Tujikumbushe kwanini Bunge la Marekani lilikataa uwepo wa television ya taifa

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
Maandiko yanasema, hakuna lililo jipya chini ya jua. Nimegundua moja ya jambo linalofanya tushindwe kung'amua, kuyaelewa na hatimaye kuyapatia ufumbuzi matatizo yetu mengi ni kuwa tunadhani matatizo yetu ni mapya. Kwamba, tunadhani hayajawahi kutokea sehemu nyingine. Matokeo yake tunashindwa kuyatafutia ufumbuzi ulio makini na unaodumu.

Nimekumbuka jambo ambalo niliwahi kulisoma sehemu moja. Wakati Marekani inapambana kutoka katika anguko la uchumi miaka ya 1930, yaani depression, taasisi moja inayohusiana na mambo ya kilimo katika serikali ya Marekani ilitengeneza makala fulani ya television, yaani documentary, iliyoitwa 'The River' ikielezea mafanikio ya Mamlaka ya Bonde la Tennessee (Tennessee Valley Authority)

Makala hiyo ilionyesha mafanikio mbalimbali yaliyoletwa na mamlaka hiyo, ikiwemo jinsi ilivyosaidia kukabiliana na matatizo ya mafuriko, kupungua kwa mazao ya kilimo na pia kuongeza uzalishaji wa umeme.

Sitaenda sana kwenye mambo ya kiufundi yaliyotumika kutengeneza makala hii ila itoshe kusema kuwa ile makala iliwavutia wengi, hadi Rais wa Marekani wakati huo, Franklin Roosevelt aliiona akaipenda hadi akatoa msukumo wa kuanzishwa kwa taasisi ya kiserikali ya utengenezaji wa filamu, U.S Film Service, ili waanze kutengeneza filamu nyingi za aina hiyo.

Lakini ile filamu ilikuwa na elements fulani za propaganda na wengi waliona siyo sahihi kutumia mali na fedha za serikali kutangaza maoni binafsi ya watawala, kwa sababu mwisho wa siku, unaposema nimefanikiwa kufanya kitu fulani, bado ni maoni yako binafsi ambayo yanaweza yasiwe na ukweli unaotaka kuaminisha watu. Ilipofika 1940, Congress ya Marekani ilikuwa imeshaondoa bajeti ya uendeshaji wa taasisi hiyo ya filamu, na badala yake uandaaji wa makala ukarudi katika taasisi binafsi moja moja za serikali.

Tukumbuke, hata leo hii sehemu kama Marekani, wakiwa wanataka kuishinikiza serikali isifanye kitu fulani, huwa wanazuia au wanaondoa tu funding kwa project hiyo, mchezo hua unaishia hapo. Of course, unaweza kusema sisi haitawezekana kwa sababu project nyingi zinafanywa bila idhini ya Bunge au funds zinahamishwa bila idhini ya Bunge au chama fulani kina majority bungeni, wanapitisha lolote wanalotaka.

Sasa tutafanyaje kuondoa matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kwa kisingizio cha 'Tumetekeleza'? Hayo nitawaachia nyie mtafakari, mimi nimeleta tu dondoo ya kuwakumbusha kuwa hakuna lililo jipya chini ya jua.
 
simple tu brother unachukua kibegi chako unahamia USA

Usiifananishe Tanzania na taifa la kishetani km USA linalonyanyasa Nchi ndogo kiuchumi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwenye nguvu ni mwenye nguvu tu. Hata umchukia.
Sisem tukubali kinyanyaswa ila kkmsingi wametuzidi kiuchumi.

And kama unadhani America tu ndio ina nyanyasa nchi ndogo, hata akina China na wenzie wanafanya the same.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bia yetu,
Wewe unafikiri kuhama ni rahisi kuchukua begi na kuhama tu? Una akili timamu kweli?

Kama mtanzania nina haki ya kujadili na kushauri kuhusu nchi yangu. Wakati mwingine tumia akili japo kidogo..kama huwezi acha kutoa mapovu yako hovyo.
 
