donlucchese
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 17,042
- 21,517
Salam wakuu,
Straight to the point. Nimekaa sehemu flani hapa wanapaita Bambalaga, Dj amegonga magoma ya amapiano hapa watu wote wamewehuka kwa vishindo vya magoma. S.A kiukweli wameweza kupenetrate muziki wa kimataifa kwa mtindo wao (midundo yao).
Wakiwa Ni waanzilishi wa mtindo wa kwaito, wasanii wa bongo walifanya sana kwaito kipindi hiko kujaribu kucope na wasauzi Ila Sina kumbukumbuku sahihi kama kuna waliotoboa thru kwaito music. Wamekuja sasa na huu mtindo wa amapiano ambapo mpaka sasa unatikisa dunia na kufanya na baadhi ya wasanii wa bongo wajiongeze.
Kwa sasa kuna ngoma za kutosha za amapiano za wabongo na zinatikisa sana (pengine kuwazidi waanzilishi wenyewe). Ngoma kama bia tamu, waiona hiyooo, ticha, nikilewa etc
Ukisikiliza kwenye spika za maana lazima ukubali. Wanaijeria pia wana identity yao wamejitengezea (japo kama wanafanana na WA Ghana). Ukisikiliza rythm ya wimbo unajua tu mapema wacongo ndio usiseme.
Nauliza kwanini singeli ambayo inatutambulisha wabongo isiende kimataifa? Enzi za mnanda kina marehemu Juma Mpogo, Jenero Lopozi, Seven Survivor, Jagwa waliupeleka mziki kimataifa. Jagwa mepiga shoo nyingi za mnanda ulaya ukichek wazungu wanavyopagawa huwezi amini. Maoni yangu, singeli hii ikiboreshwa na kuongezewa vionjo inaweza fika mbali sana. Angalia Alicia keys alivyokua anaserebuka na ngoma ya wanga wabaya ya Meja kinda.