Tujadili Kiukweli (Wanaume tu) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujadili Kiukweli (Wanaume tu)

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ligogoma, Feb 6, 2011.

 1. Ligogoma

  Ligogoma JF-Expert Member

  #1
  Feb 6, 2011
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 2,142
  Likes Received: 860
  Trophy Points: 280
  Habari wana JF

  Mwenzenu nimeoa (mke mfanyakazi) miaka mitatu iliyopita na kujaaliwa ka baby boy mmoja tu.

  Tatizo langu ni, mke wangu kamwachia majukumu yooote msichana wa kazi! Kwa mfano, usafi wa nguo zangu, maandalizi ya chakula na kazi zote za nyumbani.

  Hilo mimi sijali lakini najiuliza kuhusu hili, ninaporudi nyumbani na kifurushi mkononi hata kama mke wangu amekaa tu hana kazi yoyote atamwita msichana wa kazi na kumuamuru anipokee. Anaponipokea anasema, shikamoo baba......, pole........., karibu............., tena kwa unyenyekevu wa hali ya juu. Mke wangu desturi hiyo hanaa!!

  Atakapoandaa chakula house girl huyu huyu ataninawisha mikono na kunikaribisha chakula kwa unyenyekevu mkubwa akisema `karibu chakula baba`. Wife wala habari hana, na siku akiandaa msosi wife atasema `Baba nanii....chakula tayari`.

  Asubuhi chai napo ni vivyo hivyo, atapewa house girl viatu asafishe (kubrash) then atanirudishia na kunambia kwa utulivu, viatu tayari baba!!

  Mbaya zaidi juzi nikamkuta chumbani kwetu kwenye bafu (master) anafulia huko huku wife akiwa amekaa barazani na wenzie wanapiga story. Nikamuuliza unafanya nini huku na kwa ruhusa ya nani, alinijibu kuwa mama kamwambia afulie nguo zetu kule (za mimi na wife) then afanye na usafi wa kule msalani na chumba kizima, pia nahisi alitakiwa afue hata nguo za ndani coz nilikuta zimelowekwa pale pale.

  Kiukweli nilichukia sana na akili ilinituma nimchape kitu yule binti (ku-mdo) but ni busara tuu iliyoniepusha.

  Nimejaribu kumrekebisha mara kadhaa ananisikia na kunielewa but anaonekana ni mvivu kutimiza wajibu wake. Wife ni msikivu sana but sielewi tatizo nini jamani.

  Swali langu ni kwamba, wanaume wenzangu mnayarekebisha vipi mambo kama haya coz kikawaida hisia zinaweza kuhamia kwa binti kwa jinsi alivyoachwa kuwa karibu nami na hasa wife alivyojiweka mbali ili nisije zua balaa.

  Asanteni sana
   
 2. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #2
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Mkuu hapa naona unatafuta excuse, ukiona kama ni kero sana basi tafuta Houseboy.

  Ukigusa hapo huenda hata hiyo heshima unayopata sasa ikaisha wewe ndio ukaishia kuwanawisha wote mikono na kufua nguo
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Hauko peke yake broda, ndio maana wengi wa akina baba wanawado. Kina mama wakishaolewa huona wamemaliza mchezo. Mwisho wa siku utaambiwa chakula kiko jikoni , eti nimechoka . ????
   
 4. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #4
  Feb 6, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,859
  Likes Received: 4,544
  Trophy Points: 280
  Duh! Pole sana mkuu!

  Kwani huyo wife wako ulijuana nae kwa muda gani mpaka mkaja kuoana? Mana nafikiri kama tabia iyo ya kivivu ungekua umeijua kabla hata ya kuoana.

  Nway kwavile tayari mmeshaoana,suluhisho ni muhimu. Mi ningekushauri husikate tamaa ya kuongea na mkeo ili umueleweshe kua tabia yake ya uvivu hauipendi. Pia ungemweleza wazi kua tabia ya kumwagiza housegirl afanye kazi zote ambazo yeye kama wife alipaswa afanye,inaweza hatarisha ndoa,kwani housegirl mwishowe anakua karibu yangu kuliko wewe mke wangu!

  Honesty itatatua tatizo,kwani kama wife anataka ndoa hisivurugwe na housegirl,then atajirekebisha haraka.

  ANGALIZO: Tafadhali husiinge mtego na ushawishi wa kum-do uyo beki 3! Ni hatari kwa ndoa yako,unaeza kujenga kibanda na mwishowe mkeo ukamwona hafai.

  Ni hayo tu.
   
 5. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #5
  Feb 6, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  nyie wababa na nyie mmezidi...
  yaani ulitaka housegirl awepo na mkeo afanye kazi zote hizo???
  sasa mliajiri housegirl wa nini???
  kama kakunyima unyumba,au hajitengenezi ukirudi unamkuta yuko rough...ningeona basis ya malalamiko yako!
  kwa sasa naona unatafuta tu excuse ya kutembea na huyo housegirl...shame on you!:twitch::twitch:
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  mada ya wanaume hii, NGoja kwanza tUjadili tukimaliza tutakuita uje uone mikakati tunayojiwekea
   
 7. Rwamuhuru

  Rwamuhuru Member

  #7
  Feb 6, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole bro.mkeo anapaswa kuacha uvivu wa kijiga. msaidie kufahamu anawajibu wa kutekeleza ili kutunza ndoa yake
   
 8. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Shame on you.....tena uombe hiyo roho ikutoke....solution ya tabia ya mkeo haiwezi kuwa kulala na huyo house girl.....i pity some women....
  nashindwa hata kukushauri.....umeshafikiri kubaya sana.......:A S thumbs_down:
   
 9. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  He!! Kwaheri......
   
