Nadhani wabunge wanastahili kuelewa kuwa kila mtu ktk biashara ana malengo yake. Biashara ya kujenga nyumba na kupangisha ina malengo yake mhusika. Huwezi kunilazimisha nipokee kodi kwa mwezi kwasababu siyo mipango yangu ktk biashara yangu. Kama serekali inataka ijenge nyumba nyingi hata ikitaka kukodisha na kupokea kodi ya nusu mwezi ni hiari yake. Jamani wenzetu nchi nyingine wamepiga hatua zaidi. Na serekali zao zinawasaidia na siii kuwadidimiza. Nilipanga chumba kimoja pale Bangalo India. Nililipa kodi ya mwaka mmoja na fedha ya tahadhari $300 (fedha ya tahadhari hapa kwetu Hakuna) fedha hii inatumika pale mkataba wako utakapokwisha ilikupiga rangi na kurudishia vifaa ambavyo vimeharibika wakati wewe ukiwa mpangaji. Hapa kwetu hilo halipo. Biashara hururia iwe huria kweli. Wabunge wajadili hoja za maana zidi.