Tujikumbushe ya Adam Malima na ulimbukeni wa madaraka

Tujikumbushe ya Adam Malima na ulimbukeni wa madaraka

Siku moja alikuja na hapa Songea na watashi fulani wa madini kwenye ndege ya kukodi.Kindege kile kilijaa mabegi.Watumishi walipakua mabegi pale airport na gari tatu za madini zilikuja kubeba zile begi.Nilihisi ni za wale wazungu,kumbe sasa nashawishika kujua ni za Malima maana kama Moro tu anabeba beg tatu huku songea ilikuwa na mara mbili ya hizo.Huendsa huyu Basias alikuwepo kwenye msafara ule.
 
This is one arrogant slimy retard I f$$@ing hate him

You should be blaming the system we have or the person who appointed him to that post. We need to have a system whwich will give us capable leaders, and not those who use leadership to show themselves off.

Kuna watu ukiwateua katika nyadhifa fulani akili zao kwanza, nitakwenda nchi ile, nitakula chakula kile, nitachukua mwanamke yule, nitanunua simu mbili, nitembea na dola elfu 10 mfukoni.

Ukiangalia huwezi kuona element ya merit (labda ni appeasement policy) kwa Malima kuwa katika nafasi hiyo, na ukiangalia huwezi kuona ni nini anadeliver.

So inabidi tuwe na system ya kuwafanya wateuaji wateue kutokana na merit na sio know who.

Lakini kinachosikitisha zaidi ni kuwa, pamoja na uchafu huo hakuna kitakachotokea hatachukuliwa hatua yoyote ya kinidhamu. This is Tanzania.
 
Kwa hali ya sasa ambapo vigezo vya kuteuliwa kwenye wadhifa wowote ni kuwa mwanamtandao, hakuna uwezekano wa kumpata kiongozi mwenye "merit". Hivyo Malima, kama mwanamtandao, hawezi kuwa mwadilifu. Isitoshe yeye ni Naibu Waziri kwenye Wizara ya Madini na Nishati. Kuvaa pete ya almasi yenye thamani ya mamilioni ni ishara kuwa madini aliyo nayo kupitia uwekezaji haramu kwenye madini yanamwezesha kupata silaha za kulinda madini yake na kujilinda mwenyewe ili pete na cheni za thamani ziwe salama. Masaanduku matatu ya nguo kwa mwanaume na kwa safari fupi si jambo la kawaida. Huenda masanduku hayo yalijaa madini na alikuwa na mpango wa kukutana na wateja wake. Ndiyo Mungu akamuumbua. Kajirusha na kimwana nacho kikajisavia. Bravo kimwana. Ungepata wapi utajiri huo? Hiyo ndiyo seerikali ya JK!
 
Kama namuona pale ambapo angewafuma wezi wake! Kushoto bastola kulia SMG! Rambo na Shwazniga nyuma!
 
Hivi ni kwa nini wengi wa wanaoitwa viongozi ni watu wa hovyo hovyo tu? Hebu naomba niulize: Hawa watu walikuwa ni wa hovyo hata KABLA hawajachaghuliwa au kuteuliwa, au walianza kuwa wa hovyo mara BAADa ya kuchaguliwa/kuteuliwa? naomba mwenye uelewa mpana juu ya watu kama vile ben, JK, kayanza, ngeleja, wassira, chikawe, sophia, mponda, nkya, kawambwa, chenge, mwanyika mahita, mboma, mwema, feleshi, mwang'onda, manumba, mkama, makamba, tendwa, chande's, nk atujuze.
 
Mujwahuzia:
Mh.Malima ameshindwa kutwambia ukweli Wtz juu ya kuibiwa kwake wakati akiwa ziarani Mkoani Morogoro alikuwa anafanya nini wakati huo inakuwaje kiongozi kama yeye akiwa na vitu nyeti vya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tz zikiwemo siraha mpaka Pete fikiria kiongozi anaibiwa hadi pete makubwa haya malima Usione aibu kwa familia yako na wtz twambie ukweli kama ulikuwa unavinjari na Kiwana maana hiyo ni Moro kasoro Bahari ni usingizi gani huo???? ni wa samaki pono?????? je wewe ni mlinzi gani unaibiwa ukiwa na siraha kama ulienda kustarehe Small House ukapagaishwa na kussahau majukumu unastahili adhabu kali kwa maaana umeenda kinyume na maadili ya viongozi.
 
SUALA la kuibiwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima, si la mchezo hata kidogo kama kweli tunataka kuheshimu utawala wa sheria na maadili kwa mtumishi wa umma kama yeye, tena mwanasiasa.

Sasa, kwa mujibu wa vyombo vya habari, vikimnukuu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, hebu tuangalie alichoibiwa waziri huyo:

1.Laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya sh milioni 5.6.
Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni sh milioni moja.

2.Simu tatu, ya kwanza Nokia C6 ya sh 500,000, Nokia E200 ya sh 250,000 na Blackberry yenye thamani ya sh milioni 5.5.

3Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya sh milioni 2.5.

4Dola za Marekani 4,000 ambazo ni sawa na sh milioni 6.5.

5.Fedha taslimu sh milioni 1.5.

6.Kadi mbili za benki.

7.Mabegi matatu ya nguo.

8.Baraghashia mbili zenye thamani ya sh 50,000.

