Wanasimba Mmeyakubali Maisha Bila Soka Biriani?

Best Daddy

JF-Expert Member
Apr 2, 2019
769
1,292


Siku moja nikiwa naangalia Soka pale Gentlemen Sports Lounge (Sinza) huku najipongeza kidogo baada ya mihangaiko ya hapa na pale, nilimsikia jamaa mmoja meza ya pembeni akisema "Hii siyo Simba naijua mimi, Sisi hata tukifungwa ila tukiwa tumepiga soka safi "Sexy football au pira biriani basi tunafurahi" akarudia tena akisema "Sisi bora hata tufungwe (..tusi) ila kikubwa tucheze vizuri.

Well, nikavunja ukimya na kumuuliza ya kweli hayo mzee? akatoa maelezo mengi ila nilichagua kutomuelewa.

Ila point kubwa aliyoitoa, ni kuwa hii ndiyo falsafa ya Simba. Hata moja ya sababu ya yeye kuipenda Simba basi ilikua ni aina ya uchezaji wake. Hili sikumpinga kabisa maana kwa miaka niliyoishi duniani niliitambua Simba yenye "Sexy Football" na sio pira haram au direct football.

Ila ghafla mambo yalibadilika nilipoona amekuja Zolan, oh nikajua labda Scout haikutambua huyu ni Kocha wa mifumo ipi, nikajua ni Mistake ya Scout, akaondoka zake. Hofu tena ikatanda baada ya kumuona Robertinho, basi akajipa umaarufu na pira lake "Objective", mengi yalisemwa ila bado kichaka cha pira objective kilifunika baadhi ya vilio vya mashabiki wanaotaka pira biriani. Ni wakati pekee nilimsikia "Mangungu" akizungumza msemo wa lugha ya kidunia na nitanukuu "If you try to please everyone, you'll please no one". Hii kauli aliitoa baada ya mashabiki wakisema wanashinda ila hawana furaha, huku akimaliza na kusema kama unataka furaha katafute mchezo mwingine( Hii kauli imetolewa kwa ajili ya kujazia nyama tu katika uzi huu, haina tafsiri ya kuleta tofauti ya Mangungu na mtu yeyote yule)

Basi, baada ya kuondoka Robertinho nikashaanga Makocha wengi wanao-husishwa kufanya mazungumzo na Simba ni aina ya makocha wenye sifa ya "Haram Ball" ambayo ni sifa tofauti na Sexy football au pira biriani?

Swali kuu nikajiuliza, hivi wanatambua nature ya wachezaji wao? Ila nikatambua Sio mbaya labda huu ni wakati wa mpito, kuna dirisha dogo.

Hatimaye ametangazwa ABDELHAK BENCHIKA. Ni kocha mwenye CV kubwa. Ni kocha anayepokea pesa ndefu(Zaidi ya 80M(TZS). Sio rahisi kwa Club zetu kuwa naye. Naamini hadi anakubali kuchukua timu ni mengi yamezungumzwa, au bosi(Mo) ameamua kumleta mwenyewe. Lakini wanasimba, mmekubali kuishi maisha bila pira biriani?

Au ndiyo unamchukua "Jose Morinho" alafu baadae unamdai Sexy Football? Man, anaweza akakutukana.

Binafsi, timu inatakiwa icheze soka safi(Kwa ajili ya kuvutia/kufurahisha Mashabiki) na ipate matokeo chanya (kwa ajili ya maendeleo ya Club). Ila kama umeshindwa kupata vyote kwa pamoja, ukapata nafasi ya kuchagua soka safi au matokeo.
Kama Kocha chagua matokeo, furaha ya soka safi haidumu kama hakuna matokeo chanya.

Je mwanasimba, upo tayari kuishi bila pira biriani?​
 
Ehh timu iko sokoni
Mooh anasubiri maokoto🤣🤣
Waondoke wazee kina Boko,kapombe,chama,Mohamed husen,inonga ,timu iundwe upya
Na ukubali muda wa kuwatengeneza vijana waive kisha waelewane!

Hivi timu nyingi zinazotawala soka kwenye ligi zao, wastani wa umri wa wachezaji wao huwa inakuaje? Vijana?

Nakumbuka, timu kama Arsenal, mara ya mwisho kubeba ligi, haikuwa timu ya vijana
 
Na ukubali muda wa kuwatengeneza vijana waive kisha waelewane!

Hivi timu nyingi zinazotawala soka kwenye ligi zao, wastani wa umri wa wachezaji wao huwa inakuaje? Vijana?

Nakumbuka, timu kama Arsenal, mara ya mwisho kubeba ligi, haikuwa timu ya vijana
Hamna timu imejaa wastaafu
Wazee wa ndumba
Waondoke tuanze na vijana kina chilunda et al
 
Kila timu Ina tamaduni zake na falsafa zake Aina ya wachezaji waliokuwa wakisajili ni wale waliokuwa wakiendana na falsafa hizo.
Yanga walikuwa wanasifika toka zamani kuwa na mawinfa hatari toka enzi za kina Omary Husein mpaka Sasa.
Mpira wa Simba unaeleweka Ila kwa sababu Simba imevamiwa na watu wasiojua utamaduni wa Simba haya ndio matokeo yake.
Hata uchaguzi wa makocha ulikuwa ukiendana na uchezaji wa Simba.
 
Back
Top Bottom