Ilikuwa jumatatu tarehe 14/02/2000 mida ya mchana nilishuka kituo cha basi Moshi Technical Sec School nikiwa na mama yangu. Tukavuka barabara na kuingia shuleni ili kujiunga kidato cha kwanza. Nakumbuka nilikuwa nimechelewa wiki moja. Baada ya taratibu za usajili wakaitwa mwanafunzi wenzangu na kuambiwa wanipeleke hadi ofisi ya viranja maarufu kwa jina la TYL. Kutoka ofisi za waalimu hadi hapo TYL ni mwendo mrefu. Wanaoifahamu MTS wataelewa jinsi shule ilivyo na eneo kubwa. Nikiwa pale TYL ndo wanafunzi walikuwa wanatoka madarasani kwenda kula chakula cha mchana. Nilimwona kijana mmoja mdogo sana nikauliza ni nani huyu nikajibiwa huyo ndo kipanga wa form II. Kijana mdogo toka Manyara Ranch primary aliyekuwa akikimbiza form 2 nzima.
Waliponifikisha akaitwa dorm leader wa dorm 29, Mkwawa house ili kunipokea maana ndo bweni nililokuwa nimepangiwa. Nafika bwenini nakutana na mabro wenye sura za kihuni na mmoja wao maarufu kwa jina la GEFAMA alikuwa akivuta sigara. Hii ilinishangaza sana. Nikashangaa lile bweni kubwa ila vitanda vichache. Wale mabro walikuwa wakisikiliza muziki enzi hizo Sisqo na Dru Hill ndo wasanii maarufu duniani. Nilishangaa sana na kujiuliza kama nitaweza kuishi na hawa watu.
Wakati natafakari akaingia kijana mwingine alikuwa form II tukasalimiana na kugundua kumbe ni Home boy. Yule homeboy akaniambia usijali utahamia bwenini kwangu namba 24 maana hapa 29 majamaa mahuni watu wanawakimbia. Hatukupoteza muda tukahama. Moshi tech huwa vipindi mwisho saa 8. Then ni msosi na kuendelea na ratiba zako hadi kesho. Mchana huo homeboy akanipeleka uwanjani na maeneo mengine ya shule. Pale uwanjani nikaona kipaji hatari sana cha mpira kwa kijana aliyekuwa form II mwaka huo kwa jina la AMIR MRISHO MAFTAH. Alikuwa kidato cha pili ila ndo star wa football shule nzima. Pia alikuwepo SALIM ARAJIGA ambaye kwa sasa ni maarufu kwa jina la AHMED ARAJIGA akiwa refa maarufu nchini. Maftah na Arajiga wamesoma darasa moja. Uwanjani pia kulikuwa na mwalimu Mpande aliyekuwa anasimamia mazoezi. Huyu mwalimu kwa pale uwanjani sikumchukulia serious kumbe ndani ya masaa yasiyozidi 24 nitakutana na balaa lake... ITAENDELEA
Mara saa 12 jioni ikafika kengele ikagongwa kwa ajili ya roll call. Tulikuwa tunahesabiwa kwa house. Katibu wa Mkwawa house simkumbuki ila alikuwa jamaa mmoja mweusi naye mcheza mpira tegemeo enzi hizo. House ya Karume alikuwa jamaa mmoja mmeru nadhani jina ni Elishilia. Baada ya roll call ikawa muda wa msosi. Ugali maharage.. niwe mkweli ule ugali nilipiga kama matonge matatu nikaenda kumwaga. Ila nilishangaa watoto wa kisukuma walikuwa wanafurahia hatari. Baada ya msosi ni muda wa prepo.
Ila wakati tunajiandaa kwenda prepo kuna jambo lilitokea. Kumbe wale mabro wa dorm 29 hawakuridhika na mimi kuhamia dorm 24 wakaenda kuripoti kwa captain Mada Guy. Tukashangaa Mada Guy kaibuka pale dorm 24 na wale mabro kisha kutuita nje na yule homeboy. Captain akiwa kakasirika akampiga mabuti ya ugoko homeboy. Ilikuwa kitu cha kikatili sana. Baada ya hapo captain akasema nibaki dorm 24 ila usafi nifanye dorm 29. Ikawa imepita. Yule captain mara ya mwisho nilimwona huko mkoani Manyara akiwa kapigika vibaya kimaisha. Alikuwa katili mno jamaa.
Baada ya hiyo tafrani tukaelekea prepo. Kimsingi kwa sisi form one ilikuwa kama tunaenda tu kucheza madarasani maana bado tulikuwa kwenye orientation. Lakini kule prepo kulikuwa kuna kina John Kisomo kibao wameshaanza kuandika notes za waliotutangulia. Kuna baadhi niliona wanasolve simultaneous equation. Walikuwa wanatisha. Mimi nilipata kampani yangu ya stori za hapa na pale. Kama saa 4 usiku nikarudi dorm kulala.
Alfajiri saa 11 nikashtukia watu wanakurupuka vitandani kwa spidi ya ajabu na kukimbilia nje kama vile bweni limeshika moto... nami pia fasta nikaungana nao bila kuuliza. Kumbe ni Mwalimu Mpande kaja kuamsha watu kwa viboko. Mimi kuamka saa 11 nilishazoea nikiwa primary ila hii kuamshwa kwa viboko ilikuwa kitu kipya cha kuogofya. Saa 11 ikawa muda wa kwenda mchakamchaka na wenye zamu ya usafi kufanya usafi. Baada ya mchakamchaka ni kuoga na kwenda kupata uji. Ule uji ulivyokuwa wa moto na huku muda ukiwa unakimbia nilishindwa kumaliza kikombe kimoja kumbe baada ya muda nitakuwa mzoefu na kupiga hata vikombe vitatu.
Saa 1 na nusu tayari tulikuwa parade siku ya jumanne. Nakumbuka hiyo siku second master Mboya alikuwa anaongea ingawa sikuelewa kitu kutokana na lugha. Muda wa darasani ulivyofika nikakutana na wakali wa lugha ya kiingereza waliosoma pre-form one na English medium. Kuna jamaa mmoja wa Arusha alikuwa anatisha mno. Class pia kulikuwa na jamaa mmoja wa Shinyanga aliyekuwa anasolve maths topic za mbele sana. Mimi shule ya msingi nilikuwa star kitaaluma ila pale nilikuwa fala tu.
Siku ya jumanne na Jumatano pale Moshi tech huwa zina upekee kwa sababu msosi wa mchana huwa sio ugali maharage. Jumanne ni mchana ugali nyama na jumatano mchana wali maharage. Ukipangwa kuwa server hizo siku basi unakuwa uko matawi ya juu mno. Lazima watu wajipendekeze kwako ili ujaze sahani zao. Siku zilienda hatimaye ikafika IJUMAA JIONI...... itaendelea