Tujalie Wz’bar tuna Muungano na Tanzania Bara?kilicho tunganicha ni nini hivi sasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujalie Wz’bar tuna Muungano na Tanzania Bara?kilicho tunganicha ni nini hivi sasa?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by abdulahsaf, Mar 31, 2011.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2011
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Tujalie Wz’bar tuna Muungano na Tanzania Bara?kilicho tunganicha ni nini hivi sasa?
  Waungwana? mimi nashindwa kufahamu jee tuko ktk Muungano au tuko ktk mazoea tulio kwisha zowea? maana haingii akilini kuwa kiungo cha Muungano wenyewe Tanganyika na Raisi wa Zanzibar kuwa Makamu wa Raisi havipo? Sasa tuseme bado tuko katika Muungano tu? ni Muungano gani utauwita huu hivi sasa?mimi nahisi itafika wakati Wzanzibar tutashekwa kwa kuibiwa kimacho macho na wajanja.
  Kitandawili shengine kati ya Bilali na Raisi wa Zanzibar Dr Shein yupi boss? na kazi za Bilali ni nini hasa? Mimi sioni kazi zozote muhimu za kuiwalikicha Zanzibar huyu ispokuwa kuitwa sehemu kwenda kutia jiwe la msingi au kukata utepe?.
  Wzanzibar tushajizonga wenyewe nilazima tujizongowe haraka iwezekanavyo tukisherewa mbeleni tutaingiwa na mtafakuri wa mawazo kishwa tele na kuyatatuwa tushindwe, kama ni kupigania jihati basi kwanza tuanze kupigana jihadi ya nchi yetu kuitowa ktk makucha ya mtawala mweusi na kama ni mapinduzi mingine ya uhuru wa Zanzibar basi tuanze sasa bila kusherewa.
  Hivi sasa nitabu kuweza kumjuwa ni yupi ndie na yupi sie kutokana na wimbi kubwa la ingia toka la wageni jee huko mbeleni kwenye mawimbi makubwa kutakuwajee? Mimi namshukuru sana Pinda alipo kuja kutushtuwa na kuwatowa taka za mashkio ccm/smz kusema Zanzibar sio nchi na ndoto yake ni kufa kwa smz na Baraza la Uwakilishi ndio kero za Muungano zitakuwa zimepatiwa ufunbudhi.
  Sasa kutokana na unafiki wa viongozi wetu wa ccm/smz wana mapinduzi walitaka kujitowa kimaso maso bada ya kuyaanika mambo hadharani Pinda wakasema Pinda kateleza hakukusudia hivyo? Pinda akasema sijakosea niko timamu na nakisemacho.
  Wzanzibar tukisema tuna Serekali na viongozi shujaa tulio wakabidhi nchi wailinde basi tunajidanganya ndani ya Serekali kuna watapia mloo na wanafiki wa matumbo yao tu. Shujaa tutamuona April 8/4/2011 pakisha pitishwa mswada wa katiba jee wata shikamana kusema katiba sio muhimu kwa Zanzibar umuhimu kwa sasa ni kurudi ktk mikataba ya Muungano na bila Tanganyika hatuto kaa meza mmoja kwa ubatizo wa Tanzania.
  Wenzetu ukiwatajia Tanganyika huchopowa kwa kujuwa ikirudi Tanganyika zulma na kuikalia kimabavu Zanzibar baasi, ndio hujifanya hawaitaki kwa maana yao,vipi mtu mtoto memzaa mwenyewe umkatae na ukatafute mtoto wakulea?. Huu ni mtego wajanja wanautumia kwa mbubumbu ccm/smz siku nyingi, lakini ikiwa na cuf nawao niwajanja basi tutawaona mwaka huu?.
   
Loading...