Tuifanye Tanzania Taifa la Wajasiriamali-Risk Takers

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,490
5,525
Najua kuna watakao elewa hili ni kuna ambao hawataelewa hili;

Kama taifa inabidi wakati tuamue kama taifa tunataka kuwa taifa la namna gani,Je tunataka kuwa taifa la walalamishi,walaumuji,wajutaji na watu tusio na mbele wala nyuma au tunataka kuwa taifa la watu jasiri waleta mabadiliko waota ndo na watafutaji wa fursa?

Je tunataka kuwa taifa la mashabiki watu wasiokuwa na ndoto wala wasiofanya makubwa katika taifa na dunia?Lazima tuamue sasa kwamba tunataka kuwa taifa la namna gani.

Uamuzi huu kuufanya ni jambo rahisi sana ila kuutekeleza ni jamba ambalo linahitaji nguvu kubwa sana kwa mtu binafsi,familia na jamii kwa ujumla.Mtu binafsi lazima aamue kwamba yuko tayari kuchukua hatua kuboresha maisha yake binafsi na maisha ya familia yake kwa ujumla,mfano rahisi ni huu hapa.

Kwa utafiti niliofanya kiasi cha Pesa ambacho hupotea kila mwaka katika matumizi yasiokuwa na tija uwekezaji usiokuwa na tija,mapato ya kodi yasiyokuwa na tija na upotevu wa rasilimali ungeweza kuhakikisha kila mtu anaishi maisha ya kiwango cha kati yaani kupata milo mitatu,malazi bora na kuwa na huduma bora ya afya ila kutokana na mfumo ubovu wa kijamii na utamaduni mbaya kiasi kikibwa cha rasilimali pesa na rasilimali watu hupotea katika mamba yasokuwa na tija yoyte.

Kama taifa tunaweza kuamua namna bora na hatua bora za kuchukua ili kufikisha taifa letu katika kiwango cha maisha tunachotaka kwa watoto wetu kwa kuanza na hatua ya kwanza ambayo ni kujenga mfumo madhubuti wa kijamii nakiuchumi.

Je ni kwa namna gani na ni maeneo gani ambayo tukiyafanyia kazi tunaweza tengeneza taifa la wajasiriamali na wapambanaji waleta mabadiliko?

Tujadili
 
Back
Top Bottom