Tujikumbushe: Safari za wabunge kwenda Dodoma bungeni

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Wabunge wakipanda basi kuelekea bungeni Dodoma. Hii ilikuwa kabla ya mashangingi.

1269761.jpg
 
Hii ukipatikana uongozi wenye uanaume haishindikani kabisa; weka amri na utaratibu tu wenyewe wananyooka.
 
Usitukumbushe enzi hizo, hata sabuni za kukogea ilikuwa hamna.
 
hii ukipatikana uongozi wenye uanaume haishindikani kabisa; weka amri na utaratibu tu wenyewe wananyooka.

na wakifika huko walale kwenye ile hostel yao waliyojengewaga! Yaani ****** wa posho kwisha, mafuta na ma pa diem ya madereva kwisha! .tungekuwa mbali vibayaa
 
Wenzetu wanaotupa misaada kama Denmark hata PM wao anatumia baiskeli!!

Huu mfumo wa sasa ni wizi tu ulioandaliwa toka enzi za Mzee Ruksa!
 
Wenzetu wanaotupa misaada kama Denmark hata PM wao anatumia baiskeli!!

Huu mfumo wa sasa ni wizi tu ulioandaliwa toka enzi za Mzee Ruksa!

Hapa tutaambiwa jua kali kutumia baiskeli.
 
Lakini dhahabu yetu ilikuwa salama, leo unauza dhahabu unapewa sabuni, nimeamini machifu Mangungo bado wapo.
Siku hizi kuna mabasi maridadi sana. wangeyatumia hayo huku tukipata pesa za dhahabu na almasi kama inavyotakikana tungeweza hata kupandisha chombo cha utafiti angani.
 
Wenzetu wanaotupa misaada kama Denmark hata PM wao anatumia baiskeli!!

Huu mfumo wa sasa ni wizi tu ulioandaliwa toka enzi za Mzee Ruksa!
Hivi kwa nini wasituwekee masharti magumu? Mimi huwa wakati mwingine siwaelewi hawa wahisani wanaona kabisa kuna mismanagement lakini wanatupa misaada bila kutuwekea masharti magumu. Wana yao hao wengi wao wanajivunia mimali asili yetu kwa kubadilishana na tumisaada twao.
 
Back
Top Bottom