Fixed Point
JF-Expert Member
- Sep 30, 2009
- 11,304
- 12,753
sina wasiwasi kabisa kuwa mama yangu ananipenda sana tena sana kabisa.......
Najiuliza ni fair kutoa statement kama hii?
Ni kweli kabisa kuwa mama zetu wanatupenda sana kuliko mtu yeyote anavyotupenda?
Nina uhakika naweza kupima mapenzi yangu kwenda kwa mwingine, nina uhakika kabisa nani nampenda zaidi kuliko mwingine, lakini unaweza kujua kwa uhakika kabisa kuwa nani anakupenda sana kuliko mwingine?
Ni kweli wababa hawapendi watoto wao zaidi ya vile ambavyo mama zao wanawapenda?
Tuachane na story za kusema "mama alimbeba mtoto tumboni miezi 9" ndo sababu anampenda sana. kuna wamama ambao wanabeba mimba na wanatupa watoto au kuwatelekeza.
Haya mapenzi ya kutota upande mwingine tunayapimaje?
Naomba tujadiliane hili tafadhali