Katika programu nzuri na tamu katika ukokotoaji, uchambuzi, uwasilishaji wa data zilizopo katika namba na kupanga mambo mbalimbali ya kihesabu tunajua Excel Ina fanya yote hayo, Excel imekua ikitumika karibia Kila professional ikiwemo Engineering, Accounting, Medical professions na nyingine nyingi.
Hivyo basi sababu tunajua Excel ni pana sana na haiwezekani mtu kujua Kila kitu naomba tupia ukijuacho kuhusu Excel ili tupate elimu ya programu hii tamu ambayo inatumiwa na kila wataalamu katika kufanya kazi zao "kivyao" kama unaijua formula usiache kutujuza Kwa mfano mi naanza na hizi chache Hapo chini
Excel ni moja ya spreadsheet pana sana,binafsi naitumia excel na google sheets kwa ajili ya kutrack KPI na kufanya baadhi ya Analysis, si lazima kumaster kila kitu kwenye hizo labda kama wewe ni mkufunzi, cha muhimu kuwa deep sehemu zinazokusaidia kwenye shughuli zako, baadhi ya functions ambazo nazitumia sana ni
1.Count & Sum functions - hizi ni countif, countifs, counta,sumif, sumifs sum n.k
2.Lookup functions - vlookup, match and index, sumproduct
3.Logic functions - if, ifs, nested ifs, and , or n.k
4.Errors - iserror, isna n.k
5.Importrange - kulink data kutoka sehemu mbalimbali ktk google sheets
Zipo nyingine ambazo nazitumia mara moja moja kutokana na situation mfano average,average if, mode,mean,max,min,filter, query n.k. Zaidi ya formula & function natumia pivot table kufanya quick analysis, na natumia Charts kwa ajili ya kusummarize matokeo na kutengeneza dashboard pia natumia Power query kwa ajili ya kuandaa data kabla ya kuzianalyse, Macros na VBA natumia mara chache sana kama nimetingwa.