Ndio Tunaomba lianguke, China hawezi nyanyasa watu km USA

Angalia Venezuela now,USA ameiharibu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Ungekuwa unakunywa ARVs ungeisifu na kuitukuza marekani kwani siku wasipoleta pesa ndugu na rafiki zako wote wanaoishi kea matumaini utawapoteza na huo ni mfano mdogo tu wa namna hili shetani linavyotetea maisha ya hawa wagonjwa maskini mungu ibariki tanzania,mungu ibariki amerika
 
Taifa la Tanzania inayo watu wa tofauti kabisa na mataifa mengine. Yule anaekula chakula hua ajui kama kuna wengine wana njaa wala hajui namna ya kuwawezesha ambao hawana chakula.

Siku ambayo hatapata chakula ndipo ataanza kupiga kelele kuhusu chakula. Nikupe mifano.
1. Ndugu Mkumbo, Kafulila, Machali, Mtatiro, Waitara, Sumaye, Makonda, Magufuli, Nape, Ninja Lugora, Kabudi, Polepole, Kakulwa; kwa nyakati tofauti wakinyimwa chakula wamekua wakali sana lakini kipindi wakirudishiwa chakula uwezi kuwasikia wakibweka tena.

Uwezi kutengeneza taifa na watu wa namna hii labda uwafungie ndani uwatoe mkishatekeleza azimio tayari.

Tafuta kitabu kilichoandikwa Rugged Constitution ujisomee watu wenye nia njema walivyokaa wakatengeneza taifa kubwa la Amerika.
 
Simple tu brother unachukua kibegi chako unahamia USA

Usiifananishe Tanzania na taifa la kishetani kama USA linalonyanyasa Nchi ndogo kiuchumi

Sent using Jamii Forums mobile app
Akili ya kwapani hii.
Taifa la kishetani ungekuwa unachukua condom zao unatumia.. ungekuwa unatumia ARV zao..ungekuwa unatumia barabara zilizojengwa kwa msaada wa watu wa marekani..
Bibi yako kijijini angekuwa anatumia visima vilivyojengwa kwa msaada wa watu wa marekani??
 
Nakuona mataga wa zamu unatakeleza wajibu wako..endelea kutumika kama toilet pepa mwisho wa siku watakuchabia na kukutupa shimo la choo.

#MaendeleoHayanaChama
Simple tu brother unachukua kibegi chako unahamia USA

Usiifananishe Tanzania na taifa la kishetani kama USA linalonyanyasa Nchi ndogo kiuchumi

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio Tunaomba lianguke, China hawezi nyanyasa watu kama USA

Angalia Venezuela now, USA ameiharibu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
China haiwez kunyanyasa watu? Wanavyowanyanyasa waafrika kutokana na covid-19. Waafrika wanakuwa denied service muhim wakishukiwa kuwa wanasambaza covid-19?
China ina mambo mengi mabaya.. tofauti ni kuwa wanaficha tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taifa la Tanzania inayo watu wa tofauti kabisa na mataifa mengine. Yule anaekula chakula hua ajui kama kuna wengine wana njaa wala hajui namna ya kuwawezesha ambao hawana chakula.

Siku ambayo hatapata chakula ndipo ataanza kupiga kelele kuhusu chakula. Nikupe mifano.
1. Ndugu Mkumbo, Kafulila, Machali, Mtatiro, Waitara, Sumaye, Makonda, Magufuli, Nape, Ninja Lugora, Kabudi, Polepole, Kakulwa; kwa nyakati tofauti wakinyimwa chakula wamekua wakali sana lakini kipindi wakirudishiwa chakula uwezi kuwasikia wakibweka tena.

Uwezi kutengeneza taifa na watu wa namna hii labda uwafungie ndani uwatoe mkishatekeleza azimio tayari.

Tafuta kitabu kilichoandikwa Rugged Constitution ujisomee watu wenye nia njema walivyokaa wakatengeneza taifa kubwa la Amerika.
fill the belly and empty the mind.
 
Back
Top Bottom