Tujikumbushe MV Bukoba enzi za uhai wake

Kiukweli ile ajali ni ya kihistoria. Inatisha mno! Mkoa wa Kagera karibia kila mtu alifiwa ...kama si ndugu kuna mtu unamfahamu! Teknolojia mbovu ilitutia hasara kubwa sana. Meli ilizama pole pole hadi inapotea hakuna anayejua la kufanya! Afadhali hata "magenius" waliofikiria kuitoboa ili kuokoa watu ingawa ndio iliongeza kasi ya meli kuzama ikiwa na watu zaidi ya mia nane! Dah!
Mkuu nisaidie kidogo hivi walitaka kutoboa kuokoa watu kivip kwamba ilipinduka au ilikuaje mpaka watoboe maana hiyo kutoboa napata picha kama watu walifungiwa sehem au ni vipi
 
Inauma sana lakini kama vile waliokabidhiwa dhamana kuna kitu bado nakishangaa, kipindi MV Victory ikiwa haija simama yalikuwa na majira ya sikukuu za krisimas na mwaka mpya, nilibahatika kufika kwenye maeneo ya bandari ya Bukoba nilishangaa sana kuona umati mkubwa sana wa watu wamejaa wanasubiria kupanda chomboni, huku Meli ilibeba mizigo mingi sana binafsi nilihisi meli ilijaa sana na kupitiliza lakini binadamu hatujali ikitokea ajali ndo tujitia unabii. Kwakweli msiba wa MV BUKOBA ni ngumu sana kusahaulika ukijumuisha na msiba ule wa Spice..ya Zanzibara
 
Wakati ilikuwa hiv
9dd77946cc154f56bd09416a8abaa2e0.jpg
ohooo. poleni sana
 
Ivi naomba niulizew, kwani maboya hayana mchango wowote mbn sioni mtu aliepona coz ya maboya
Dah, kwa kweli maboya Yale ni kwa ajili ya uokozi ila jinsi yalivyofungwa kwa ustadi hata namna ya kuyafungua kwa haraka huwa ni ngumu sana sana, sasa utaona ww uendelee kunywa maji huku unafungua boya au ukimbie. Maana wakati huo pumzi inakuwa inayoyoma kama sio kuisha kabisa. so Yale maboya nadhani yangewekwa kila mahali na sio upande mmoja kama ambavyo huwa nayaona kwenye kigongo ferry
 
Back
Top Bottom