolewa
Walimu wamelipwa madeni yao
Mikopo ya wanafunzi inafika kwa wakati
 
MADINI:
Makinikia yamepigwa kabali
Almasi zimekamatwa
Sheria za kusomamia Rasilimali zimebadilishwa kwa manufaa ya nchi
Mererani imepata ukuta ndani ya miezi minne
Mauzo ya Tanzanite yamepaa kwa jina la TZ
Gulio la Tanzanite linafanyika Mererani
Mwezi wa Sita tunasubiri mzigo kutoka Barrick huku majadiliano ya kodi yetu yakiendelea..
.........

UNAULIZA SERIKALI IMEFANYA NINI.....HAHAHA....ENDELEA KUFUATILIA NA NI HAKI YAKO KUULIZA ILA UNAWAJIBIKA KUFUATILIA NA KUWA MKWELI
 
Tunapoendelea kuacha unafiki,tujiulize sisi tumefanya nini?kwa serikali,kwa taifa,kwa familia zetu.
Sisi tumekamuliwa kodi...au ulitaka tufanyeje...twende ikulu kufyeka bustani..ama tuingie office zao na sisi tupige kazi....sisi tumepafanyia pakubwa sana serikali kuliko wao vitambi msuuzo...wanatukamua kodi tunasubiri return yao..
 
NISHATI
Lile dubwana la IPTL limedhibitiwa vilivyo ndio maana wapiga dili mnalia
Umeme vijijini kupitia REA unawaka...ikumbukwe chadema na CUF walitusemea tukakosa fedha za MCC ila tulisimama kidete kuhakikisha mradi unaendelezwa kwa fedha za ndani(yaani Punda afe ili mzigo ufike) na hivi jana tu Waziri kazindua umeme Oljoro huko Arusha.
Umeme wa kinyerezi unawaka
Stieglars gourge iko mbioni kuanza yaani wakandarasi wameshakuwa shortlisted
.............
Kana wewe ulikuwa kishoka wa Tanesko lazima vyuma vikaze na visisikie grisi!!
 
MAJI:
Miradi mikubwa ya Maji imezinduliwa mfano ni Sengerema na Longido.
Hivi umesahau uzinduzi wa mradi wa maji Ruvu?hadi mkaanza kuuliza Makonda kafuata nini?
...........
Kitila Mkumbo yumo humu atakuja kukushushia Nondo za maji .....SI UNATAKA CHAI USILALAMIKE INAUNGUZA!!

NAONA UMEKIMBIA MADA JE NIENDELEE??
 
UTALII:
Tuliongeza VAT wapiga dili mkatukana sana na mkaja na mikwara yenu mbuzi eti watalii watapungua .....bullshit....sasa watalii na mapato ya utalii yanedouble.
Ujangili wa Tembo umepungua
Majangili wamekamatwa na kuhukumiwa
Mali za Wizara ya maliasili zinarudishwa
...............

Niendelee au umechoka?
 
Back
Top Bottom