Tujikumbushe enzi za ufalme wa Inspector Haroun

Kweli,waliona mbali sana na pamba zao "gangwe gear" nadhani walikuwa wanasimamiwa na Sebastian Maganga
Yaah! ni kweli Mkuu Seba ndio alikia na mkono wake pale na dili la kusaini ule mkataba Inspector alipiga pesa ndefu sana kwa miaka ile, ilikua ni Milioni moja ya Kitanzania. Sidhani kama kuna msanii aliewahi kupiga dili kubwa kama lile kwakipindi kile
 
Aliingia kujaza nafasi tu, maana mule ndani kuna vichwa vilikuwa vinaandika kweli kama Prof Jay, SoloThang,JayMo,Afande,Mwanafalsafa,Soggy, sasa hapo angetoboaje?, sema kwa rap katuni hakuwa na mpinzani. Nature alilalamika kwakuwa hakuingizwa kwenye mashindano, nikamshangaa aingizwe kwa mistari ipi?. Nakumbuka mwaka uliofatia walijaribu kutafuta Mkali wa Rhymes tena ila ikafeli za chini chini zilisema alipangwa mshindi washiriki wakajitoa, sema Fid alikuwa na nafasi ya kuchukua ndio alikuwa kwenye peak kwa wakati huo. Kwenye mistari yake anakwambia 'Washanitabiri watu wangu wa mtaani, mi ndio mfalme nitayefuata baada ya Suleiman...'
Hahah!!

Watoto wa Temeke hawakua wanastahili kuingia kwenye yale mashindano ila kama Nature angeingia labda angeshinda kwa ifluence ya mashabiki tu...

Mashindano yenyewe kipindi kashinda Afande yaliingia dosari maana wasanii kama Sollo walilalamika sana kua kuna namna imefanyika nakumbuka alitoa hadi ngoma akiongelea hilo swala ililua inaitwa 'kilio changu' kama sikosei
 
Wadau wengi naona wanabishania nani kaanza kati ya Inspector na Nature lakini mimi naona ni mabishano yasiokua na maana yeyote, kwasababu uzi unamuhusu Inspector acha nimuongelee yeye....

Jamaa Alitoa nyimbo ya kwanza mwaka 1998, 'Mauzauza', akiwa na Luteni Kalama kwenye kundi la Gangwe. ...

Baada ya hapo wakatoa nyingine mwaka 2000 'Mtu Be,' kisha ndio akatoa jiwe la 'Mtoto wa Geti Kali' ndio lilimpa umaarufu mkubwa. Aliutoa wimbo huu peke yake ingawa alikuwa bado yupo kwenye kundi lake....

Album walizotoa Gangwe bob

♤Simulizi La Ufasaha(2001)
♤Nje Ndani (2002)

Pia ikumbukwe jamaa ndio wasanii wa kwanza kua na website hapa bongo..

Gangwe=hardcoreView attachment 753914

Hii cover ya album yao inanifurahisha na kunisikitisha sana jamaa wamegonga ndala tu na pozi za hatari...

We have to respect them kwakweli wameitoa game mbali sana, ndio maana huwa najisikia vibaya mtu akiwabeza hawa wakongwe wa hili game...
Sema nini vingine walikuwa wanatudanganya kwavile wabongo tulikuwa hatuvijui, kuna mistari Inspekta anawema sasa wanapatikana kwenye tovuti 'wwgangwemobb.m', hapo tulikuwa hatuelewi kitu zaidi ya kuwapa respect tu
 
Hahah!!

Watoto wa Temeke hawakua wanastahili kuingia kwenye yale mashindano ila kama Nature angeingia labda angeshinda kwa ifluence ya mashabiki tu...

Mashindano yenyewe kipindi kashinda Afande yaliingia dosari maana wasanii kama Sollo walilalamika sana kua kuna namna imefanyika nakumbuka alitoa hadi ngoma akiongelea hilo swala ililua inaitwa 'kilio changu' kama sikosei
Yap alimshirikisha Q Chief, Solo aliumia sana naona ndo akaamua na kulitosa game la bongo na kukimbilia mbele
 
Pia ikumbukwe 'Nje ndani' ilikua album bora ya mwaka 2004 katika tuzo za Tanzania Music Awards ambayo baadae ndio ikawa Kili Music Awards...
 
Kwa mnao fuatilia bongo fleva toka kitambo nadhani mtakuwa mnamkumbuka sana huyu jamaa.
Haroun Rashid Juma Kahena.Almaarufu kama Inspector Haroun aliteka sana soko la muziki wa Bongo fleva miaka ya 2000 mwanzoni.
Tujikumbushe enzi za ufalme wa Inspector Haroun kwenye muziki wa Bongo Fleva
Title ilitakiwa kutaja jina la juma nature na sio inspectah,mawazo tu.
 
Nature katoka 2000 mwishoni, ilianza julietha ya dully, ikaja kigetogeto ya kingsepeto, biko na nature, ikaja machozi lady jay dee, ikaja kigetogeto remix ya nature na mr paul, ikaja niko gado, ikaja mtoto wa geti kali, ikaja jinsi kijana ya nature, hizi ni 2000 mwishoni, nyimbo za 2001 ni km bongo dsm ya prof jay, mtani jirani ya gwm na nature, maskini jeuri ya manduli mobb(humu yupo bwana mkubwa na mh temba feat nature) wakaja kina sister p, dah joh, balozi kwenye chat, jose mtambo, salome ya dully nk
Jose mtambo kaanza kabra ya wote uliowataja apo.
 
Kuna nyimbo moja ya kibabe sana inaitwa "bunda siliga"
japo nimeisahau kidogo.

Chorus:
Bunda siliga kiatu mtu
Hima saka mpira usijitusu
Huu thubutuu
Umo ndani kashilikiswa ommy g luteni wakati anaingiza verse alichemka kama mara kumi ivi adi mastar j akamtaka aje kuludia siku nyingine kwa sababu tulikuwa tunawai kwenye lieso ya summer jum mwaka 2001 ambayo siku izi ndo inaitwa fiesta
 
Mbukwa Tai.
Bye bye
Mtoto wa uswazi.
Nje ndani
Kisa cha baba mkwe.
Vidonge vyao
-------------------
Usafiri choki ndani ya RVR hahahahaa
 
Pengine aliamini ye ndo mkali kuliko wote. Sema binafsi nilikuwa namkubali Solo kuliko Afande
Mimi nilikua mdogo sana nilitekwa na upepo wa darubini ila nilivyopata upeo wa kupambanua mambo nikaona Prof. alistahili kupata ule ushindi...
 
Umo ndani kashilikiswa ommy g luteni wakati anaingiza verse alichemka kama mara kumi ivi adi mastar j akamtaka aje kuludia siku nyingine kwa sababu tulikuwa tunawai kwenye lieso ya summer jum mwaka 2001 ambayo siku izi ndo inaitwa fiesta
"makerere,
Makerere shule aliyosoma Nyerere"

Bunda siliga,kiatu mtu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom