BLACK MOVEMENT
JF-Expert Member
- Mar 11, 2020
- 2,704
- 6,499
Ukiangalia trend za Kilimo Chetu ni kama kinashuka badala ya kupanda, kwa sababanu kuna baadhi ya takwimu ambako Tanzania zamani ilikuwa inaongoza kwa chai au Pamba ila leo hii hakuna Tena.
Umewahi fika Kilimanjaro siku za hivi karibuni? Vijijini hasa kwenye mashamba ya kahawa? Wanaolima ni wazeee sana na hao hata ndo unakuta wanakimbizana na KNCU chama cha chao cha Ushirika, Hakuna kijana mwenye shamba la kahawa, ni wazee na wengi wao kwa sababu nguvu zimepungua wameamua kutelekeza kahawa au wanalima kiasi fulani.
Nenda Meru kule Aruaha hali ni hiyo hiyo Wazeee ndio wanaolima kahawa na wamechoka wameamua hata kuuza mashamba na watu kujenga nyumba za kuishi au Mahoteli au Mashule. Nenda Bukoba kwenye kahawa wamebakia wazee.
Ukienda Mkoa wa Shinyanga kwenye Pamba, utaona kabisa uzalishaji unapungua sana, Kilimo cha Pamba Mikoa ya kanda ya Ziwa sio kama zamani ukiachana na mambo ya bei hata nguvu kazi ni Changamoto sana vijana wako Jiji la mwanza wanafanya Umachinga.
Nimewahi fanya kazi na Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula WFP kwenye mkoa wa Kigoma na Vikundi vyote vya wakulima sikuona kijana hata mmoja ni wazee tupu wa mama kwa Wababa. Vijana wamekimbilia miji kama Kahama, au miji yao kama Kasulu mjini na Kibondo mjini na kule wanafanya umachinga na kuendesha Pikipiki.
Ukiangalia Kanda ya Kaskazini, Vijana waliokuwa wakulima kule Singida kwenye alizeti sasa wako Arusha, wako Dar au wako Singida Mjini. Hali ni hivyo hivyo Morogoro, Tanga, Mbeya, Iringa, Songea na kwingineko.
Siku hizi ni kazi ngumu kupata vijana wa kukufanyia kazi shambani kwa sababu asilimia kubwa hawapo kabisa wamekimbili Mijini, waliobakia ni Wazee au vijana ambao ni addictade na pombe.
Serikali inapaswa kuja na mikakati thabiti sana kusaidia kupunguza hii hali.
Ushauri wangu kwa Serikali;
1. Serikali iweke ugumu sana wa vijana kufanya uchuuzi mijini, yaani mazingra ya kuwa Mchuuzi mjini yawe magumu sana na yasivutie kabisa vijana, Awamu ya 5 vijana walivutiwa sana na mazingira na kipindi hicho ndio mamia kwa maelfu ya Vijana walikimbilia Mijini kufanya uchuuzi na kuacha wazee wakilima.
Mazingira ya uchuuzi yanavuta sana vijana na hapo ndio Serikali inapokosea kabisa, the more unavyowavuta mjini ndio the more kilimo kina-lose.
2. Wazee ambao kwa sasa kweli ndo wazalishaji kule vijijini wasaidiwe basi, iangaliwe namna ya kuwasaidia wale wazee wanaokoa sana Taifa kwa Chakula lakini wanahitaji Sapoti ya kuwafuta Jasho, Fikiria mzee analima halafu ukame unapita unaangamiza kila kitu, hapo ndo kijana anaamua kukimbilia mijini make anaona hailipi. Linapokuja suala la kusapoti Wakulima Wazee wapewe kipaumbele hawa ndo wanaookoa kwa sasa.
3.Bila Motisha kwenye Kilimo vijana wataendelea kukimbia vijijini, Kilimo kinahitaji motisha sana, Moja ya sababu ya vijana kukimbia ni kwa sababu wanaona hakilipi na wako sahihi kabisa, Kilimo kinahitaji upendeleo special kwa kila nyanja, Upendeleo wa Serikali kwenye Kilimo unaweza wavutia sana Vijana kubakia kwenye Kilimo.
Kwa sasa Motisha ziko tu kwenye makaratasi hakuna uhalisia wala jitihada
- Kuwe na motisha special kwa vijana wao lima hasa vijijini.
4. Maeneo ya Kilimo pia ni bora yakawekewa mazingira kidogo yafanane na Mijini, ingawa kidogo kwenye Umeme wanajitahidi sana, pia huduma za kijamii jama Maji, Afya na kadhalika, Kunapo kuwa na huduma bora vijijini angalau inapunguza asilimia kiasi ya vijana wanaokimbilia mjini.
Serikali iweke mazingira magumu mjini na wakati huo huo mazingira rafiki ya kuendesha kilimo vijijini, na kwa wale vijana wa Vijijini ambao wamekubali kubakia na kulima wale wasaidiwe sana ili wawavutie wenzao waingie kwenye kilimo pia. Hatuwezi kuwa Taifa la uchuuzi pekee, tunahitaji sana kuzalisha mazao ya chakula na ya Biashara, lakini hii haitawezekana bila hatua kubwa.
Kanda ya Ziwa Jiji la Mwanza limemeza nguvu kazi yote ya ile kanda ukangalia Kaskazini ni Arusha imemeza wote, Dar imemeza nchi nzima.
Ukiangalia baadhi ya maeneo tayari hali ishakuwa mbaya, kama Moshi kwenye kahawa, Arusha kahawa na Ngano kama kule Karatu, Bukoba kahawa, Kanda ya ziwa pamba.
Na sisi wasomi tuache kubanana mijini twende tukawekeze kwenye kilimo huko vijijini kuokoa jahazi labda vijana watatuiga na wao watulie.
Serikali weka mazingira magumu sana mijini, Sheria kali za mambo ya Mipango miji, Usafi wa miji na ufanyaji biashara holela.
Nakaribisha michango.