Tujikumbushe ya Adam Malima na ulimbukeni wa madaraka

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
1,959
872
SUALA la kuibiwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, si la mchezo hata kidogo kama kweli tunataka kuheshimu utawala wa sheria na maadili kwa mtumishi wa umma kama yeye, tena mwanasiasa.

Sasa, kwa mujibu wa vyombo vya habari, vikimnukuu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, hebu tuangalie alichoibiwa waziri huyo:

1.Laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya sh milioni 5.6.
Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni sh milioni moja.

2.Simu tatu, ya kwanza Nokia C6 ya sh 500,000, Nokia E200 ya sh 250,000 na Blackberry yenye thamani ya sh milioni 5.5.

3Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya sh milioni 2.5.

4Dola za Marekani 4,000 ambazo ni sawa na sh milioni 6.5.

5.Fedha taslimu sh milioni 1.5.

6.Kadi mbili za benki.

7.Mabegi matatu ya nguo.

8.Baraghashia mbili zenye thamani ya sh 50,000.

9.Nyaraka mbalimbali za serikali.

Pia awali ilitajwa na vitu hivi:

Pasipoti mbili za kusafiria (zimeokotwa jalalani karibu na hoteli).
Lakini bahati yake hakuibiwa silaha hizi, Bastola moja na bunduki iliyotajwa bila aibu kuwa ni SMG (Sub-Machine Gun).

UCHAMBUZI RAHISI

Kuna element ya excessiveness kwenye orodha ya vitu hivi. Kwa maoni yangu huu ni ulimbukeni kama wa hadithi ya zuzu aliyeshinda bahati nasibu akaamua kununua kila kitu mtaani kwake, hadi kituo cha basi.

Waziri kwa mishahara yetu ni mtu maskini labda kama ni mwizi.

Ndiyo, yeye ni mbunge mwenye maposho, lakini bado alipataje mali zote hizi?

Katika hali ya kawaida, mwanasiasa anasafiri na laptop tatu za nini?
Huu ni ulimbukeni wa kujua kompyuta na kuweza kuzipata kirahisi au kupewa hovyo hovyo tu; vinginevyo nini kinaweza kuwa sababu?

Vinasa sauti, je, yeye amekuwa mwandishi wa habari au mpelelezi anayetafuta ushahidi wa sauti? Nini hasa?

Simu tatu, bahati mbaya ni utamaduni wa hapa nchini Tanzania lakini pia sijawahi kusikia Blackberry ya gharama zote hizi karibu zaidi ya dola 3,400 za Marekani.
Hiki ni kioja na ushamba mwingine. Ina nini hiyo simu? Inavaa chupi?

Pete mbili ni sawa lakini bado alipoongea na waandishi alikuwa amevaa mapete mengine. Sasa yote ya nini?
Dola za Marekani zote hizo kwa safari ya vijijini ni za nini? Au alizitoa huko huko?
Fedha za Tanzania nadhani ni sawa maana yake alihitaji kulipia gharama kadhaa.

Pia, kadi mbili za benki ni sawa na hata mabegi matatu ya nguo si ajabu, kama alikuwa na safari ndefu na hata baraghashia mbili si tatizo.
Nyaraka za serikali, hii ni fedheha kubwa kwa kuwa kama naibu waziri alipaswa kujua jinsi ya kutunza nyaraka za serikali mara aingiapo hotelini au popote pale. Huwezi kuziweka nyaraka nyeti hovyo hovyo tu.
Pasipoti mbili zote za nini? Alihitaji kwenda nazo Morogoro za nini?

Huenda moja ni ya kidiplomasia na nyingine ya utumishi serikalini ama ya kiraia, lakini za nini zote hizo?

Kwenye silaha hapa ni suala la uhalifu kwa mujibu wa sheria zetu labda kama kuna maelezo mengine.
SMG ni silaha ya kivita, labda kama yeye na polisi wa Morogoro wanamaanisha kitu kingine kwa kutumia maneno "SMG".

Huu ni uvunjaji wa sheria na wala hakuna haja ya kujiuliza kwamba anaogopa nini au analinda nini, mbona ameshindwa kulinda mali alizoibiwa?

Ingeibiwa angekuwa amewaweka raia wengi sana na hata polisi hataraini. Nashangaa wale waandishi hawakuuliza mapema ili tupate maelezo. SMG?

