Tujikumbushe mambo Enzi za Mwalimu

Kumbe hatujaanza siku hizi serikali kutumia magari ya 'kifahari'! 109 enzi hizo lilikuwa kama V8 tu...

Acha utani bwana.......hilo lina bawaba kabisa milangoni litakuwaje sawa na V8 na halina hata AC.......NILICHUKIKUBALI HAPO NI YEYE KUTUMIA GARI LA MKUU WA WILAYA..........siku hizi mkuu akienda mafia shurti ile Merc S500 ibebwe nayo kwa ndege
 
 
Mwalimu akiwa kazini na watendaji wengine kuleta maendeleo ya Taifa
Uzalendo wake haupimiki..........................................
Mwalimu alipong'atuka Tanzania ilikuwa imepiga chini maendeleo au ilikuwa imepiga hatua kimaendeleo?
Kweli Mwalimu alikuwa mzalendo lakini aliiacha nchi ikiwa katika ufukara na foleni refu. Au ndio uzalendo na maendeleo yenyewe tuliyopata chini ya mwalimu?

Mwalimu aliamua kung'atuka baada ya fikra sahihi za mwenyekiti kugonga ukuta. Kosa la mwalimu aliongoza serikali kutokana na haiba ya mtu mmoja badala ya kujenga taasisi/ mfumo wa kitaasisi. Hili kosa bado linaendelea na hivyo hakuna chombo cha kumwajibisha mtendaji anapoboronga mambo.

Tuna safari ndefu kama Taifa. Hivi bado nchi yetu inafata sera ya ujamaa na kujitegemea?
 

Hizo ni fikra zako, na ni upo sahihi kuwaza ufikiriavyo na uhuru wa mawazo...............
 
Hizo ni fikra zako, na ni upo sahihi kuwaza ufikiriavyo na uhuru wa mawazo...............
Fikra zako wewe zikoje? Tumia uhuru wako wa mawazo, jieleze tufaidike na mchango wako.
 
Fikra zako wewe zikoje? Tumia uhuru wako wa mawazo, jieleze tufaidike na mchango wako.

Ziko tofauti na wewe, zangu zipo more +Ve kumuunga mkono Mwalimu Julius Kambarage Nyerere...........
 
Reactions: BAK
Kumbe magari ya kifisadi yalianza enzi za mwalimu? sikulijua hili! maana hili enzi hizo lilikuwa kama lile la Mh Zitto Kabwe linalowatoa roho watu ! kumbe kibabu hakina tofauti na mafisadi wa sasa anhe?!
 
enzi hizo '109' haikuwa gari ya kifahari. Jaribu ku-google uone gari za kifahari 1970s : Chrysler Imperial, Lincoln Continental (kama hii aliitumia Kwame Nkrumah), Buick Riviera, Cadillac Eldorado, Lincoln Mark V, Audi Coupe, Lamborghini Jalpa, na nyingine nyingi

Kumbe hatujaanza siku hizi serikali kutumia magari ya 'kifahari'! 109 enzi hizo lilikuwa kama V8 tu...
 

We unazungumzia gari za kifahari Marekani, mimi nazungumzia Tanzania! Sababu hata sasa V8 si gari ya kifahari Marekani wakati kwetu ni...na Chrysler, Lincoln, Cadillac, Lamborghini bado ni gari za kifahari Marekani. Obama anatembelea Cadillac...definition ya 'ufahari' sio absolute, ina element ya context...na context ya Marekani na Tanzania ni tofauti!
 
zee wangu alikuwa nalo tena version ya nyuma ya hilo liliuwa na accelerator ya mkono, we acha akamuachia dingi mdogo basi kuna kipindi indicator zilikufa zote basi dingi mdogo akitaka kukata kona anatoa mkono nje anaonesha ishara ya indicator kwamba tunakata kona kulia au kushoto, basi mie na bro wangu hatuna mbavu . hiyo ndo ilkuwa Tanzania bana!!!
 
Ufukara gani unauongelea mkuu, wa akili au rasilimali asilia?
 
LET US OPT FOR 'Duet' this well paid politicians dont add anything 2 our economy rather than surbotage in various scandals! even Vitz to them is a big favour!
 
Kumbe hatujaanza siku hizi serikali kutumia magari ya 'kifahari'! 109 enzi hizo lilikuwa kama V8 tu...

Hapana mkuu! hata kipindi hicho kulikuwa na magari ya kifahari na yagharama hivyo kama huyu mzee angekuwa na tamaa basi angekua akitembelea gari kama au zaidi ya lile ya JONH KENNEDY na N.K! acha mambo yako wewe mkuu wetu wa sasa ivi apande gari la mkuu wa wilaya? hata kama ni hummer au vorgue hapandi ng'o! lakini mzee wetu wa enzi zile wala alikuwa hana hizo!usimfananishe kabisa nyerere na hawa jamaa wa sasa usije ukapata lana bure mkuu.
 
Acha utani bwana.......hilo lina bawaba kabisa milangoni litakuwaje sawa na V8 na halina hata AC.......NILICHUKIKUBALI HAPO NI YEYE KUTUMIA GARI LA MKUU WA WILAYA..........siku hizi mkuu akienda mafia shurti ile Merc S500 ibebwe nayo kwa ndege

hapo umesema mkuu! ile dhana ya kutoka kituo chako cha kazi kwenda kituo kingine na kutumia usafiri unaoukuta huko imekwisha kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…