Tujikumbushe kwanini Bunge la Marekani lilikataa uwepo wa television ya taifa

Mkuu I stand To be Corrected ila Kuna kituo kinaitwa PBS ni US government funded Station. Ni Mali ya Serikali ya US.

Juzi tu Bibi Pelosi na Democrats walipitisha muswada kwenye congress kuidhinisha PBS ipewe funds na American Government kama kuiinua mgongo kwenye kipindi Hiki Cha Corona.
Maandiko yanasema, hakuna lililo jipya chini ya jua. Nimegundua moja ya jambo linalofanya tushindwe kung'amua, kuyaelewa na hatimaye kuyapatia ufumbuzi matatizo yetu mengi ni kuwa tunadhani matatizo yetu ni mapya. Kwamba, tunadhani hayajawahi kutokea sehemu nyingine. Matokeo yake tunashindwa kuyatafutia ufumbuzi ulio makini na unaodumu.

Nimekumbuka jambo ambalo niliwahi kulisoma sehemu moja. Wakati Marekani inapambana kutoka katika anguko la uchumi miaka ya 1930, yaani depression, taasisi moja inayohusiana na mambo ya kilimo katika serikali ya Marekani ilitengeneza makala fulani ya television, yaani documentary, iliyoitwa 'The River' ikielezea mafanikio ya Mamlaka ya Bonde la Tennessee (Tennessee Valley Authority)

Makala hiyo ilionyesha mafanikio mbalimbali yaliyoletwa na mamlaka hiyo, ikiwemo jinsi ilivyosaidia kukabiliana na matatizo ya mafuriko, kupungua kwa mazao ya kilimo na pia kuongeza uzalishaji wa umeme.

Sitaenda sana kwenye mambo ya kiufundi yaliyotumika kutengeneza makala hii ila itoshe kusema kuwa ile makala iliwavutia wengi, hadi Rais wa Marekani wakati huo, Franklin Roosevelt aliiona akaipenda hadi akatoa msukumo wa kuanzishwa kwa taasisi ya kiserikali ya utengenezaji wa filamu, U.S Film Service, ili waanze kutengeneza filamu nyingi za aina hiyo.

Lakini ile filamu ilikuwa na elements fulani za propaganda na wengi waliona siyo sahihi kutumia mali na fedha za serikali kutangaza maoni binafsi ya watawala, kwa sababu mwisho wa siku, unaposema nimefanikiwa kufanya kitu fulani, bado ni maoni yako binafsi ambayo yanaweza yasiwe na ukweli unaotaka kuaminisha watu. Ilipofika 1940, Congress ya Marekani ilikuwa imeshaondoa bajeti ya uendeshaji wa taasisi hiyo ya filamu, na badala yake uandaaji wa makala ukarudi katika taasisi binafsi moja moja za serikali.

Tukumbuke, hata leo hii sehemu kama Marekani, wakiwa wanataka kuishinikiza serikali isifanye kitu fulani, huwa wanazuia au wanaondoa tu funding kwa project hiyo, mchezo hua unaishia hapo. Of course, unaweza kusema sisi haitawezekana kwa sababu project nyingi zinafanywa bila idhini ya Bunge au funds zinahamishwa bila idhini ya Bunge au chama fulani kina majority bungeni, wanapitisha lolote wanalotaka.

Sasa tutafanyaje kuondoa matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kwa kisingizio cha 'Tumetekeleza'? Hayo nitawaachia nyie mtafakari, mimi nimeleta tu dondoo ya kuwakumbusha kuwa hakuna lililo jipya chini ya jua.
 
Hapana siyo kweli. Ukigoogle tu utapata maelezo ya kutosha kuhusu PBS. Kiufupi PBS ni shirika lisilo la kiserikali linaloandaa na kutengeneza vipindi mbalimbali vya kuelimisha jamii linalojiendesha kwa michango ya mashirika na watu binafsi pamoja na fees wanazochaji vituo vya television vinavyorusha vipindi vyao. Kiufupi, PBS haina mkono wa serikali.
 
Asante Kwa kunielimisha Nimetoka kugoogle hapa ni non governmental na non profitable na funds zinatoka kwenye fundraising na donations.
 
Maandiko yanasema, hakuna lililo jipya chini ya jua. Nimegundua moja ya jambo linalofanya tushindwe kung'amua, kuyaelewa na hatimaye kuyapatia ufumbuzi matatizo yetu mengi ni kuwa tunadhani matatizo yetu ni mapya. Kwamba, tunadhani hayajawahi kutokea sehemu nyingine. Matokeo yake tunashindwa kuyatafutia ufumbuzi ulio makini na unaodumu.

Nimekumbuka jambo ambalo niliwahi kulisoma sehemu moja. Wakati Marekani inapambana kutoka katika anguko la uchumi miaka ya 1930, yaani depression, taasisi moja inayohusiana na mambo ya kilimo katika serikali ya Marekani ilitengeneza makala fulani ya television, yaani documentary, iliyoitwa 'The River' ikielezea mafanikio ya Mamlaka ya Bonde la Tennessee (Tennessee Valley Authority)

Makala hiyo ilionyesha mafanikio mbalimbali yaliyoletwa na mamlaka hiyo, ikiwemo jinsi ilivyosaidia kukabiliana na matatizo ya mafuriko, kupungua kwa mazao ya kilimo na pia kuongeza uzalishaji wa umeme.

Sitaenda sana kwenye mambo ya kiufundi yaliyotumika kutengeneza makala hii ila itoshe kusema kuwa ile makala iliwavutia wengi, hadi Rais wa Marekani wakati huo, Franklin Roosevelt aliiona akaipenda hadi akatoa msukumo wa kuanzishwa kwa taasisi ya kiserikali ya utengenezaji wa filamu, U.S Film Service, ili waanze kutengeneza filamu nyingi za aina hiyo.

Lakini ile filamu ilikuwa na elements fulani za propaganda na wengi waliona siyo sahihi kutumia mali na fedha za serikali kutangaza maoni binafsi ya watawala, kwa sababu mwisho wa siku, unaposema nimefanikiwa kufanya kitu fulani, bado ni maoni yako binafsi ambayo yanaweza yasiwe na ukweli unaotaka kuaminisha watu. Ilipofika 1940, Congress ya Marekani ilikuwa imeshaondoa bajeti ya uendeshaji wa taasisi hiyo ya filamu, na badala yake uandaaji wa makala ukarudi katika taasisi binafsi moja moja za serikali.

Tukumbuke, hata leo hii sehemu kama Marekani, wakiwa wanataka kuishinikiza serikali isifanye kitu fulani, huwa wanazuia au wanaondoa tu funding kwa project hiyo, mchezo hua unaishia hapo. Of course, unaweza kusema sisi haitawezekana kwa sababu project nyingi zinafanywa bila idhini ya Bunge au funds zinahamishwa bila idhini ya Bunge au chama fulani kina majority bungeni, wanapitisha lolote wanalotaka.

Sasa tutafanyaje kuondoa matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kwa kisingizio cha 'Tumetekeleza'? Hayo nitawaachia nyie mtafakari, mimi nimeleta tu dondoo ya kuwakumbusha kuwa hakuna lililo jipya chini ya jua.
Sio kwemba walikataa kwa sababu private media zingekosa hela, ya kuadvertsise na ku air hizo session
 
Back
Top Bottom