Tujadili kuhusu matuta barabarani

mie sio mtaalamu .. but nachojua yanawekwa ili kudhibiti mwendo mkali na wakati mwingine kwa demand ya wananchi baada ya eneo husika kukumbwa na ajali mara kwa mara.

but to be honest yanahitaji standard mengine ni makubwa hadi kero.. ukipita na ka vitz kako unatamani ukabebe mgongoni kukavusha kwi kwiiiiiii.
 


umeona eeh neggirl.....hapa ni akili ya kawaida tu wala sidhani kama ni utaalamu wa kwenda anga za juu unaohitajia

nashauri TBS waweke standards au unaonaje jamani
 
Last edited by a moderator:


Mkuu mwanaharakati mamba kweli wewe ni mamba, hoja yako imeshiba sana. Nilipobold umeonyesha issues zinazohusiana na uwekaji wa matuta na kumbe haw jamaa wa TANROADS ndio ulaji wao?

Maana nimekuwa nikijiuliza, kwa nini matuta hayako integrated kwenye ujenzi wa bara bara toka mwanzo? Kwa nini wanasubiri kwanza wakishaweka lami hadi mwisho, ndio wanaanza KUIBOMOA tena kuweka matuta? katika design kwa nini hii isiwepo?

Kweli kabisa highway zimepoteza umaana na uhalali wake tukubaliane tu kwamba tuna vistreet tu...

learned brother Mr Rocky hebu tupe muktadha wa kisheria hapa na besidei boy Ruttashobolwa
 
Last edited by a moderator:
mie katika pita pita zangu huko nje sijaona matuta. Kaizer

hahaah Kipaji Halisi unamaanisha nje ya nchi? kama nje ya nchi sawa hawana hii makitu bana,,,kule ni sheria mtindo mmoja na watu wako conscious, huku majanga

kama ni hapa mitaa ya bongo utakuwa umeona hii
 
Last edited by a moderator:
haki ya nani sitoagi zaidi ya hiyo tena hapo unakuta nina haraka ya kuwahi mahali otherwise nipo tayari kabisa tupotezeane muda coz ya 5k, bia mbili ati hapo, hahahahha,

hahaaa na chenji inarudi kutegemeana na bar....lol
 

Mkuu nje unakusudia Ulaya, Marekani? usiende huko kote tembelea hata kwa jirani zatu tu hapa Afrika mashariki mbona mambo ni tofauti na hapa kwetu,experience yangu ya Uganda, Burundi na Kenya inanionesha alama za barabarani ni nyingi zaidi ya matuta especially kwenye highways. Taztizo ni nni? ignorance ya madereva au watumiaji wengine wa barabara au wote?
 
hahaaa na chenji inarudi kutegemeana na bar....lol

unaona sasa, mie mara kibao namcal msukuma nimekamatwa, hapo tumefanya ubishani wa kumpa 5k,hahahaha, kuna jmosi moja niliimalizia kituoni, mwanamke nimegoma kutoa 5k, kuna trafiki wawili wa kike wananichukia mbaya kabisaaa, (sikuwapa walichotaka)hahahahaha yaani wameshika no ya ka vitz kangu kama sala ya baba yetu, wakiniona kuanzia kuleeee lazima wanipige mkono na mkwara wa kike kike juu.
 
Kwa sheria za kimataifa Highway haziruhusiwi matuta! Yawe yenye kiwango ama hayana. Ukienda kwa nchi za wenzetu kuna askari wenye magari na hata pikipiki ambao kazi zao ni ku-control speed. unapoweka speed humps ni hatari as sio kila mmoja mwenyeji wa barabara hiyo! Hasa ukizingatia kwa serekali yetu ni ANASA kuweka vibao mbalimbali vyenye kuonyesha matazamiao ya kinachojiri mbele! Kwa uzembe wa traffic wetu wao hukaa na kukusanya mapato tu bila kufuata sheria!
Mimi nafikiri serekali itafute njia mbadala! Mojawapo ni kufunga wireless cameras kwenye highways ambazo hizo hazihongwi unless waamue kuziharibu! Dereva akizidisha mwendo kamera inapeleka kwenye central data base then driver ama owner wa gari anakutana na bill yake kwenye box lake. Hii mambo ya kuongeaongea na maaskari ifikie mwisho sasa.
 
Ni kweli
 
Njia hii unahitaji kusivilise kwanza wananchi wako, yaani uwe na mfumo mzuri wa kutambua watu, hii kwa bongo tunahitaji miaka kibao! kwanza hata data base ya nchi hatuna unategemea hiyo barua ieende kwa nani? watu tunaauziana magari ka karanga..! mpaka huyo mtu anakuja kukamatwa ni maisha mangapi yameshapotea? kuleta idea za nje bila kuzi locolised ni kutwanga maji kwenye kinu
 
kuna tuta moja lipo eneo linaitwa nyeregani! kabla hujafika shinyanga ukielekea mwanza...

ile kitu ni noma.
Tunashukuru kidogo, barabara ya kuja huku kwetu Mtwara haiwekew matuta mengi sana!!

Then matuta hayapunguzi ajal kivile..
tuta copy nayo tu!
 

haaaa na mwenyewe umehakikisha hadi first aid kit unayo mwe mwe mwe mwe
 

Najua wengi wangesema hivyo kama wewe lakini inawezekana kabisa. Uvivu wa kufikiria ndo unatufanya tusitambue haya. Wewe unaamini kuwa hatuwezi kuwa na database ya nchi hii? We unakubali kuwa matuta ni suluisho? Hiyo miaka kibao unayoiongea watakuwa wamekufa wangapi ka matuta tu achilia mbali mwendo kasi?
Mradi wa anuani za makazi ya watu alieyeuanzisha ni mwananchi ama viongozi wako? Mbona hausikiki tena? Narudia ni uvivu wa kufikiri tu ndo unaotufanya tuwe hapa!
 
kuna tuta moja lipo eneo linaitwa nyeregani! kabla hujafika shinyanga ukielekea mwanza...

ile kitu ni noma.
Tunashukuru kidogo, barabara ya kuja huku kwetu Mtwara haiwekew matuta mengi sana!!

Then matuta hayapunguzi ajal kivile..
tuta copy nayo tu!

Mkuu kiwatengu nalipata ilo ni noma!
 
Last edited by a moderator:
Tatizo hukunielewa mwanzo, mi nimekupa scenario kama hiyo kua tunahitaji kufanya vitu vingi kabla hujafikia hapo kwenye kamera na fine ya posta! sikusema matuta ni suluhisho hila nilichosema hao wanataka matuta yaondolewe itakua shida..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…