Tuipende nchi yetu, tuwe Wazalendo

alumn

JF-Expert Member
Jul 15, 2018
2,366
3,109
Tusali ndugu zangu. Kama kuna sehemu tumemkosea Mungu/ Allah atusamehe. Sio kwa ubaya ndugu zangu na nisieleweke vibaya.

Tuombe hofu ya Mungu itawale kwa watu wote, upendo, uwajibikaji. Muhimu hofu ya mungu itawale. Utawala bora uwe huru na haki kwetu sote.

Ndugu zangu tusali kwa imani zetu ili nchi yetu iwe na ustawi bora wenye kujali utu, uadilifu, matumizi bora ya rasilimali kwa watu wote na kwa usawa usio na mawaa.

Ni muhimu na ni vyema kukumbushana. Tusali sana ndugu zangu watanzania. Mambo mengi yanayoendelea yanahitaji mkono wa mungu uonekane.

Nasema hivi mwenye sikio na asikie. Tuipende nchi yetu, tuwe wazalendo na tuchape kazi. But tusali.

Ameen
 
Kuipenda nchi yako ni pamoja na kusema kweli kuhusu maovu mbali mbali yanayoendelea nchini yakifanywa na Serikali haramu ambayo haikupewa ridhaa na Watanzania bali ilipora uchaguzi.

Maovu hayo ni pamoja na kubambikia kesi FEKI, uporaji wa pesa na mali nyingine za Watanzania sehemu mbali mbali nchini, kuminya uhuru wa raia, vyama vya siasa, vyombo vya habari, kugomea Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi pia mauaji.
 
Kupendwa kwa nchi kunategemea wale waliopo madarakani wanatumia vipi nyadhifa zao kuboresha maisha ya raia wake. Sasa kwetu toka kupata uhuru bado.

Raia kukosa maji na umeme wa uhakika.

Huduma za afya na elimu bado duni sana.

Ustawi wa jamii kwa watoto yatima, wazee, vilema na kina mama ni kama hakuna. Sheria kubana na kukusanya kodi toka kwenye makampuni makubwa kutokusimamiwa vyema na kufanya dola kuendelea kutoza vijisenti toka kwa raia wake na kuendeleza umaskini.

Fujo na ufisadi wa rasilimali na maliasili ya taifa kutumiwa vibaya na viongozi kwa visingizio vya usalama kwa viongozi na matumizi mabaya ya viongozi mpaka kuonekana kuishi kifalme huku raia akihangaika kupata mlo mmoja kwa siku.

Matumizi mabaya ya fedha kwa manunuzi ya vitu visivyo na faida kwa raia kutokana na viongozi kuziba masikio na kufumba macho kelele na matatizo yanayomkumba raia.

Vyombo vya usalama kwa makusudi kunyima haki raia. Kutokana na hayo viongozi kuzidisha woga na kujilimbikizia mali na kitumia rasilimali za nchi kwa kujilinda kama tuko vitani!

Nauliza hapo utapata uzalendo na mapenzi toka kwa raia?
 
Back
Top Bottom