Hii ninayoita element ya excessiveness ni ulimbukeni wa kiafrika haswa kwamba sasa una madaraka, kwa hiyo unataka kila kitu kijazane kwako tu kwa kuwa hela zipo na "haki" ipo hata kama haikubaliani na sheria zetu.

Mavitu, makompyuta, mahela, masilaha, mavinasa sauti, mapete, madude mengi tu - Swali ni je, kuna busara hapo? Kuna utu-uzima hapo? Hii ni sifa nzuri ya kiongozi kweli kujijazia mavitu hovyo hovyo tu na kuishiwa kuibiwa kirahisi namna hii bila haya?

Lakini kutokana na utamaduni wetu wa kulindana unaojengeka siku hizi, huyu hataguswa.

Hii ni aibu kubwa mno kwa taifa letu na yeyote anayetetea mambo kama haya, hana nia njema na taifa hili. Pana tatizo hapa, ni zaidi ya kuibiwa naibu waziri fulani.


Chanzo Tanzania Daima Jumatano machi 14, 2012
email_open_log_pic.php
 
Huyu jamaa kwani alikua anakaa hapo Moro kwa muda gani? Huko alikotoka hana familia? Kama hapo hotelini tu ana vitu vyote hivyo, huko kwake si ndio atakua na makontena yamejaa vitu vya thamani?
Jamani hii nchi, halafu eti mnasema ni maskini. Kwi kwi kwi kwi kwi!!!
Nchi hii maskini ni wewe tu unayelia, wengine wanaelea kwenye bahari ya utajiri.
 
Huyu jamaa kwani alikua anakaa hapo Moro kwa muda gani? Huko alikotoka hana familia? Kama hapo hotelini tu ana vitu vyote hivyo, huko kwake si ndio atakua na makontena yamejaa vitu vya thamani?<br>
Jamani hii nchi, halafu eti mnasema ni maskini. Kwi kwi kwi kwi kwi!!!<br>
Nchi hii maskini ni wewe tu unayelia, wengine wanaelea kwenye bahari ya utajiri.
<br>
Na huo ulikuwa ni mtoko wa Morogoro tu,fikiria akiwa anaenda Canada inakuwaje. Kunauwezekano home kwake akawa na AK 47 au hata ile ya kutungulia ndege, waandishi walisahau tu kumuuliza vizuri
 
kwa hilo la pete nawapongeza wezi waliomuibia.ingawa nahofia usalama wao.maana yale mapete yanaonekana hayakuwa ya kawaida.yasije yakawatokea puani.mtoto wa pwani yulee....:wink2:
 
nijuavyo mimi ni kuwa mawaziri wetu wana wasaidizi, wasaidizi hawa ni wasomi tu, na moja ya kazi zao ni kuwa wanabeba na kutunza zile nyaraka za serikali zote ambazo waziri husafiri nazo. sasa inanipa mashaka mheshimiwa waziri wetu anakumbatiaje nyaraka za serikali chumbani kwake?
 
Wakuu nji hii ni zaidi ya tuijuavyo, baba Mwanaasha kazi anayo.:violin: :peep:
 
kwa hilo la pete nawapongeza wezi waliomuibia.ingawa nahofia usalama wao.maana yale mapete yanaonekana hayakuwa ya kawaida.yasije yakawatokea puani.mtoto wa pwani yulee....:wink2:

Haha wa pwani eeh! Hakuna chochote wala lolote, hayo watakuwa wameyatupilia mbali. Huenda ndiyo yaliyokuwa yanamtia kiburi wenziye wakayagundua wakayaiba ndiyo maana akapagawa na kuanza kusema ovyo. Alisahau yuko mji kasoro bahari.
 
