kimarabucha
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 791
- 621
WADAU naomba tujaribu kujikita kwenye mada tajwa hapo juu kwani nimemsikia Waziri Wa Ardhi Mh.Lukuvi sikuamini Bunge kuwa Wizara yake inatunga Sheria ya kuwataka wenye nyumba wachukue kodi ya kila mwezi badala ya miezi 6 au mwaka.Hoja yangu ni je ni faida gani au hasara atakayoipata mwenye nyumba/Mpangaji Kwa Sheria mpya ya upangaji? Je ni faida/hasara gani Kwa Sheria ya Kulipa Kwa miezi 6/Mwaka anayoipata mpangaji/mwenye nyumba ?
Ngumu, kikubwa tupambane na hali zetu hatimae tujenge za kwetu. Usimuamin mwana siasa hata siku 1anakataa
Hahahaha sawa mkuuNgumu, kikubwa tupambane na hali zetu hatimae tujenge za kwetu. Usimuamin mwana siasa hata siku 1
Kwanini isiingilie?Makubaliano/Mktaba ya mpangaji na mwenye nyumba huwa ni baina yao serikali inawezaje kuingilia. Hawa mawaziri watafakari kabla hawajatoa sheria zisizoeleweka.
Kwa sheria ikipita tutegemee wapangaji wengi watapewa notice.
Inawezekana lkn one at a time.Shule nazo ziambiwe hivyo ili ngoma iwe droo! Karo iwe mwezi mmoja mmoja badala ya muhula.
Nyumba za kupangisha siku hizi ni biashara, kwa hiyo hata ile kodi ya "property tax" inazingatia hilo. Tatizo la wanasiasa ni "kiki" wengi wao wana miradi mikubwa ambayo inawawezesha kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kulipa ada za vyuo vikuu wanao, kufanya matengenezo ya nyumba zao bila wasiwasi kwani wanapokea fedha mamilioni, Je huyu mwenye nyumba anayepokea shilingi laki 2 kwa mwezi,anahitaji kusubiri miezi mitatu kukusanya fedha ili aweze kufanya jambo kubwa, wakati huo huo anahitaji kula, matibabu na mengine mengi. Sheria hii naifananisha na ile ya Mafao ya kujitoa katika mifuko ya kijamii. Ni wakati sasa kuwa na viongozi wanaosaidia wananchi kupata maendeleo na sio kutafuta njia ya kupata kura kama ile aliyotumia mugabe ya kupora mashamba ya wazungu kwa ajili ya kupata kiki ya kisiasa, madhara yake yanaonekana. Mimi nasema hivi kama NSSF na PPF wanaweza kujenga maghorofa, basi wajenge na nyumba za kupangisha kwa kodi ya kila mwezi, lakini serikali kuwapangia wanye nyumba kupokea kodi kwa mwezi ni adhabu kubwa sana kwa wenye nyumba. Nitashangaa endapo umoja wa wamiliki wa nyumba za kupanga hawatapinga sheria hii mahakamani.sheria itafanya biashara ya ujenzi wa nyumba za kupanga kutokuwa na faida.
haiwezekani kujenga nyumba kwa milioni 30 halafu upokee kodi ya laki 2 kila mwezi.. lini fedha itarudi.
lakini italeta unafuu kwa wapangaji ule mzigo wa kulipa 3.6m stress zake hazikuwa za kawaida
Wakati wanajenga nyumba zao walipata Ruzuku kutoka serikalini?Kwanini isiingilie?
Sio lazima wakupe ruzuku serikali lazima iregulate baadhi ya mambo.Wakati wamejenga nyumba zao walipata Ruzuku kutoka serikalini?
✅Nyumba za kupangisha siku hizi ni biashara, kwa hiyo hata ile kodi ya "property tax" inazingatia hilo. Tatizo la wanasiasa ni "kiki" wengi wao wana miradi mikubwa ambayo inawawezesha kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kulipa ada za vyuo vikuu wanao, kufanya matengenezo ya nyumba zao bila wasiwasi kwani wanapokea fedha mamilioni, Je huyu mwenye nyumba anayepokea shilingi laki 2 kwa mwezi,anahitaji kusubiri miezi mitatu kukusanya fedha ili aweze kufanya jambo kubwa, wakati huo huo anahitaji kula, matibabu na mengine mengi. Sheria hii naifananisha na ile ya Mafao ya kujitoa katika mifuko ya kijamii. Ni wakati sasa kuwa na viongozi wanaosaidia wananchi kupata maendeleo na sio kutafuta njia ya kupata kura kama ile aliyotumia mugabe ya kupora mashamba ya wazungu kwa ajili ya kupata kiki ya kisiasa, madhara yake yanaonekana. Mimi nasema hivi kama NSSF na PPF wanaweza kujenga maghorofa, basi wajenge na nyumba za kupangisha kwa kodi ya kila mwezi, lakini serikali kuwapangia wanye nyumba kupokea kodi kwa mwezi ni adhabu kubwa sana kwa wenye nyumba. Nitashangaa endapo umoja wa wamiliki wa nyumba za kupanga hawatapinga sheria hii mahakamani.