Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,959
- 719
Nimekuwa nikifuatilia siasa na muelekeo wa nchi jirani Kenya. Mwaka jana kabla ya uchaguzi nchini humo tuliona kikundi cha Redykyulass kikizunguka karibu nchi nzima kufanya kampeni ili wananchi wa Kenya kujitokeza kwa wingi kupiga kura. Na walijitahidi kwa kadri walivyoweza kutumia vipaji vyao kuwaeleza wananchi wa Kenya nini kilichokuwa kikiendelea nchini humo.
Kwa kutumia vipaji vyao waliweza kumuakilisha mwananchi wa kawaida nchini Kenya kwa kuonyesha maisha duni wanayoishi. Jinsi haki zao zinavyopotezwa na kuupuzwa by hao walioko juu. Na siamini kama Redykyulass walikuwa ni wawakilishi wa chama cha ODM bali walichokuwa wakikisimia kilikuwa ni sawa na kile ambacho ODM ilikuwa ikikipigia kelele "HAKI YA MKENYA"
Tulishuhudia wananchi walijitokeza kwa wingi kwa ajili ya kutetea na kudai haki zao kwa njia ya kura. Sio siri, siasa ya Kenya imebadilika na ninaamini itakuwa na ADABU.
Watanzania tumekuwa tukipoteza haki na mali zetu kwa MAFISADI. Sasa hivi mtanzania anagharamia gharama kubwa za Umeme kutokana na Mdudu RICHMOND. Wanafunzi wanakosa madawati, wananchi wanakosa madawa, maji safi n.k kisa ni MAFISADI kujikwapulia chochote walichotaka. Waakanza kuumbuliwa na Mh. Dr. Slaa, tukaona serikali kwa kutumia kodi yetu kusafirisha mawaziri wake nchi nzima kuzima hicho cheche za Slaa na Zitto.
Najua baadhi ya vyombo vya habari Tanzania vinajitahidi kuweka Uchafu wa viongozi wazi ili wananchi wajue ni nini kinafanyika. Na JF imekuwa mstari wa mbele katika hilo pia.
Nikirudi kwenye Mada, kikundi hiki cha Redykyulass kiliweza kuwaelimisha wananchi wa Kenya jinsi ya ku-reclaim their country and rights back. Hawakuwaachia ODM na vyama vingine vya upinzani kuwaelimisha wananchi wao jinsi serikali inavyochezea haki zao. Na hapa kwetu tujifunze hilo, tutumie uhamasishaji huo huo kuwaelimisha wananchi kuwa gharama za maisha imekuwa juu, madawa hayaonekani, maji safi hakuna na mahitaji muhimu hayapatikani kutokana na ubadhirifu wa baadhi ya viongozi (MAFISADI). Serikali imekuwa kimya kuwachukulia hatua hao watuhumiwa. Sasa tunasikia kuwa katika tume ya Rais inayoongozwa na Mwanyika imeingiliwa na FISADI ambaye naye anashirikishwa katika vikao vyao. Sasa hapa tunafanya nini!!
So, kila mwenye uwezo wa kutumia talent yake basi na aitumie katika kuwaelimisha wananchi huu uchafu na tusiwaachie Wapinzani. Wenye talent ya uhandishi tumeona kazi yao na wengine wako hapa kutufahamisha kile ambacho serikali haitaki sisi tujue. PENYE UKWELI HAKI USIMAMA NA HATA KAMA ITACHELEWESHWA.