Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,086
- 6,568
Wanabodi wa JF hili ni bandiko linalohitaji majibu chanya kwa mustakabali wa taifa letu.
Maana kila kukicha wanasiasa wa upinzani wamekuwa na munkari wa kutaka nchi yetu iwekewe vikwazo hasa na taifa la marekani kwa kile wao wanafikiri kuwa ni msaada wa kwao ili kupata manufaaa ya kisiasa.
Mfano kipindi taifa ketu limegubikwa na matukio ya raia kutekwa na kupotea , serikali ya Usa wakati huo ilimuwekea zuio la kutoenda Usa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Kwa ufupi wapinzani walifurahi sana maana waliona sasa hii kwao ni adhabu tosha kwa watesi wao. Usa ilienda mbali na kuweka zuio la watanzania wote kutocheza bahati nasibu ya green card kwa watanzania wasiende Usa kusaka maisha.
Pia baada ya uchaguzi kuisha wapinzani wamelalama sana na cha kushangaza serikali ya Usa wakati huo iliweka zuio kwa waliokuwa wasimamizi wa uchaguzi Tanzania bila kutaja majina yao wasikanyage Usa.
Je, haya mazuio ya kutokanyaga Usa yanayowekwa dhidi ya watanzania yana manufaa gani kwa upinzani mpaka wafuasi na viongozi wakenue meno nje? Je toka Paul Makonda awekewe ribiti kwenda USA Upinzani hapa Tanzania umenufaika na nini?