Mamboz, unakumbuka nini ambacho huwezi kusahau kipindi ukiwa msingi?
kaburu matata hia.matata hia...
mimi nakumbuka kitambu cha english book 7 toleo la mwaka 1968
unit one;
KALAGESYE
Everybody in the village of ibigi knew Kalagesye
my own first memory of him went back to time when
i was a very small boy, my sister and i were going to our glandmother's house.
sunddenly we heard, Alealealealeaa1" sung in good voice
"Quick, let's hide in the bush1" hissed my sister.
'but what for?" I said.
"there's a madman coming," she replied.
'No, he's not mad. he's just singing
Ahee ! Kana ka nsungu, ka nsung' umwelu
Ahee1kana ka nsu..........
International
Kuna mwalimu alikuwa hajui zile hesabustd six. Alikuwa anapiga bakora si mchezo. Lakini nitamkumbuka daima mwl theonestina nduke mwl wa kingereza std 4 nilizipenda hasa hasa zile story za mr daud,mrs daud , na watoto wao asha na baraka. Alinitoa utandu machoni. Mungu amrehemu mwanga wa milele amwangazie. Amina
Da! yan mi nakumbuka mambo mengi kwel yan,
1:Nakumbuka std1 kuna ticha wetu mmoja ye alikua akiingia tu darasan, yani ni full kuwaimbisha nyimbo za kisukuma mwanzo mwisho, regardless unakijua/hukijui ilikua ni lazma uimbe. sasa we pga buyu wakati wenzio wanaimba,utaona balaa lake!!
2:Namkumbuka ticha wetu 1 wa hesabu std6 swali lilikua likimshinda anavunga cm imeita anaenda kuongea nje,kumuona tena mpaka keshooo na akija halirudii. sasa we jidai kisabengo kumkumbushia hlo swal,utaona moto wake!
3: Nakumbuka kale kawimbo ka"huyo huyo huyoo isike shujaa,huyo huyo huyooo mangimeli shujaa kwa sime na rungu kampiga mkoloni"
Kumbe mkuu u kijana sana wakati unasoma primary mobile phone zilikuwepo.
Mfuko wangu wa sport wa kubebea daftari ulikuwa haukosi majarida ya sani, bongo na tabasamu, stori za john kaduma (r.i.p), fortunatus ndila, m.m.bawji n.k zilifanya niwe star clas kwa kusimulia! Namumiss captain mapung'o alivyopiga soka haijawah tokea, bifu la zena na betina dah mama betina alikuwa mwanga haijawahi tokea, jomba nchumali anapiga kona anafunga mwenyewe, chepe, lodilofa na mikwara ya mazoezi ya bush stars! Namiss sana!
Vp kuhusu kutajana wapiga kelele darasani...