 10. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wasalimie nyumbani Tandahimba!:msela:
   
 11. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Chelle usikasirike huyu jamaa ana point kuwa vitu vyote alivyotakiwa kufanyiwa na mkewe anafanyiwa na HG anakaribishwa,ananawishwa, anafuliwa mpaka chupi wamekuwa na ukaribu nae sana.Bado hajalala na HG mshauri aweze kurekebisha uhusiano.
   
 12. LD

  LD JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nooooooo acha mawazo mabaya, wala msimpe ibilisi nafasi, nauliza tu ukitembea na huyo house girl unakuwa umemkomoa nani?? Mkeo au huyo binti. Wewe mwache mtoto wa watu, kama umeshindwa kumshauri na kumfundisha mkeo usimwaribu mtoto wa watu, makazi yote akufanyie afu bado.......... Wewe wewe!!! fanya wewe hizo kazi umuoneshe mfano huyo mkeo. Hiyo roho ishindwe na ilegee!! Haya mnisamehe kama nimewavamia.
   
 13. Mbaha

  Mbaha JF-Expert Member

  #13
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 697
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mnanishangaza, kwanza nyinyi si wanaume, pili badala ya kumpa solution juu ya matatizo ya huyo mwanamke mwezenu anaeshindwa kutimiza majukumu yake mnadakia kumshambulia!!! Kwani aliyesababisha jamaa kufikia kuwaza hayo ni nani?? si mwanamke mwenzenu??

  Mkubwa kama sikosei umesema mkeo umeshamuonya mara kadhaa lakini habdiliki, mimi nakushauri kama hali hiyo inaendelea itabidi uitishe hata kikao cha wazee wanaomhusu wamuonye mkeo. Kwa kweli ni jambo la aibu beki 3 kuingia katika chumba chenu tu wacha kufua nguo zenu za ndani!!! Hayo mambo ya kupokewa mzigo, kuandaliwa chakula na beki 3 siyo mbaya sana lakini maswala ya chumba chenu yanatakiwa yawe yako na mkeo tu. Mawazo ya kum-do beki 3 yafute kabisa!!! Mwisho wa ubaya aibu!!!
   
 14. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #14
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Jinsia yangu haioneshwi na avatar....naweza kuwa mwanaume au mwanamke......

  Pili umeshamshauri,asante sana.
   
 15. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #15
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 196
  Trophy Points: 160
  Roto....lol,naona unafupisha jina langu nimeona nifupishe na lako.....
  namshauri amueleze mkewe anayesema ni msikivu jinsi ambavyo hili linamuumiza na hapendi wajibu wa mkewe ufanywe na HG......mwanamke anayempenda atamuelewa,na pia amuombee Mungu hilo li roho linaloleta fikra za kulala na HG lishindwe yawezekana limekuja bomoa ndoa na furaha yake....inaanzaga viubishi vya hapa na pale mwisho ndoa kwishney....so,please talk to the woman you love..
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Feb 6, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Umekosea kua na mawazo ya kutembea na HG wako!!
  Tayari umeshasema mkeo na msikivu...sasa kwanini usimwambie jinsi
  gani kutojihusisha kwake na mambo mengi yanayokuhusu inavyokukera?
  Vunja ukimya...ongea nae!!
   
 17. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #17
  Feb 6, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Now that is 'our resident queen ' talking,tatizo ukifupisha jina langu linakuwa tusi lol!
   
 18. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #18
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kama umemshauri na bado habadiliki jaribu kuipeleka hiyo mada kwa walowazidi umri ila nao wajaribu kumshauri....Ila katika mambo yote mkuu usijaribu asilani hata siku moja kumlamba huyo mtoto.... Ila hiyo ya kurudi na kumkuta chumbani kwenu anafua nguo zenu na 'kufuli' sijawahi sikia... Aisee hapo nakupa pole sana mkuu :twitch: .....
   
 19. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #19
  Feb 6, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Pole sana kaka ila nasi wadada tukiolewa tunajisahau sana agrrrrrrrrr
   
 20. s

  seniorita JF-Expert Member

  #20
  Feb 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wanaume mnaona ili mpate wa kuwafanyia kazi kama wafalme! Duh, hayo makubwa....mbona na wewe mwanamume usim-encourage waif wako mfanye hizo kazi pamoja; hasa kama na yeye ni mfanyakazi somewhere else...hizo bla bla zote ni kututafuta "justification" kwa kutoridhika baada ya kuona, acheni kuangaza angaza huko na huko...kwani kabla hujaoa, nani alikuwa anakufanyia hayo yote?
   
Loading...