9.Nyaraka mbalimbali za serikali.

Pia awali ilitajwa na vitu hivi:

Pasipoti mbili za kusafiria (zimeokotwa jalalani karibu na hoteli).
Lakini bahati yake hakuibiwa silaha hizi, Bastola moja na bunduki iliyotajwa bila aibu kuwa ni SMG (Sub-Machine Gun).

UCHAMBUZI RAHISI

Kuna element ya excessiveness kwenye orodha ya vitu hivi. Kwa maoni yangu huu ni ulimbukeni kama wa hadithi ya zuzu aliyeshinda bahati nasibu akaamua kununua kila kitu mtaani kwake, hadi kituo cha basi.

Waziri kwa mishahara yetu ni mtu maskini labda kama ni mwizi.

Ndiyo, yeye ni mbunge mwenye maposho, lakini bado alipataje mali zote hizi?

Katika hali ya kawaida, mwanasiasa anasafiri na laptop tatu za nini?
Huu ni ulimbukeni wa kujua kompyuta na kuweza kuzipata kirahisi au kupewa hovyo hovyo tu; vinginevyo nini kinaweza kuwa sababu?

Vinasa sauti, je, yeye amekuwa mwandishi wa habari au mpelelezi anayetafuta ushahidi wa sauti? Nini hasa?

Simu tatu, bahati mbaya ni utamaduni wa hapa nchini Tanzania lakini pia sijawahi kusikia Blackberry ya gharama zote hizi karibu zaidi ya dola 3,400 za Marekani.
Hiki ni kioja na ushamba mwingine. Ina nini hiyo simu? Inavaa chupi?

Pete mbili ni sawa lakini bado alipoongea na waandishi alikuwa amevaa mapete mengine. Sasa yote ya nini?
Dola za Marekani zote hizo kwa safari ya vijijini ni za nini? Au alizitoa huko huko?
Fedha za Tanzania nadhani ni sawa maana yake alihitaji kulipia gharama kadhaa.

Pia, kadi mbili za benki ni sawa na hata mabegi matatu ya nguo si ajabu, kama alikuwa na safari ndefu na hata baraghashia mbili si tatizo.
Nyaraka za serikali, hii ni fedheha kubwa kwa kuwa kama naibu waziri alipaswa kujua jinsi ya kutunza nyaraka za serikali mara aingiapo hotelini au popote pale. Huwezi kuziweka nyaraka nyeti hovyo hovyo tu.
Pasipoti mbili zote za nini? Alihitaji kwenda nazo Morogoro za nini?

Huenda moja ni ya kidiplomasia na nyingine ya utumishi serikalini ama ya kiraia, lakini za nini zote hizo?

Kwenye silaha hapa ni suala la uhalifu kwa mujibu wa sheria zetu labda kama kuna maelezo mengine.
SMG ni silaha ya kivita, labda kama yeye na polisi wa Morogoro wanamaanisha kitu kingine kwa kutumia maneno "SMG".

Huu ni uvunjaji wa sheria na wala hakuna haja ya kujiuliza kwamba anaogopa nini au analinda nini, mbona ameshindwa kulinda mali alizoibiwa?

Ingeibiwa angekuwa amewaweka raia wengi sana na hata polisi hataraini. Nashangaa wale waandishi hawakuuliza mapema ili tupate maelezo. SMG?

Hii ninayoita element ya excessiveness ni ulimbukeni wa kiafrika haswa kwamba sasa una madaraka, kwa hiyo unataka kila kitu kijazane kwako tu kwa kuwa hela zipo na "haki" ipo hata kama haikubaliani na sheria zetu.

Mavitu, makompyuta, mahela, masilaha, mavinasa sauti, mapete, madude mengi tu - Swali ni je, kuna busara hapo? Kuna utu-uzima hapo? Hii ni sifa nzuri ya kiongozi kweli kujijazia mavitu hovyo hovyo tu na kuishiwa kuibiwa kirahisi namna hii bila haya?

Lakini kutokana na utamaduni wetu wa kulindana unaojengeka siku hizi, huyu hataguswa.

Hii ni aibu kubwa mno kwa taifa letu na yeyote anayetetea mambo kama haya, hana nia njema na taifa hili. Pana tatizo hapa, ni zaidi ya kuibiwa naibu waziri fulani.


Chanzo Tanzania Daima Jumatano machi 14, 2012
email_open_log_pic.php

Ukifatilia mambo mengine lazima uwe chizi.
 
falaaaaa huyo wazir!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
Siku moja alikuja na hapa Songea na watashi fulani wa madini kwenye ndege ya kukodi.Kindege kile kilijaa mabegi.Watumishi walipakua mabegi pale airport na gari tatu za madini zilikuja kubeba zile begi.Nilihisi ni za wale wazungu,kumbe sasa nashawishika kujua ni za Malima maana kama Moro tu anabeba beg tatu huku songea ilikuwa na mara mbili ya hizo.Huendsa huyu Basias alikuwepo kwenye msafara ule.

Hadithi za Sinbad Wa Baghdad!
 
inanikubusha waziri fulani aliyekimbia na nyaraka za serikali uingereza ili jamaa wakazisaini huko huko ugaibuni. isijekuwa nyaraka hizo za serikali alizobeba malima ni mikataba waliyosainiana na wawekezaji kuchimba rubi huko matombo.
 
Back
Top Bottom