Matema beach, tawaqal, embakassy, safina,
Kiswele, widambe dar mbeya 90s
Matema beach, tawaqal, embakassy, safina,
The Big Mayai - Dar to Dom
Naona kuna mchanganyiko wa mabasi kati ya 80s na 90s, na kidogo late 70s. Katika miaka ya 70-80s KAMATA na Relwe ndio walitawaala katika kusafirisha abiria, aidha waliweza kuwa na huduma za luxury, Express na Ordinary.
Kwa mfano, KAMATA walikuwa na watoa mabasi mawili kila siku toka Arusha kwenda Dar. Moja likiondoka saa kumi jioni (ordinary) na lingine likiondoka saa mbili usiku(luxury). Hili la kuondoka usiku ndio liliokuwa likiwahi kufika Dar, kati ya saa moja asubuhi au saa mbili.
Baada ya kuanza kuingia kwa mabasi mengine Arusha ilishuhudia kuongezeka kwa mabasi ya Luxury kama vile Imam na Rafiki ambayo nayo yalikuwa yakitoka saa mbili usiku na kuwahi kuingia Dar mapema asubuhi, huku yakiyapita mabasi ordinary ya saa kumi kama vile Bon City, Ngorika, Masama Cliff na mengine kadha wa kadhaaa...
Kwa iringa kulikuwa na Embakasy Nyuma iliandikwa ' Che wililye che Chako"
Enzi hizo ulishawahi kupita na basi hapa? Ilikuwa ukifika hapa ni kasheshe au faraja.
Kwa wale waliozaliwa au kuwepo Dar miaka ya 80s watakumbuka usafiri wa UDA kwa kutumia mabasi ya Ikarus 'kumbakumba'.
Mimi nilikuwa napenda kukaa pale kwenye maungio kwa kweli nimekumbuka mbali sana enzi hizo mji msafi,watu wastaarabu kila kitu kiko kwenye mpangilio na wanafunzi hawanyanyaswi, DART wanataka kuleta mabasi aina hii, ya kisasa zaidi.
Kwa wale waliokuwepo hebu tupeni experience yenu.
Teh teh sijui inaandikwaje kwa lugha yake ila mie nakumbuka tulikuwa tunaita HEKALUS.
...shie wagosi SIMBA MTOTO tumetoka nayo mbali sana, 80's I think.
No challenge. Champion. Bazuu. Lang'ata. Imam. Ngorika. Rombo safaris. Rombo mwelekeo. Rombo investment. Air chalinze. Shabaa. Ttbs. Tahfif. Tawfiq. Bembea mtoto. Kwacha transport. Atlanta. Atlas. Hood limited.