Kighoma malima naye ni Waziri ? No wander wizara inakwenda kombo.chaguzi la wasahidizi wako ni kitu muhimu kwelikweli ambacho JK kilimshinda...wacha nchi uende jinsi inavyokwenda ... Tutakapodondoka tutajifunza vizuri tumezoea ku Learn the hard way.
 
mwenye habari kamili atujuze hapo kwenye SMG..,nadhani ingepewa uzito sana kwenye magazeti hapa nyumbani..Media zote ingekuwa habari kuu..
 
semekana alipatiwa rest house ya tanesco na huduma zote za kiwaziri akasepa...akaingia kitaa!!!!
 
ukiwa mwanasiasa TANZANIA NI RUKSA kufanya chochote!unaweza ukaua usifanywe chochote, unaweza kuiba mali za umma usiguswe.TANZANIA ZAIDI YA UIJUAVYO,
 
Na bado aliwashangaa wezi kwa kuacha kuiba bunuki ambazo according to matamshi yake ni MTAJI wa kumtoa mtu,sasa yeye alisafiri nazo kama silaha za kujilinda yeye au alikuwa anlida mtaji wake na aliofia kuziacha nyuma,hizo silaha sio bastola ya mtu kukaa nazo,alitakiwa azisalimishe polisi morogoro kwa ajili ya hifadhi,pia hiyo hoteli inabidi wachukuliwe hatua kwa kutokuwa na limit na security control,ina maana kwa vile ni waziri hata angeingia na mzinga kwenye chumba chake cha kulala wasingemzuia?
 
Ni analysis nzuri kwa ujumla wake. Vitu vyote hivyo vya nini kwa safari ya Morogoro tu? Huenda kompyuta moja ilikuwa ni kwa ajili ya internet (hasa hasa jamiiforums), nyingine kwa ajili ya games, nyingine mahesabu kwenye excel, na kadhalika na kadhalika!! Ahh, nchi hii bwana, watu wanakula matunda ya uhuru wa mwalimu Nyerere tu kwa raha zao!
 
Mimi binafsi nilishanga naibu waziri kusafikri na mivitu hiyo yooote, sijui alikuwa nanakaa morogoro kwa muda gani, manake mabegi 3 ya ngu si mchezo, huyo ni naibu waziri, Jiulize waziri Ngeleja akisafiri kwenda sengerema inakuwaje? Halafu mwanaume na mabegi matatu ya nguo, yanini yote hayo, sijui sophia simba akisafiri anenda na mabegi mangapi

Halafu Mwashangaa SMG? Kwake ana handaki la silaa huyo, mtoko huo wa Morogoro ndo aliamua atoke kiSMG, subirini akienda Arusha sasa.........AK 47 ndo atakayobeba
 
Huyu ndugu malima ujana,usharobaro, 'umjini' anao sana....hizo silaha, ukitafakari sana na tusimlaumu...jamaa aliwahi poteza baba ktk mazingira ya sintofahamu, so anaweza kuwa anaogopa kivuli au kuna hatari ya ukweli inamtishia...Aliwahi shambuliwa sana chenge kwa tabia ya kunawa nawa mikono kila asalimiwapo (wanajua kinachoendelea) ...leo tunaona jinsi (dr.kyembe) watu wanavyopakazwa sumu mikononi...HALI SI SHWARI NDANI YA SERIKALI YA TZ..haaminiki police wala mamamkwe hatari!..
 
Juzi jioni tukiwa eneo moja maarufu sana kwa starehe mjini Morogoro. Kaka mmoja ambaye pia anapenda sana kujirusha alitusimulia jinsi mheshimiwa Adam Kigoma Malima alivyofika pale Klabuni na kukaa meza moja na dada mmoja mrembo sana, mweupe mrefu aliye na nywele ndefu, kwa stahili ya tanzania unaweza kusema kwamba ana makalio makubwa. Huyu dada ni maarufu kwa shuguli za kujiuza kwa watu matajiri tu. Pia anamiliki pikipiki 3 za bodaboda na texi moja.

Mshikaji aliyetusimulia hakuwa na uhakika kama mh. Malima alikuwa anakunywa, lakini meza yao ilijaa vinywaji na nyama. Mnamo saa 8 usiku, mheshimiwa aliinuka na kuondoka na huyu mrembo huku wameshikana mikono. Walikoelekea hapakujulikana lakini ukweli ni kwamba waliondoka pamoja. Kinachowashangaza hawa vijana ni picha walizoziona mtandaoni; watu wengine tofauti wakituhumiwa kuwa wezi. Wanajiuliza ni kwanini yule dada hayumo? Mshikaji anaimani 100% kwamba mheshimiwa aliibiwa na changudoa. Hawa kwenye picha amekataa katakata kwamba hakuna hata moja aliyekuwa na mheshimiwa Malima club

IMG_7297.jpg
 
Back
Top Bottom