Tujikumbushe Mashairi tuliyoyapenda shule ya msingi

ChizzoDrama

JF-Expert Member
Sep 29, 2019
1,317
1,229
Wanangu Wa faida mpo?
.
Kuna vitu vinafanya wakati Fulani mtu mzima utamani kurudi utotoni
Ingawa ni ngumu ki nadharia (mawazo) yanaweza kukurudisha na ukajikuta Una tabasamu peke yako njiani
.
Nakumbuka moja ya vitu vilivyo ni Fanya niipende shule ili kuwa ni pamoja na kukaa makundi na kusoma hadithi mbalimbali na baadae kuulizana maswali ya hadithi husika.
.
Lakini pia ile Mwalimu anakuja ghafla darasani kisha anamchagua mwanafunzi yeyote aimbe shairi na akikosea basi viboko vinamiminwa

Basi ikawa kila unaporudi home unakariri haswa mashairi ili kesho na wewe uonekane konki
Mashairi yalikua murua Sana na haya ni mfano tu

"BABA NA MAMA SALAMU
nyumbani nawatumia
Siwezi kupiga simu
Niko Mbali na dunia
Bila Shaka mwafahamu
Jela Nina tumikia
Sina Wa kumlaumu niliyataka mwenyewe"

"NIKIMALIZA KUSOMA
Nitafanya kazi gani
Nipende kuwa rubani
Kazi nzuri ya heshima
Nirushe ndege angani
Inifikishe salama
Nikimaliza kusoma nitafanya kazi gani"



"CHITEMO MIMI MASIKINI
uvivu wangu nyumbani
Nikiwa huru njiani nakufa
Nakufa hapa kwanini
Sadiki sasa hashiba
Chakula kingi kwa baba
Nirudi tena kwa baba nakufa hapa kwanini"

Ebwana tupia nawewe shairi lako pendwa tujikumbushe zile nyakati za dhahabu kabisa
 
Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia
hadithi uliyongoja leo ninakuletea
Alitoka siku moja njaa aliposikia
njaa aliposikia sungura nakuambia

Siku hiyo akaenda porini kutembelea
akayaona matunda mtini yameenea
sungura akayapenda mtini akasogea
Mtini akasogea sungura nakuambia

sungura karuka ruka lakini hakufikia
matunda hakuyashika mikononi hakutia
hakika alisumbuka nguvuze zikapungua......
 
Karudi baba mmoja, natoa beti mbili nnazozikubali

6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli
Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata Mali
Haya Sasa buriani, na kifo kimewasili
Kama mnataka Mali, mtaipata shambani

12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali
Pale kwenye shamba lao, wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli
Kama mnataka Mali, mtaipata shambani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom