Safari_ni_Safari
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 23,265
- 17,123
Katiba yenyewe hii hapa http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf
Mimi naanzia kwenye utangulizi.
Hivi tuliamua lini haya na tuliamua vipi?Tulipiga kura au?Mimi sikumubki kushiriki
Halafu hapo nilipo underline mbona hapaeleweki
Sheria ya 1984
Na.15 ib.3
KWA KUWA SISI Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi
yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na
amani:
NA KWA KUWA misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika
jamii yenye demokrasia ambayo serikali yake husimamiwa na
Bunge lenye wajumbe waliochaguliwa na linalowawakilisha
wananchi, na pia yenye Mahakama huru zinazotekeleza wajibu
wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo
kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na
kulindwa, na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa uaminifu:
KWA HIYO, BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BUNGE
MAALUM LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii
kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Tanzania
inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia
na ujamaa.