Tujikumbushe vijiji vya Ujamaa 1972

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
51,670
68,631
Umofia kwenu wana JF,

Miaka ya 1972 Mwalimu alianzisha vijiji vya ujamaa katika mikoa yote ya Tanzania,kwa upande wa Mzizima (DSM) kulikuwa na vijiji vya Kibugumo,Kimbiji,Mwanaliwato na Gezaulole.

Lengo lilikuwa vijana waachane na biashara za umachinga,uchuuzi kuuza njugu na korosho kwenye nylon na kujikita kwenye kilimo cha pamoja chenye tija.

Serikali ya CCM imejaribu kuiga baadhi ya fikra lakini wanadondokea pua,kuanzia kilimo kwanza mpaka big result now hakuna kitu.Tuanzisheni vijiji vya ujamaa ili kukuza uchumi wetu na kuwaondoa vijana mijini na biashara za uchuuzi na kuwapeleka vijijini huko na kulima kitaalamu,kwa sasa tuna wasomi wengi na zana za kutosha katika ulimaji wa kisasa tofauti na miaka hiyo ya 72',Tanzania karibu 70% ya ardhi haijawahi kuguswa kabisa.
 
Isome vizuri historia ya ujamaa Tanzania. Vijiji vya ujamaa havikuwepo kila mahali. Nenda Kilimanjaro, Kagera na Mbeya kama utakuta historia ya vijiji vya ujamaa. Hakuna. Ujamaa ulikuwa ni kwa baadhi ya sehemu tu.
 
Oscar Kambona alipinga wazi wazi vijiji vya ujamaa na kumshauri Mwl.Nyerere wachukue vijiji vichache vya mfano kama mambo yataenda vizuri basi na watu wa maeneo mengine watahamasika na kuanzisha vijiji vya ujamaa katika maeneo yao.
Kambona hakufanikiwa katika jambo hilo kwani katika majadiliano makali katika mkutano kwa upande mmoja Mwl.Nyerere na upande wa pili Oscar Kambona walibishana sana na mara nyingine walitoka pembeni kwa ajili ya majadiliano ya faragha na hatimaye kurejea katika mkutano.

Maeneo ya kusini ambako Rashid Mfaume Kawawa amnbaye alifahamika pia kama simba wa vita hatosahaulika kwa kitendo chake cha kutekeleza maagizo ya Mwl.Nyerere bila kuhoji wala kutumia busara. Alitumia nguvu kubwa kulazimisha wakazi wa vijiji vya Songea kutoka katika makazi yao na kuwapeleka maporini kuanzisha vijiji vya ujamaa. Wengi wao walikufa kwa maralia, kuliwa na wanyama wakali chui, simba ndio maana labda a.k.a ya "simba wa vita" itabeba umana kama litakumbukwa hilo pia.

Vijiji vya ujamaa havikupatikana kwa maridhiano bali uwezo wa madaraka ya Mwl.Nyerere, ilikuwa miak ya 1960's na amri amri zilianzia katika Kufuta Vyama vya Upinzani mkakati ambao ulimwondoa Chief Abdallah Fukindira wa III aliyekuwa waziri wa kwanza mara baada ya uhuru katiza wizara ya sheria na katiba. Baadae muungano, ujamaa.

Vijiji vya ujamaa havitufai tena kuvirejea gharama yake kubwa sana, na sawa na kuukaribisha umasikini
 
Bola we kaka emetueli misha kwamaana viongozi wetu wa wamekalia fedha wanatusomea makaratasi.
 
Umofia kwenu wana JF,

Miaka ya 1972 Mwalimu alianzisha vijiji vya ujamaa katika mikoa yote ya Tanzania,kwa upande wa Mzizima (DSM) kulikuwa na vijiji vya Kibugumo,Kimbiji,Mwanaliwato na Gezaulole.

Lengo lilikuwa vijana waachane na biashara za umachinga,uchuuzi kuuza njugu na korosho kwenye nylon na kujikita kwenye kilimo cha pamoja chenye tija.

Serikali ya CCM imejaribu kuiga baadhi ya fikra lakini wanadondokea pua,kuanzia kilimo kwanza mpaka big result now hakuna kitu.Tuanzisheni vijiji vya ujamaa ili kukuza uchumi wetu na kuwaondoa vijana mijini na biashara za uchuuzi na kuwapeleka vijijini huko na kulima kitaalamu,kwa sasa tuna wasomi wengi na zana za kutosha katika ulimaji wa kisasa tofauti na miaka hiyo ya 72',Tanzania karibu 70% ya ardhi haijawahi kuguswa kabisa.

ujamaa ni njia pekee ya kuwaondolea umasikini jamii yenye wakulima zaidi ya 50% bado tunauhitaji.
aluta continua
 
Kwa uanzishaji wa vitu hodari lakini usimamizi sifuri. Hata baada ya kuingia ujamaa nchini ambao ulipelekea watu wengi waliokuwa wanamiliki mali walizozipata kihalali na kiharamu walizipoteza kwa kile kilichoitwa UTAIFISHAJI. Mfano Livinstone Hotel iliyokuwa inamilikiwa na Ghikas ikawa ya serikali na kuitwa MOSHI HOTEL na utendaji wake ukashuka.
UTAIFISHAJI uliendelea hadi kwenye mashamba ya mkonge ambayo yalikuwa yanamilikiwa na wazungu ambao kwa wakati huo waliamua kuwa kuwa Watanganyika yakakabidhiwa UMMA, uzalishaji wa katani kipindi cha wazungu tani 220,000 zikashuka hadi 12,000 mara baada ya kutaifishwa.

Pamoja na kuwa na ujamaa ulioenda sambamba na Azimio la Arusha bado mambo yalienda kombo kimaadili kwa viongozi wa TANU na baadae CCM. Pamoja na Hayati Edward Moringe Sokoine kujitahidi walau nchi iendane na Azimio la Arusha na Ujamaa ulioletwa na Mwalimu Nyerere bado alihujumiwa na viongozi wenzake kiasi cha kuonekane peke yake katika kurekebisha na hatimaye alikufa kwa ajali ya utata, na kuacha viongozi waliobaki na Mwl.Nyerere huru kula matunda ya UHURU.
 
kambona alikimbia Tanzania mwaka gani na vijiji vya ujamaa vilianzishwa lini?
 
Back
Top Bottom