Mkuu ni ukweli usiopingika kuwa madereva wengi wa nchi hii hawazingatii sheria za usalama wa barabarani...
Kwa mantiki hiyo nadhani ndiyo maana wasimamizi wa usalama walikuja na idea ya kuweka matuta kama moja ya njia ya kudhibiti mwendokasi wa vyombo vya usafiri...
Hilo ni wazo zuri sana tu, lakini kasoro iliyopo ni kwenye utekelezaji wa lengo hilo...fine wameamua kuweka matuta lakini kuna matuta mengine aisee nadhani ni adhabu kwa madereva na magari...
Hapa Dar kuna baadhi ya njia zina matuta makali mno mathalani barabara ya Akachube na nyinginezo kadhaa...
nakubaliana na mchango wa watu8.
The THOMCOM Inc.: Magufuli akataza matuta barabaraniMagufuli akataza matuta barabarani
Posted by B.M.T on Tuesday, January 04, 2011 // 0 comments
IWAZIRI wa Ujenzi, John Magufuli, amepiga marufuku ujenzi wa matuta kwenye barabara zote kuu nchini kwa kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria.
Pia ameagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kukagua na kusimamia miradi yote ya barabara za lami inayojengwa kwenye maeneo yao, tofauti na utaratibu uliokuwapo wa
miradi hiyo kukaguliwa na wataalamu wa makao makuu.
Magufuli alitoa maagizo hayo juzi alipozungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo mjini hapa, baada ya kukagua barabara ya Singida-Katesh wakati wa ziara yake ya ghafla ya siku moja.
Katika ziara hiyo pia alimwagiza mkandarasi anayejenga barabara ya Singida- Katesh - Sinohydro Corporation Limited ya China, kukamilisha kazi hiyo kwa wakati, vinginevyo Serikali haitaipa zabuni nyingine siku zijazo.
Kabla ya kutoa maagizo hayo, Kaimu Meneja wa Tanroads wa Mkoa, Joseph Masige, alisema ujenzi wa barabara hiyo uko nyuma kwani kazi iliyofanyika hadi sasa ni asilimia 51 tu badala ya asilimia 70 iliyopangwa.
"Ni kweli ujenzi unakwenda vibaya. Lazima mbadilike, mmalize kazi hiyo kwa wakati bila visingizio vyovyote, vinginevyo nitahakikisha hampati zabuni yoyote nchini.
"Kwanza mmelipwa fedha nyingi sana. Badala ya kununulia mitambo na zana mpya, nyie mnafanya mchezo wa kuhamisha vifaa hivyo kutoka mradi mmoja hadi mwingine kitendo kinachodhoofisha ufanisi wenu.
Hapa si mahali pa kuja kucheza," Waziri alimwonya mkandarasi huyo ambaye aliwakilishwa na Meneja Mradi huo, Xhinhua Chen.
Awali Chen alisema moja ya sababu za kuzorota kwa ujenzi huo ni kucheleweshwa malipo yao na Serikali suala ambalo Waziri aliahidi kulifanyia kazi.
Barabara ya Singida - Katesh yenye urefu wa kilometa 65.2 inafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa asilimia 60 na Serikali ya Tanzania asilimia 40 na inatarajiwa kukamilika Septemba mwaka huu.
Matuta yanatuharibia sana magari hasa sisi tulio na Vitz tunapata tabu sana.........
Bila matuta wenye Vitz mnatumalizia ndugu na watoto wetuMatuta yanatuharibia sana magari hasa sisi tulio na Vitz tunapata tabu sana.........
Hivi mkuu hekimatele kwa hekima kabisa huoni kuna haja yankuwa na viwango vya haya matuta? Maana apo ndo kuna balaa
Nakubaliana na wewe lakini kwa uzoefu wangu katika pita pita zangu humu Tanzaniano ni ngumu kufanya kama unavyosema. Unakuta sehemu nyingine ni high way ila kwa sababu kuna vijiji na makazi ya watu lazima tuta liwekwe la sivyo tutapoteza watanzania wengi sana huku nchini. Madereva tulionao wengi ni careless sana. Wao ndo wana haraka kuliko mtu yeyote huku duniani. Binafsi napenda sana kuheshimu wapita njia (pedestrians) kwa sababu hata mi kuna siku natumia njia hizo kama wao.
Bila matuta wenye Vitz mnatumalizia ndugu na watoto wetu
Nakubaliana na wewe kabisa kwenye point ya standard za matuta hapo ndo tunakosea ila kuondoa matuta ni kukaribisha janga kwa watoto wetu. Kiuhalisia madera wa bongo hatufuati sheria kabisa kwa hiyo dawa ni matuta, kwasababu tuta huwezi kulihonga upite itabidi upunguze tu mwendohahahahh Zanta bana......matuta sawa. hata ukiwa kwenye basi, kuna matuta unaona kabisa hili hapana
Mara kibao nimeona magari yakiwa yameviringika kutokana na kukutana na matuta makubwa pengine yasiyokuwa na alama na hivyo kusababisha uharibifu mkubwa
Katika pita pita zako huko nje umeona hao madereva wa nje wanavyotii sheria? huwezi kulinganisha na wakwetumie katika pita pita zangu huko nje sijaona matuta. Kaizer
Bila matuta wenye Vitz mnatumalizia ndugu na watoto wetu