Tujadili hatima ya soka ya Tz na makocha wazawa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujadili hatima ya soka ya Tz na makocha wazawa...

Discussion in 'Sports' started by Sajenti, Jan 22, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kuna habari kuwa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF hawataongeza muda wa mkataba wa kuifundisha timu ya taifa ya Tanzania kwa kocha Marcio Maximo utakapokwisha mwezi wa Juni. Hivyo shirikisho hilo linategemea kutangaza nafasi hiyo ili kuweza kupata kocha wa kuchukua mikoba ya Maximo.

  Juzi katika kipindi cha michezo TBC, kocha wa timu ya Manyema Rangers Abdallah Kibadeni "King Mputa" aliweka wazi kuwa yeye kama kocha mzawa ataomba nafasi hiyo kama mzawa kwa kuwa ana vigezo na uwezo wa kumaliza kiu ya watanzania kupata mafanikio katika medani ya soka la kimataifa.

  Pia kocha mwingine kutoka visiwani Zanbibar, Hemed Morocco ambaye aliiwezesha Zanzibar kushika nafasi ya tatu katika mashindano ya Challenge hivi karibuni naye alionyesha nia ya kuomba nafasi hiyo. Tanzania ina makocha wa soka wengi tu wenye sifa zinazotofautiana miongoni mwao. Mbali ya hao niliowataja hapo juu wapo pia watu kama Charles Boniface Mkwasa, Fredi Felix Minziro, Juma Mwambusi, Sunday Kayuni, Syllersaid Mziray, Salum Madadi na wengine wengi.

  Je tunadhani ili kupata mafanikio katika soka Tanzania inahitaji kocha wa aina gani? Kwani wazawa wamekuwa mstari wa mbele kuonyesha kuwa wanaweza kama watapata support aliyopewa Maximo, pia kuna makocha wa kigeni walionyesha pia nia ya kuitaka kazi hiyo....Nawasilisha.
   
 2. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2010
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  kwa maoni yangu mi bado napendelea apatikane kocha atakayekuja kuleta maendeleo zaidi na sio longolongo, hawa makocha wazawa sijaona kikubwa wanachokifanya ktk timu zetu za hapa nyumbani zaidi ya kutufanya tuendelee na mambo yetu yaleyale ya simba na yanga, kama kweli hilo la kufanya maajabu na timu ya taifa linawezekana nadhani lingeanzia huko walipo na sio kutoa sababu kuwa una vigezo au timu yako inashika nafasi nzuri kwenye ligi, hii ni timu ya taifa ambayo ipo kwenye mchakato wa maendeleo hakuna kubabaisha. Mi naona hawa wazawa bado coz hakuna nayemuona aliyefanya kitu kikaonekana, wengi wao leo wamefanya vzr kesho hamna kitu, so tukiruhusu hilo lifanyike tutaendelea kuguna na kutupiana lawama kila siku. Hakuna kocha ambaye yupo tayari kuacha hiyo nafasi coz kwa hali ya sasa mambo ya mshahara na wadhamini nao wapo juu, so kila mtu mwenye hiyo fani lazima atatoa macho huko, lakini je anafaa??? Kocha atoke nje hawa wazawa wanajua sana kutunga sababu wanapochemka, tunataka mabadiliko na sio kubahatisha.
   
 3. K

  Konaball JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,771
  Likes Received: 465
  Trophy Points: 180
  Mhh nyie ndio mkiumwa mnaenda kutibiwa nje amuwaamini madoctor wa hapa nchini ehh, kama kuna mzawa ana sifa za kufundisha wanazoziitaji TFF na apewe tu, tumeona hapa Timu zimeleta makocha kutoka nje kumbe ni mabomu!!!
  Nakupa mfano wa makocha wa hapa ndani waliowezeshwa na wakafanya vizuri. Mwaka 1993 Abdallah Kibaden aliwezesha Simba kufika fainal ya kombe la CAF, Simba wakati huo wakiwa chini ya Ufadhili wa Azim Dewji. Mwaka 1994 Mziray aliiwezesha Kilimanjaro Stars kubeba kombe la challange huko Nairobi wakati huo Kilimanjaro Stars ikiwa chini ya jopo la wafadhili kina AZIM DEWJ, MENGI, RAZA, MURTAZA DEWJI, Taifa Stars ikiwa chini ya kocha Mzee Kheri na Sunday Kayuni lilikuwa kidogo lifanikiwe kuipeleka Taifa Stars katika fainal za CAN mwaka 1996 nchi Africa Kusini isingekuwa kuongezewa kocha kutoka Brazil wakati huo Taifa Stars ikiwa chini ya ufadhili wa jopo ilo nililolotaja hapo juu!!
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
Loading...