Tukiacha unafiki, hadi leo utawala huu umeifanyia nini Tanzania?! Umewasaidia nini watanzania!?

Elimu bure inatekelezwa
Mikopo kwa wanafunzi elimu ya juu inafika kwa wakati
Ukarabati wa Shule kongwe unamalizika
Michango ya kipuuzi mashuleni imeondolewa
Walimu wamelipwa madeni yao
Kama elimu kuwa BURE kweli ni imekuwa BURE KABISA!

Miundombinu isiyovutia kwa ujifunzaji na ufundishaji

Maabara za Kikwete hadi leo bado ni magofu kwa asilimia kubwa

Mitaala mipya isiyokuwa na vitabu shule za msingi (wanaambiwa waazime shule za binafsi)

Walimu kila wakati wako stressed na bize kwa uhakika usio na kikomo (japo hili lingefanyika kwa akili ni zuri zaidi)

Upungufu wa madawati na ofisi za walimu, vyoo, Maabara, maktaba nk

Kwa hayo yote, kwa watu makini kipi kilitakiwa kuanza : kuboresha Miundombinu ya shule na maslahi ya walimu au kufuta ada na michango mingine kisha kuwarundika watoto wa watu madarasani huku wakikaa kwa kubanana na wengine chini kabisa!
Halafu, hivi viongozi wa serikali hii wao hawapendi watoto wao wasome bure!? Mbona watoto wao hatuwaoni huko!? Watoto wao wanasoma wapi!? Kwanini wanatengwa na watoto wetu!?!
 
Hilo ni swali fikirishi, naomba uorodheshe kikubwa tulichofikia hadi leo ukilinganisha na utawala uliopita!

Kama ni Bara Bara, zilikuwepo na zilikuwa zinaendelea kujengwa!

Watumishi wa umma vilio vilikuwepo vya mishahara midogo japo wakilinganisha na sasa, wanaona bora zaman (hawa kila siku wao ni kulia tu ila kwa sasa wamezidishiwa stress)

Hayo ni yangu machache, nisaidieni kuleta mapya mazuri yakujenga Tanzania mpya yaliyoanzishwa awamu hii
Jiulize kwanza wewe umeifanyia nini nchi yako tanzania..
 
Wewe mpaka hivi sasa umeifanyia nini Tanzania hata siku ukifa uje kukumbukwa vizazi kwa vizazi?
 
Kwa serikali nitaandamana kupinga upuuzi wake. Kwa taifa nitaandamana kuhakikisha amani,uhuru na usawa vinatawala. Kwa familia nitaamdamana ili kuwatengenezea misingi bora kwa maisha ya kesho.
Ebu toa hilo "nita" weka "nime" hili twende sawa kulingana na swali lako.
 
Ngoja nikudanganye mtoa post.
utawala huu umepandisha sana ada na michango mashuleni,hivyo wazazi wengi kushindwa kusomesha watoto wao.
utawala huu umefukuza wafanya biashara wote wadogo waache kuuza vitu katikati ya miji.
utawala huu umefanya watu kuwa wazembe sana makazini.
utawala huu umekuwa na safari za nje za mara kwa mara nakadhalika.
pole kwa kukudanganya.
 
Utakuta hapo alipo hata viatu vya kuvaa kaazima asichomwe na miba...

Loosers...Endeleeni kujiliwaza by the time tutakapokumaliza kujenga empire zetu tutawaajiri na vizazi vyenu ili viendeleze complains mlizowarithisha...
Duuh!
 
Tunapoendelea kuacha unafiki,tujiulize sisi tumefanya nini?kwa serikali,kwa taifa,kwa familia zetu.
Sisi tumesoma kwa bidii tena bila mikopo, halafu BAKAYOKO katunyima ajira
- Tukaamua kufanya kazi yoyote hata ya ulinzi SEKTA BINAFSI, BAKAYOKO akasema SITES zote za UMMA zilindwe na SUMA JKT, Kampuni binafsi zikakoswa SITES zikatupunguza kazi.
- Tukataka tuchukue angalau vipesa vyetu tulivyokuwa tukichangia NSSF/PPF wakati tukiumwa na mbu, ili hata tufungie GENGE maisha yaendelee, BAKAYOKO katudhulumu hizo pesa ili aziinjoi yeye na BASHITE wake
- Mpaka sasa tupo hatuna usalama na hatujui Jana KAHOJIWA ASKOFU NJAMA, leo atafuata nani ?
- Juzi kauawa AQUILINE ni nani anafuata ?

MUNGU TUNUSURU na JINAMIZI HILI !
 
Hamna kitu hapo.Kazi kukuza mambo kwa kutumia media kuaminisha watu mmefanya mambo makubwa.

Hiyo kesi ya IPTL unashitaki waliochotewa hela wakati watumishi wa serikali(BOT) waliowezesha hizo fedha kutoka wako maofisini alafu mnatuambie eti kuna kesi inaendelea.

REA huo ulikuwa ubunifu wa serikali ya JK ambapo sisi watumiaji wa maji na umeme tunakatwa hela ili zitumika kusambaza umeme vijijini na hivyo sio ubunifu wa awamu hii.

Isitoshe huu ni ubunifu wa kumnyonya mtanzania masikini kwa kukata hela yaka anayonunulia umeme na maji.

Miradi mingi mnayojisifu nayo baaadhi ni kwa misaada ya wafadhili na sio kwa fedha zetu za ndani maana vyanzo vya mapato vipya hakuna zaidi ya TRA na Polisi kukamua watanzania.

Nyie ni watu wa makelele mengi tu lakini la maana hakuna zaidi ya kukopa na kununua ndege na kujenga sijui flyover na vitu kama hivyo.

Kwa kifupi mafanikio yenu ni kutuongezea deni la Taifa kwa miradi isiyo na tija kwa watanzanua walio wengi na ndio maana umasikini umeanza kuongezeka na watoto wanaodumaa nao wanaongezeka.
Kubuni ni jambo jingine. Kutekeleza ni jambo jingine. Unakumbuka Mkukuta na mkurabita?
 
aiseee mimi mtu yeyote asizungumzie kuhusu elimu kwa hii serikali maana naweza hata kumtemea mate. Vituko vinavyoendelea kwenye sekta ya elimu hata havielezeki. You are talking of mikopo,

1. hata hufikirii kwamba serikali inawapa mikopo wanafunzi wachache kipindi hiki kuliko hata kipindi cha Kikwete?
2. Kwa mara ya kwanza tumeshuhudia wanafunzi wa kada ya afya wakinyimwa mikopo.
3.This time kupata mkopo mpaka uwe hauna atleast mzazi mmoja, nimeshuhudia watu wakifake vyeti ya vifo vya wazazi wao ingali wazazi wao wako hai, ili tu mtu apate mkopo.
4. Wanafunzi wanapata Hela ya kujikimu tu, wengi wao hawalipiwi ada. I have proven it.
 
Back
Top Bottom