Tujadili Kiukweli (Wanaume tu)

Wanaume mnaona ili mpate wa kuwafanyia kazi kama wafalme! Duh, hayo makubwa....mbona na wewe mwanamume usim-encourage waif wako mfanye hizo kazi pamoja; hasa kama na yeye ni mfanyakazi somewhere else...hizo bla bla zote ni kututafuta "justification" kwa kutoridhika baada ya kuona, acheni kuangaza angaza huko na huko...kwani kabla hujaoa, nani alikuwa anakufanyia hayo yote?

Duh,hadi kufuli mtu afuliwe.....duniani kuna mambo!!!mmmhhhh tusaidiane kazi bwana.....na vitu kama kofuli,fua mwenyewe...ahhhhh:sick:
 
Mkuu hapa naona unatafuta excuse, ukiona kama ni kero sana basi tafuta Houseboy.

Ukigusa hapo huenda hata hiyo heshima unayopata sasa ikaisha wewe ndio ukaishia kuwanawisha wote mikono na kufua nguo

Noma Houseboy itakua ndio mpango mzima, bora kupambana nae ukawii mkuta house boy nae anafua master na mkeo....
 
Jinsia yangu haioneshwi na avatar....naweza kuwa mwanaume au mwanamke......

Pili umeshamshauri,asante sana.

Mhhhh! Michelle hapo penye nyekundu pameniacha hoi. Haya enjoy the rest of the weekend.

 
Tatizo kama hili limekuwa la kawaida sana kwa maisha ya mjini Dar...kisingizio kikiwa watu wanafanya kazi wanachoka. Nani kasema kwamba hizo kazi afanye mke? Suluhisho sahihi hapo ni kumuondoa housegirl na nyie wenyewe kugawana majukumu na kusaidiana.
 
nyie wababa na nyie mmezidi...
yaani ulitaka housegirl awepo na mkeo afanye kazi zote hizo???
sasa mliajiri housegirl wa nini???
kama kakunyima unyumba,au hajitengenezi ukirudi unamkuta yuko rough...ningeona basis ya malalamiko yako!
kwa sasa naona unatafuta tu excuse ya kutembea na huyo housegirl...shame on you!:twitch::twitch:

Thread ni kwa akina baba tu au vipi?
 
Pole sana kaka ila nasi wadada tukiolewa tunajisahau sana agrrrrrrrrr

Daaah, majibu ya wadada yameniacha hoi kweli ukiondoa jibu la Maria Roza

Wengine ndo hivyo aongezwe hausi boy . . .
Jamaa kashaeleza kwamba aliingia majaribu kwa kutamani ku-do na busara ikamuokoa, lakin naona bado watu wanakazania hapohapo USIM-DO kama vile mhusika kauliza am-do au la.

My friend pole kwa mkasa. Inaonekana wazi mkeo ni mama wa nyumbani wakati wewe ni mtafuta pesa za kulisha familia . . .
Naungana mkono na wale wote waliopendekeza ulipeleke suala kwa wakubwa, maana ni wazi kwamba mwanamke ni mvivu
 
Ofisini wanaitwa secretary, Bar wanaitwa Bar maid, Nyumbani wanaitwa House Girl; zote ni ajira tu kama ni edible kula vitu ruksaaa....caution - umeshindwa tumia cond**
 
Ofisini wanaitwa secretary, Bar wanaitwa Bar maid, Nyumbani wanaitwa House Girl; zote ni ajira tu kama ni edible kula vitu ruksaaa....caution - umeshindwa tumia cond**
Duh hii kali.........mkuu inaonekana wewe ni onja onja sana, angalia isije kukutokea puani.
 
kwa kweli huyo mke wako ni mvivu wa wavivu.Haaa jamani ndoa zina siri nyingi,mimi nikimpata ninaempenda,nitamuenzi hasaaaa,atajua faida ya kuwa na mke.labda ninasema kwa kuwa sina.Jamani wanawake wenye waume mjitahidi ili isiwe sababu ya m.me kutafuta wa pembeni,maana ndoa sio kitandani tu.Back to the topic,kama umeshamfahamisha hajakusikia,mtafute ndugu yake wa karibu mfahamishe yote usibakishe hata moja,kwani kuita ndugu naona kama ni aibu fulani,na huyo mke wako umwambie kama hatobadilika mwisho wake nitawaita ndugu.siyo mambo yote amwachie mfanyakazi,kama kufua kufuli afue mwenyewe,au chumba chake asafishe mwenyewe,au muonyeshe kimapenzi chumbani mwenu msafishe wote.
 
Kijana Juzi, nakupa pole kwa kufikia hatua hii lakini naamini bado mnaweza kushauriana na mke wako ili usifike huko unakotaka kuelekea.

Binafsi sina shida na house girl kufanya majukumu ya nyumbani kama ulivyoeleza lakini la kuwafulia nguo za ndani nafikiri siyo busara na hamumtendei haki huyu house girl. Wewe na mke wako mmeshindwa kweli hata kufua nguo hizi za ndani wakati mnapokuwa bafuni kama kweli mnaona hamna muda wa kufua?

Binafsi ninakaa na housegirl kama mdogo wangu wa kike na kwa sababu hiyo wazo la kufikiria kuwa siku moja naweza kulala na huyu housegirl au binti yeyote anayetusaidia kazi nyumbani naliondoa kichwani, nalikemea na kuomba Mungu anisaidie kuliepuka kwa gharama yoyote.

Hata hivyo najua wakati mwingine roho inakuwa radhi lakini mwili unakuwa dhaifu na hapa ndipo unapaswa kumwambia mke wako aache kutengeneza mazingira yanayoweza kukuingiza wewe majaribuni kwa yeye kuwa mbali na wewe na kumruhusu house girl kuwa karibu yako.

Lakini kwa habari ya kazi/majukumu ya nyumbani binafsi sina shida kwa kuwa na mke wako umesema ni mfanyakazi na mmeleta huyo house girl awasaidie. Kwangu shughuli zote ulizosema house girl anafanya isipokuwa hakanyagi kwenye chumba chetu kama ni binti ambaye ni ndugu anaweza kuruhusiwa kuchukua kitu chumbani kwa haraka i.e kuchukua mtoto anayelia au kupeleka mtoto kumlaza. Usafi wa chumbani tunafanya mimi na mke wangu.

Nakushauri na kukuombea epuka kukaribisha roho ya kulala na house girl, ni mbaya itakuharibu na kuharibu familia yako.
 
Hivi hawa wanawake walio kuwa wanajibu humu kubwa waliloliona ni jamaa kutaka kumnanilii hg....
Jamaa mkeo sio....
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom